CUSNA Investment Limited yatoa msaada wa magongo 100 MOI

Joined
Apr 15, 2025
Posts
91
Reaction score
174
Kampuni ya CUSNA Investment Limited imetoa msaada wa magongo 100 kwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo (MOI) ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kusaidia makundi mbali mbali ya wahitaji.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya msaada huo jana Februari 10, 2026, kwa niaba ya Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Bi. Harieth Olindo alisema lengo la kutoa vifaa hivyo ni kusaidia wagonjwa wenye uhitaji pamoja na kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha huduma za afya.

“Tumeamua kutoa msaada huu wa magongo 100, vitimwendo 15 pamoja na walker 6 kwa MOI ili kuwasaidia wagonjwa wanaohitaji vifaa hivi katika hatua zao za matibabu. Tunaamini kuwa mchango huu utapunguza changamoto wanazokutana nazo wakiwa hospitali na baada ya kutoka hospitali,” alisema Bi. Olindo.

Mbali na magongo 100, kampuni hiyo pia ilitoa msaada wa vitimwendo 15 na walker 6 (vifaa vya kusaidia wagonjwa kufanya mazoezi ya kutembea), ikiwa ni mwendelezo wa dhamira ya kampuni hiyo kushiriki katika shughuli za kijamii.

Msaada huo ulipokelewa na Meneja wa Wagonjwa wa Ndani wa MOI, Bi. Magreth Kumpuni, ambaye ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo na kueleza kuwa utasaidia kwa kiasi kikubwa wagonjwa wanaohitaji vifaa vya kutembelea.

“Tunawashukuru sana CUSNA Investment Limited kwa msaada huu muhimu... Vifaa hivi vitasaidia wagonjwa wetu hasa wale waliofanyiwa upasuaji na wenye changamoto za mifupa na viungo. Vifaa hivi vitasaidia katika kuboresha huduma zetu,” alisema Bi. Kumpuni.

Taasisi ya MOI inaendelea kuwaalika makundi mbalimbali ya kijamii kuja kuwafariji waginjwa wenye mahitaji kwa pamoja na huduma zibazotolewa na wataalam wa MOI , wagonjwa huhitaji faraja kutoka kwa jamii.
IMG-20260211-WA0053.jpg
 
Kampuni ya CUSNA Investment Limited imetoa msaada wa magongo 100 kwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo (MOI) ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kusaidia makundi mbali mbali ya wahitaji.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya msaada huo jana Februari 10, 2026, kwa niaba ya Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Bi. Harieth Olindo alisema lengo la kutoa vifaa hivyo ni kusaidia wagonjwa wenye uhitaji pamoja na kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha huduma za afya.

“Tumeamua kutoa msaada huu wa magongo 100, vitimwendo 15 pamoja na walker 6 kwa MOI ili kuwasaidia wagonjwa wanaohitaji vifaa hivi katika hatua zao za matibabu. Tunaamini kuwa mchango huu utapunguza changamoto wanazokutana nazo wakiwa hospitali na baada ya kutoka hospitali,” alisema Bi. Olindo.

Mbali na magongo 100, kampuni hiyo pia ilitoa msaada wa vitimwendo 15 na walker 6 (vifaa vya kusaidia wagonjwa kufanya mazoezi ya kutembea), ikiwa ni mwendelezo wa dhamira ya kampuni hiyo kushiriki katika shughuli za kijamii.

Msaada huo ulipokelewa na Meneja wa Wagonjwa wa Ndani wa MOI, Bi. Magreth Kumpuni, ambaye ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo na kueleza kuwa utasaidia kwa kiasi kikubwa wagonjwa wanaohitaji vifaa vya kutembelea.

“Tunawashukuru sana CUSNA Investment Limited kwa msaada huu muhimu... Vifaa hivi vitasaidia wagonjwa wetu hasa wale waliofanyiwa upasuaji na wenye changamoto za mifupa na viungo. Vifaa hivi vitasaidia katika kuboresha huduma zetu,” alisema Bi. Kumpuni.

Taasisi ya MOI inaendelea kuwaalika makundi mbalimbali ya kijamii kuja kuwafariji waginjwa wenye mahitaji kwa pamoja na huduma zibazotolewa na wataalam wa MOI , wagonjwa huhitaji faraja kutoka kwa jamii.View attachment 3542431
We just want food. We want to feel something in our fuckin empty stomachs.

Give us food now not those Magongoz.

Nyaunyie
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom