CUF Zanzibar kutoshiriki uchaguzi kuna athari gani?

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,426
18,231
Wakuu,

Naomba nifahamu athari za CUF kususia uchaguzi,athari zipi zinaweza kutokea?
 
Athari zipo nyingi lakini kubwa kuliko ni kuibuka kwa matukio ya mauaji yakutisha na kushtukiza(UGAIDI).

Kwa maana magaidi wapo kila sehemu wanachokosa ni sababu tu yakuhalalisha ugaidi wao. Uhalali wa uchaguzi itakua sababu murua kwao.

Hivyo tutegemee kuona vikundi vingi vitakavyopinga suala la Uchaguzi Z`bar kwa style tofauti ikiwemo hii ya ugaidi. Stay tuned..!
 
Kuna athari kubwa sana. Kwa mfano.
1/Uchaguzi kukosa uhalali(Legitimacy)

2/Zanzibar kuingia kwenye mgogoro mkubwa wa kisiasa kwa miaka mitano.

3/Zanzibar kutengwa na jumuiya za kimataifa.(Tayari jumuiya hizo zimeshatoa msimamo wa kutokutambua kurudiwa kwa uchaguzi huo wakati mazungumzo ya muafaka yamekufa)

4/Kusitishwa kwa misaada ya Kiuchumi(Why? Wahisani wanaamini serikali za kidemokrasia ndio zinawekeza kwa wananchi na sio kwa viongozi)

5/Kuibuka kwa machafuko ya kisiasa(Wananchi watatafuta sauti zao zisikike kwa nguvu)

6/Kuongezeka kwa uhasama wa kisiasa baina ya CUF na CCM.

7/Mgogoro wa Kikatiba katika kuendesha serikali(Katiba ya sasa ya Zanzibar inatamka kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ni lazima atokane na Chama cha CUF au CCM na baraza la Mapinduzi(mawaziri) liwe na wajumbe kutoka CCM na CUF katika uwiano unaokaribiana sana)
 
Wakuu,

Naomba nifahamu athari za CUF kususia uchaguzi,athari zipi zinaweza kutokea?
Mkuu Viol kabla sijakujibu uzi wako naomba nikuulize swali moja tu; mkuu ushawahi kuishi ama kushuhudia kampeni za uraisi Zanzibar?
 
Mkuu sijawahi kushuhudia live kampeni za Zanzibar zaidi ya kuangalia vi-clips kwenye social media
 
M
Kuna athari kubwa sana. Kwa mfano.
1/Uchaguzi kukosa uhalali(Legitimacy)

2/Zanzibar kuingia kwenye mgogoro mkubwa wa kisiasa kwa miaka mitano.

3/Zanzibar kutengwa na jumuiya za kimataifa.(Tayari jumuiya hizo zimeshatoa msimamo wa kutokutambua kurudiwa kwa uchaguzi huo wakati mazungumzo ya muafaka yamekufa)

4/Kusitishwa kwa misaada ya Kiuchumi(Why? Wahisani wanaamini serikali za kidemokrasia ndio zinawekeza kwa wananchi na sio kwa viongozi)

5/Kuibuka kwa machafuko ya kisiasa(Wananchi watatafuta sauti zao zisikike kwa nguvu)

6/Kuongezeka kwa uhasama wa kisiasa baina ya CUF na CCM.

7/Mgogoro wa Kikatiba katika kuendesha serikali(Katiba ya sasa ya Zanzibar inatamka kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ni lazima atokane na Chama cha CUF au CCM na baraza la Mapinduzi(mawaziri) liwe na wajumbe kutoka CCM na CUF katika uwiano unaokaribiana sana)

MA CCM hayawezi kwani kubadilisha katiba wakatoa ivyo vipengele mkuu,naomba kujua
 
Pamoja na yaliyosemwa tatizo lingine kubwa litakuwa upande wa Pemba ambayo ina wafuasi wengi wa CUF. sera za serikali zitatekelezwa kwa shida sana kule Pembwa. watawala wa kisiasa kama wakuu wa wilaya na mkoa watakuwa katika hali ngumu. Itabidi serikali itumie zaidi nguvu za dola hali ambayo itazidi kujenga chuki.
Kwa ujumla kunaweza kuwa na uhasama mfano wa ule wa wayahudi na wapalestina.
Kutekeleza agizo la Jecha ni hatari zaidi ya kulipuuza.
 
