CWT na serikali wote wagomewe na walimu

Felixonfellix

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
1,672
182
NA, GORDON KALULUNGA


NIWEKE wazi kuwa huu si uchochezi bali nataka niweke ukweli ambao ni sawa na juisi ya Mwarobaini ambayo ni chungu lakini inaponya homa kali.

Hivi karibuni viongozi wa chama cha walimu Tanzania (CWT) katika mikoa na wilaya wameunga mkono kile kilichoitwa mgomo wa walimu nchi nzima unaotarajiwa kutangazwa na Rais wao Gratian Mukoba mwezi huu Julai 2012.

Wakati CWT kinawahamisisha na kuwaandaa walimu kwa ajili ya kugoma, jambo moja la msingi ambalo walimu wanatakiwa kujua kwa undani zaidi ni kujua haki zao mbalimbali ambazo CWT chenyewe kwa ubabe na kwa kuvunja Katiba na sheria za nchi kimekuwa kikiwanyang’anya walimu kwa miaka yote 17 ya uhai wake. Pia CWT kimekuwa kikishirikiana na serikali katika kuwakandamiza walimu nchini kwa ushahidi ufuatao:-
Kwanza kabisa, CWT imeshirikiana na Serikali kuandaa waraka wa Siri wa serikali wenye namba C/AC.44/45/01/A/84 ambao ulikuwa unawakandamiza walimu wote wanaojiendeleza kielimu nchini kwa kuwashusha vyeo na mishahara badala ya kuwapandisha kama inavyotakiwa.

Baada ya hapo baadhi ya walimu walijitoa muhanga na kupigania haki zao hasa wale waliojiendeleza ambapo waliungana nchi nzima na kuanzisha chama chao kipya kinachojulikana kwa jina la UMET.

UMET imepigania haki ya kutaka kufutwa waraka huo ambapo mchakato huo ulizaa matunda tarehe 14/12/2011 baada ya UMET kufika Ofisini kwa Waziri Mkuu tarehe 12/12/2011, Ikulu tarehe 14/12/2011 na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma mara mbili yaani tarehe 05/12/2011 na tarehe 14/12/2011.

CWT kwa makusudi ya kuua mafanikio ya walimu wanaojiendeleza hapa nchini kwa hofu ya kukimbiwa na walimu, kimeshirikiana na serikali (Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma) katika kuandaa waraka mwingine kwa lengo la kuendelea kuwakandamiza walimu wote wanaojiendeleza kielimu nchini wenye namba CAC.44/45/01/A/121 wa tarehe 20/12/2011 ili walimu wote wanaojiendeleza kielimu nchini waendelee kukandamizwa kwa kupewa vyeo vya majina tu lakini wasipewe vyeo vya madaraja ya mishahara yao kama wanavyostahili.

Waraka huo kandamizi una mruhusu mwalimu Y ambaye hajajiendeleza kielimu apande daraja la mshahara kutoka TGTS D na kwenda TGTS E. lakini mwalimu X ambaye amejiendeleza kielimu ataendelea kubakia na mshahara wa ngazi ya TGTS D kwa miaka mingine mitatu ila badala yake apewe cheo cha jina tu.

Yaani kama alikuwa ni mwalimu wa daraja la IIIA sasa aitwe Afisa Elimu Msaidizi kama amejiendeleza kwa kiwango cha Diploma au aitwe Afisa Elimu daraja la II kama amejiendeleza kwa kiwango cha Degree.

CWT kilishiriki katika kuandaa waraka huo kuanzia tarehe 17/12/2011. Pia CWT kikausambaza waraka huo haraka sana nchi nzima kwa kuwatumia makatibu wake wa Mikoa na Wilaya kwa barua yake yenye kumbukumbu namba CWT/004/MM/VOL.II/208 ya tarehe 30/12/2011 iliyosainiwa na Naibu Katibu Mkuu wake Ezekieli Oluoch yenye kichwa cha habari kinachowahadaa walimu kwa kusema “ Shukrani, salaam za mwaka mpya na taarifa ya kufutwa kwa waraka kandamizi”. Waraka huo kandamizi bado upo na unaendelea kuwakandamiza walimu nchini.

