Cyprian Musiba: Sasa nitafia kwenye siasa!

Cyprian Musiba: Sasa nitafia kwenye siasa!

Makao Makuu

Member
Joined
Aug 28, 2016
Posts
7
Reaction score
4
musiba.jpg

Mtangazaji wa zamani wa runinga ya Channel Ten na radio za Magic FM na Clouds FC, Cyprian Musiba (38), amesema kwamba sasa maisha yake amejikita kwenye siasa na yuko tayari kufia huko.

Mwanahabari huyo ambaye mbali ya kufanya kazi kwenye runinga na radio lakini pia amepata kufanya kazi katika Idara ya Habari na Uhusiano (IPR) katika Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi, amesema licha ya kuendesha shughuli zake binafsi za habari kwa sasa lakini anaona ni vyema ajikite kwenye siasa ambayo iko ndani ya damu.

“Nimeshafanya kazi katika vyombo vya habari vya binafsi lakini pia nimefanya serikalini, lakini moyo wangu unaendelea kunisukuma nizame kwenye siasa, hivyo bora niende huko kwa vile nimezaliwa na kukulia katika mazingira ya siasa,” anasema mwanahabari huyo ambaye amepata kumiliki gazeti la Afrika Leo.

Anasema pia kwamba, kwa sasa anajipanga kuwania uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) licha ya kushindana mara kadhaa na kushindwa.

Itakumbukwa kwamba, mwanahabari huyo, ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya CZ Information and Media Consultants Limited, aliwahi kugombea mara mbili ubunge wa Jimbo la Mwibara wilayani Bunda, lakini mara zote alishindwa na mbunge wa sasa, Alphaxard Kangi Lugola katika miaka ya 2010 na 2015.

Mwaka 2012 aliwania ujumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM, lakini akashindwa na katika uchaguzi wa CCM wa mwaka 2012 aliwania Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kutokea wilayani Bunda, ambapo alipata kura 996 akishika nafasi ya pili nyuma ya M-NEC Boniface Gitare aliyepata kura 1,001.

“Kura hazikutosha wakati ule, lakini siasa ndiyo maisha yangu, siyo kwa sababu nilishindwa ndipo niachane na siasa, ninaendelea na nitafia huko,” alisema na kuongeza kwamba anashukuru kuona Dk. John Magufuli amekabidhiwa uenyekiti na sasa lile wimbi la rushwa na michezo michafu ambayo ilikuwa inalalamikiwa linaweza kuondoka na chama kitaimarika.

Musiba alizaliwa mwaka 1978 huko Bunda na elimu yake ya msingi aliipata katika Shule ya Msingi Luhwaji kabla ya kujiunga na sekondari ya Ifunda Technical iliyoko Iringa. Baadaye akajiunga na kidato cha tano katika Shule ya Sekondari Ihungo mkoani Kagera.

Kati yam waka 2000 na 2003 alisomea stashahada ya Uandishi wa Habari katika Chuo cha Dar es Salaam School of Journalism (DSJ). Shahada yake ya Mawasiliano ya Umma aliipata Julai 2016 katika chuo cha Kenya Institute of Mass Communication.

Amepata kufanya kazi katika Idara ya Habari na Uhusiano ya Jeshi la Wananchi ambako aliondoka mwaka 2005. Baada ya hapo akajiunga na African Media Group Ltd (Radio Magic FM na Channel Ten TV) ambapo alikuwa mtangazaji na mwandaaji wa vipindi mbalimbali vikiwemo vya michezo, taarifa za habari na mhariri wa michezo wa Magic FM.

Aliondoka mwaka 2012 na kuendesha gazeti lake binafsi la Afrika Leo lakini mwaka 2014 akajiunga na kampuni ya Vision Broadcasting Limited (Tumaini International) (CTN TV) ambako ndiko aliko hata sasa akiwa mhariri mkuu wa habari, mtangazaji na mwandaaji wa vipindi.

Japokuwa ni mahiri katika habari za mazingira, lakini mwanahabri huyo amejipatia umaarufu mkubwa kutokana na uchambuzi wa michezo, hususan mpira wa miguu. Ameripoti mashindano mbalimbali ya moja kwa moja (live coverage).

Habari za siasa ndizo zinazoonekana kuchukua nafasi kubwa kwake licha ya utashi wake kwenye mpira, kwani ndiye alikuwa mwandishi wa kwanza kuwahoji ‘live’ baadhi ya viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) waliokuwa wamekwenda kutafuta hifadhi katika Ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam Aprili 2008 wakitaka Kisiwa cha Pemba kijitenge na Zanzibar kwa sababu walikuwa wanadhalilishwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Ripoti hiyo ya moja kwa moja ya viongozi hao wa CUF ilirushwa na runinga za Channel Ten na DTV.
 
Kumbe amewahi kugombea mara nyingi hivo na kupgwa chini!

Akitaka ashinde ahame kuishabikia club yake ya Arsenal chn ya kocha wake Wenger (Specialist for failure) other wise nayeye ataendelea kuwa Specialis for failure kama alivyo kocha wao.
 
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] kumbe ndio wale wale wa majipu
 
Kupata nafasi kwenye chama cha magamba hadi urefushe mkono kwa wajumbe. Ni jamaa fulani hivi ndo alipata zali baada ya timu Membe na timu mzee wa mafuriko kukwaruzana. Sasa sijui ndg Cyprian umejipangaje maana inaoekana una damu ya kunguni.
 
Its only in Tanzania where politiks is a carrier. Hata donald trump hajawahi kula hiko kiapo.akikosa uraisi atarudi street.
 
Back
Top Bottom