Hakuna bei ambayo ni standard, hii inatokana na sababu zifuatazo
1. Developer Standards: Kila developer ana standards zake za bei kulingana na mazingira anayofanyia kazi, vitu vinavyo define kazi yake, mfano security, SEO, responsiveness ya website, n.k
2. Requirements: Kuna developer anacharge kulingana na idadi ya mahitaji yako katika website, kwa hiyo mfano client anayekuja na requirements 10 charges zake zitakuwa tofauti na client atakayekuja na requirements 100
3. Aina ya website: Kuna developer anakucharge kwa kuzingatia aina ya website unayotaka kutengenezewa, mfano kuna static website, dynamic website, web based app (system) n.k
4. Interest ya Website: Kuna developer anakucharge kulingana na interest na maudhui ya website, mfano akigundua kuwa website yako ina uwezo wa kukuingizia million 100 kwa mwaka ni tofauti na website ambayo labda inahusisha masuala ya kijamii isiyoingiza mapato yoyote, hapa lazima kuwe na utofauti wa bei
5.Market competition: Kutokana na soko la IT kukua kwa kasi developer wanajikuta wanapanga bei ili kumvuta mteja, cha muhimu wewe client unatakiwa uwe na vigezo vyako (requirements) ambazo mwisho wa siku unatakiwa kuziona zinafanya kazi kama zinavyotakiwa kufanya kazi
NB: Maelezo niliyotoa hapa ni uzoefu wangu kama developer na jinsi ninavyowacharge wateja wangu, sio standard za developer wote, kila deveoper ana standard zake katika kumchaji client wake