Mimi ni mmojawapo wa waliojitokeza kuomba. Utaratibu uliokuwepo ni kwamba unapeleka barua kwa katibu wa wilaya. Kuna form maalum za kuangalia vigezo na unapewa alama(marks) mfano uliwahi kuwa mwakilishi wa tawi au kiongozi wa wilaya unapewa alama, una diploma, digrii au cheti unapewa alama. Baadaye form hizo zinachambuliwa kuonyesha waliopata alama za juu. Zinapelekwa mkoani zote(waliopata alama za juu na za chini). Mkoani nao wanazipitia kuangalia kwanini huyu amepata alama za juu au za chini. Nao wanafanya mchakato huo huo. Kisha zinapelekwa Taifani na katibu wa mkoa. Kule kuna watu wanaitwa KUT (kamati ya utendaji ya taifa) ndio wanaofanya short listing na baadaye interview. Ukipenya hapo unakula shavu.
NB:
Mfumo huu unawabeba zaidi viongozi kuliko walimu wa kawaida. Hii ni kwasababu wanapata alama nyingi zaidi kuliko blackboard teacher. Huu ndio uelewa wangu. Naomba kuwasilisha.