CWT kinawagawa walimu ili kiendelee kuwaburuza na kuwaandamanisha vizuri kwa kuandaa muundo mpya wa mishahara ya walimu wa vyuo vya Ualimu kwa kuwabagua walimu wa shule za msingi na sekondari dhidi ya walimu wa vyuo vya ualimu na hilo lilifanyika tarehe 30/06/2011.

Waraka huo ulianza kutumika upesi tarehe 1/7/2011 hata kabla haujachapwa na mpiga chapa mkuu wa serikali. Kwa mfano kama kuna walimu wawili mwalimu X na mwalimu Y wanasoma Chuo kikuu kimoja, mwaka wa masomo mmoja kundi la kujisomea (group discussion) moja na wakahitimu pamoja na kuajiriwa pamoja katika taasisi mbili tofauti za serikali.

Mwalimu X akiajiriwa shule za msingi au shule za sekondari ataitwa Afisa Elimu daraja la II na ataanza na mshaahara wa Tsh. 400,000/= (TGTS D) wakati mwalimu Y akiajiriwa kwenye vyuo vya ualimu ataitwa Mkufunzi wa Chuo na ataanza na mshahara wa Tsh. 600,000/=(TGTS E).




Nayasema haya ili kuweka kumbukumbu sahihi kwa walimu ili kauli ile ya Rais Jakaya Kikwete aliyowahi kuitoa kwa wafanyakazi wote kuwa jambo la kuambiwa changanya na la kwako liweze kutimia na kuachana na migomo ambayo inalenga manufaa ya baadhi ya vinara ambao mara kadhaa wanakutana na Serikali na kugonga bilauli.

CWT kilishiriki kuyakataa madeni halali ya walimu kwa mujibu wa sheria zinazotawala utumishi wa Umma ((Public Service Act 2002 and Regulations 2003) kifungu cha 103, kidogo cha 1 na 2, Standing Orders kifungu G.16(a), kifungu G.32 kifungu kidogo cha (a) na (b), kifungu G.17 na kifungu G.35 kifungu kidogo cha (a) na (b), kifungu G.36 pamoja na mpango wa Utumishi wa Walimu (Teachers’ Service Scheme – 2008) kifungu cha 41), wakati wa kuhakiki madeni ya walimu nchini ambayo ilidaiwa kuwa yalifikia bilioni 49.6.

Kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya nchini na kwa kupitia makatibu wa CWT wa Wilaya, CWT kiliyakataa madeni ya walimu waliokuwa wamejiendeleza kielimu katika ngazi ya Degree na Masters. Makatibu hao wa CWT walikuwa ni miongoni mwa jopo la watu watano (5) waliokuwa wanahakiki madeni hayo kila Halmashauri nchini.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 ibara ya 20 pamoja na sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini namba 6 ya 2004, kifungu cha 9, zinazungumzia juu ya uhuru kila mtanzania na hususan mfanyakazi wa kujumuika na wenzake, uhuru wa kujiunga na kuanzisha vyama na vikundi kwa lengo la kulinda na kutetea imani, haki na maslahi.

Pia kifungu cha 60 kifungu kidogo cha 1 kinasema mwajiri atakata fedha kutoka kwenye mshahara wa mfanyakazi na kuziwasilisha kwenye chama cha wafanyakazi kilichosajiliwa kama mfanyakazi ataruhusu kwa maandishi ili makato hayo yafanyike kwenye mshahara wake.

CWT kimekuwa kikivunja Katiba na sheria za nchi kwa kuwafanya walimu wajiunge na CWT kwa shuruti na kukata mishahara ya walimu wengi bila idhini yao.

Kifungu cha 60 kifungu kidogo cha 4 cha sheria hiyo kinasema hata kama mfanyakazi (mwalimu) alikuwa ameruhusu makato kufanyika kwenye mshahara wake bado anayo haki ya kuahirisha na kutengua maamuzi hayo kwa kutoa taarifa ya maandishi ya mwezi mmoja (siku 30) kwa mwajiri na kwa chama (CWT) na makato hayo yasitishwe mara moja mara siku 30 zitimiapo.

Walimu wengi wamekuwa wakiandika barua za kuwataka waajiri (wakurugenzi) na CWT kuacha kukata mishahara yao mara moja lakini CWT kwa ubabe kimekuwa hakitaki kufanya hivyo kwa kisingizio cha Agency Shop Agreement.

Kifungu cha 72 cha sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini namba 6 ya 2004 kinafafanua juu ya Agency Shop Agreement kuwa ni mkataba anaoingia kwa hiari mfanyakazi (mwalimu) ambaye hataki kujiunga na chama cha wafanyakazi (CWT) juu ya malipo ambayo mwalimu huyo atakilipa CWT endapo kuna manufaa atakayoyapata mwalimu huyo kutokana na kazi ya CWT.

Na mkataba huo ni lazima usainiwe na mfanyakazi(mwalimu), mwajiri (mkurugenzi), chama (CWT) na shuhuda mwingine atakayeshiriki katika mkataba huo na kila mmoja atakuwa na nakala ya mkataba huo.

CWT hakijawahi kuingia mkataba wowote wa Agency Shop Agreement iwe kwa shuruti au kwa hiari na mwalimu yeyote. Hata kama kingeingia kilipaswa kulipwa ada hiyo na walimu ambao wangekuwa tayari wamefaidika na kazi yoyote. Walimu wengi hawajawahi kupata manufaa yoyote kutokana na uwepo na kazi za CWT na kila wanapopata kero wanaparangana wenyewe, je hapa nani agomewe, Serikali au CWT?


CWT kimepoteza mwelekeo kwa kuacha kumpigania Mwalimu wa Tanzania na badala yake kimemfanya mwalimu kuwa ni kitega uchumi na msingi wa vitega uchumi vingine kama vile Mwalimu House, majengo ya ghorofa zisizopungua mbili kila mkoa kwa nchi nzima, nk.

Viongozi waandamizi na watendaji wakuu wa CWT walishaacha kazi ya ualimu serikalini na wamepeana ajira kwa kujuana ndani ya CWT na wanalipana mishahara minono na wakiumwa wanapelekana nje ya nchi kama wanavyofanya viongozi wa serikali.

Kwa hiyo kero za walimu siyo kero za viongozi wa CWT kwa kuwa wao si walimu kwa kazi zao. Hivyo kumpigania mwalimu kwao ni sawa na kumpigania mtoto wa jirani ambaye ni yatima kitu ambacho ni sawa na usamaria wema na siyo wajibu wa lazima.


CWT kimekiuka lengo la awali la kujenga kitega uchumi cha Mwalimu House ambalo lilikuwa ni kukusanya fedha ili siku ikitokea kuwa walimu wanagoma na serikali ikawatishia kwa kuwanyima mishahara wangeweza kuendesha mgomo na kujilipa wenyewe mishahara kama wanavyofanikiwa walimu wa Kenya.

Mpaka kufikia mwezi Septemba 2011, CWT kilikuwa kinakusanya zaidi ya Tsh. Bilioni 40 kwa mwezi kutokana na vitega uchumi na makato ya mishahara ya walimu, kuna usiri mkubwa juu ya mapato na matumizi ya fedha za CWT. Wamenogewa na utamu wa fedha sasa wanaanzisha Benki ambayo kwa jina itaitwa Benki ya walimu pasipo kuwashirikisha walimu, kujenga maghorofa kila mkoa bila kuwashirikisha walimu, kuanzisha na kuendesha Kampuni ya kibiashara inayoitwa Teachers Develoment Company Limited iliyoanzishwa 2005, Kampuni ambayo walimu hawajui mahali ilipo, inaendeshwaje na inamsaidiaje mwalimu.

Viongozi wa chama kipya cha walimu nchini kinachojumuisha Maafisa Elimu Tanzania (UMET) akiwemo Katibu Mkuu wao Meshack Kapange anasema kuwa Lengo la walimu ni kuwa na kipato na uchumi mzuri utakaomuwezesha mwalimu kukopesha na siyo kukopa kopa lakini CWT kimewapotosha walimu kwa kuendelea kuwajengea mawazo na fikra za kukopa kwa kuanzisha SACCOS zinazokopa mitaji kutoka mabenki kama vile CRDB badala ya kutumia fedha kinazokusanya.

‘’ Je uliwahi kuona au kusikia madaktari, wanasheria, maafisa ugani wa kilimo na mifugo, askari polisi na wanajeshi na kada nyingine wanakopa kopa kama walimu? Madeni humuondolea mtu uhuru na kumfanya mtumwa na mkimbizi wa mazingira. CWT kinawafanya walimu wawe watumwa wa madeni. Hatutaki utumwa, tunataka uhuru wa kipato na mahitaji’’ Anasema Mwalimu Kapange

.
Anasema CWT kimedhoofisha nguvu za walimu kwa kuwagawa na kuvunja matawi yaliyokuwa katika ngazi ya Kata na shule ili walimu wasiweze kukutana na kufanya vikao vya pamoja kwa lengo la kujadili juu ya matatizo yao, badala yake wamewaweka wawakilishi wa mahali pa kazi ambao wanahudhuria vikao vya Baraza la Wilaya mara moja kila baada ya miaka miwili na nusu (miezi 30), na kuwafanya walimu wasiwe na mahali pa kutolea mawazo na kero zao.

Pilika pilika za CWT za kuandaa mgomo zimeanza rasmi tarehe 5 Juni 2012 kwa kuitisha kikao cha ghafla mjini Dodoma, baada ya kuona UMET unaendelea na harakati za Kidemokrasia za kupigania na kudai haki za walimu nchini na kufanya mazungumzo na mamlaka mbalimbali za serikali kuhusu haki na madai ya walimu kwa kuanzia Bungeni tarehe 28/01/2012 mpaka tarehe 09/02/2012, ambapo pai UMET kilipeleka hoja zake Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Wabunge mbalimbali bila kujali itikadi za vyama vyao.

Tarehe 28/05/2012, UMET, ulifanya kikao na Kamati ya kudumu ya Huduma za Jamii ya Bunge kwenye Ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar-es-Salaam na kuwasilisha hoja za madai ya walimu zipatazo 19 ambapo katika kikao hicho CWT hawakupangua katika ratiba lakini waliitwa. Walijitahidi sana kupata hoja za UMET ndani ya kikao hicho bila mafanikio.

Katika kablasha la hoja 19 za UMET, CWT wakaamua kuchukua hoja tatu tu na ndizo wanazoziandalia mgomo. Kero ambazo wao wenyewe wameshiriki kuzitengeneza kama vile waraka kandamizi na madeni ya walimu wameamua kuyaacha na wala hawataki kabisa kuzungumzia.


‘’CWT na serikali wanagombana kwenye vyombo vya habari lakini wakiitana ofisini wanamalizana na kuwaacha solemba walimu. Safari hii tutawaaminije? Ningependa kukishauri CWT kuwa kiwe cha kwanza kuachilia haki za walimu ndipo kiitishe mgomo. Walimu wenzangu, tunayo haki ya kugoma kama tukiamua kugoma, lakini tuwagomee wote wawili, CWT na serikali wote ni wabaya wetu na waporaji wa haki za walimu’’ anasema Mwalimu Kapange.

Mwandishi anapatikana kwa simu 0754 440749 au barua pepe kalulunga2006@yahoo.com na www.kalulunga.blogspot.com
 
UMET ndio mkombozi wa mwalimu kuliko hao wezi CWT. Walimu jitoeni huko jiungeni na chama hicho kipya cha kisasa.
 
Agency Shop Agreement! Mwl umenifumbua macho hebu elezea kidogo, yaani tunakatwa pesa kwa ajiri ya vyama vya wafanyakazi hata kama hatukuwahi kuomba kuwa wanachama wa vyama hivyo?
 
Makubwa, kumbe ndivyo ilivyo. Ngoja niwashtue na wengine. Hasa imenikera sana hii ya waraka kandamizi. Kujiunga na UMET masharti yake yakoje?
 
Wewe unaetaka kujiunga mpigie katibu mkuu wake no. Mwl. Meshac Kapange 0756204568.
 
Mungi Siasa gani? Kama kutetea na kuleta ukombozi kwa walimu ni siasa basi sawa.
 
Last edited by a moderator:
UMET ndio mkombozi wa mwalimu kuliko hao wezi CWT. Walimu jitoeni huko jiungeni na chama hicho kipya cha kisasa.
Lakini CWT si kwa mujibu wa Sheria? Je tukajitoa huko CWT si tutaenda lea kukatwa 2% ya mshahara wetu ka mchango aw CWT? Coz wengine hata hatukuomba Kuwa members tumesajiliwa automatically? Na je mnatuhakikishiaje Kuwa hamtakuwa ka CWT na je mnaongozwa na Sheria gani? Na vipi kuhusu. TSD

 
Round hii kila kitu kitakuwa wazi. Uamuzi ni wetu kama tuko tayari kwa mabadiliko au bado tunapenda kuendelea kunyonywa.

Amua sasa
 
...(naomba ninukuu hii mistari)...CWT kimekiuka lengo la awali la
kujenga kitega uchumi cha
Mwalimu House ambalo lilikuwa
ni kukusanya fedha ili siku
ikitokea kuwa walimu
wanagoma na serikali
ikawatishia kwa kuwanyima
mishahara wangeweza
kuendesha mgomo na kujilipa
wenyewe mishahara kama
wanavyofanikiwa walimu wa
Kenya(mwisho wa kunukuu)...huu mpango umenvutia sana,kumbe mambo yanawezekana walimu mkijipanga?...
 
Greatest article. Imechapwa kwenye gazeti gani? I wish nilisome hilo gazeti!
 
Kali kuliko zote kuna mwl aliandika barua asiwe anakatwa mshahara kwa ajil ya cwt badala yake jamaa akakatwa mshahara wote mpaka leo ana madai serkaln ya ule mwenz mmoja
 
Kuen makin. Sa hv hawatafanya tena makosa. Watawaulimboka kabla hata hamjasikika vya kutosha.
 
Sheria zipo. Tangu lini vyama vya hiari vimegeuzwa kuwa wanyang'anyi wa fedha ya mwl. bila hiyari.? Amini uanachama si lazima, pia kuanzisha chama kingine ruksa. Tuhamasike tujitoe ndipo CWT itajua kuwa ilijisahau kutetea walimu. Mwisho aminini kuwa hata mgomo huo unao hubiriwa na Mkoba ni viini macho vya kumfanya yeye avute mshiko. Mkoba na .......... damu damu!.
 
Da kubabake! kumbe hawa Cwt ndio wanaotufanyia uhuni huu? aisee ngoja nifanye mpango nitafute hilo gazeti niwasambazie jamaa zangu au kuwabandikia kila mahali,sisi sio walimu wa kipindi kile,pia nanyi UMET mnatumia njia zipi haswa kuwafikia walimu wote Tz? njooni Kigoma huku watu walishajitoa kitambo tuu huko cwt
 
Back
Top Bottom