Mkuu sijawahi kushuhudia live kampeni za Zanzibar zaidi ya kuangalia vi-clips kwenye social media
Mimi mkuu uchaguzi wa 2005 ulinikuta huko nikiwa na miaka miwili naishi huko (nafanya kazi). Athari itakuwa kubwa sana hasa kwenye suala la umoja wa kitaifa (siombei vifo/kuuana). Kipindi hicho CUF waliamini uchaguzi wa 2000 walinyang'anywa ushindi,ilifikia hatua wakagawana misikiti kuwa huu ni msikiti wa CCM na huu ni CUF. Vilevile ilikuwa kama ukifiwa wewe ni mwana CCM basi watakuzika wana CCM wezako vilevile ukifa CUF watakao kuzika ni CUF wezako. Wakati wa kampeni lilikuwepo kundi la Janjaweed (vijana wa CCM) kazi yao ilikuwa kuwapa adabu wafuasi wa CUF (kwa sasa nasikia wanajiita Mazombi). Vilevile CUF walikuwa na vijana wao waliofunzu karate na jundo nao kazi yao ilikuwa ni kutoa kisago kwa mwana CCM yoyote atakayeonekana anaingilia mambo yao. Baada ya Dr. Aman Karume raisi mstaafu kutengeneza serikali ya mseto hiyo hali ikaisha na Wazanzibar wakawa wamoja kitu ambacho kwa yanayoendelea sasa yatarudisha nyuma kila mafanikio waliyokuwa wameyapata. Na vikwanzo vitakavyowekwa amini vitakuwa na athari kubwa sana Tanzania bara kwa sisi walala hoi mkuu wangu Viol.
 
Wakuu,

Naomba nifahamu athari za CUF kususia uchaguzi,athari zipi zinaweza kutokea?
Kubwa sana nahisi siasa za chuki zitszidi sana na kweli nitamuonea huruma hiyo rais doctor sheni itakuwa katika kipindi kigumu cha uhasama has a Pemba juzi nilimsikia kiongozi mmoja akisema mfanyabishara yoyote ikiwa hatamuuzia MTU kwa itikadi ya kisiasa atapokonya laisens sasa hiyo ni moja tu watu hawazikana na sijuwi kama karafuu zitachumwa wapemba umoja wao ndio ushindi wacha tuone picha inavyokwenda
 
Uamuzi wa kurudia uchaguzi umetokana na kujiamini zaidi kuliko hali iliyopo. hii inatokana na imani kuwa kuna nguvu za dola nyuma na pia kuwepo kwa muungano. Ingelikuwa hakuna muungano hali ingeshakuwa tete kule visiwani. Jecha aliona hilo kama kinga kwake wala hakuzingatia uhalali wa matokeo.
 
M

MA CCM hayawezi kwani kubadilisha katiba wakatoa ivyo vipengele mkuu,naomba kujua
Sidhani kama hilo linawezekana, kwa sababu.
1/Vipengele vile vinavyohusu Serikali ya Umoja wa kitaifa vilitokana na Kupigiwa kura ya maoni na wazanzibar wote. Hivyo kuvifuta inahitajika mchakato wa kura ya maoni tena, na huo ni mchakato mrefu.

2/Serikali ya umoja wa kitaifa ilitokana na Muafaka baina ya CUF na CCM chini ya usuluhishi maalum baada ya mlolongo mrefu wa majadiliano. Sasa sio rahisi kufutwa kienyeji enyeji sana.

Yote kwa yote, chini ya CCM lolote linawezekana, hivyo hata hilo tusishangae CCM wakilazimisha litokee, na tayari dalili zimeoneka wazi wazi baada ya makada wa juu wa CCM Zanzibar (Akiwemo Balozi Amina, Salmin Amour, Balozi Seif Idd) kuonyesha msimamo wa kuchukia muundo mzima wa serikali ya umoja wa Kitaifa ambapo CUF ilipata mwanya wa kuingia serikalini na kujikita barabara.
 
Mkuu shukran kwa darasa murua
 
Kuna athari kubwa sana. Kwa mfano.
1/Uchaguzi kukosa uhalali(Legitimacy)

2/Zanzibar kuingia kwenye mgogoro mkubwa wa kisiasa kwa miaka mitano.

3/Zanzibar kutengwa na jumuiya za kimataifa.(Tayari jumuiya hizo zimeshatoa msimamo wa kutokutambua kurudiwa kwa uchaguzi huo wakati mazungumzo ya muafaka yamekufa)

4/Kusitishwa kwa misaada ya Kiuchumi(Why? Wahisani wanaamini serikali za kidemokrasia ndio zinawekeza kwa wananchi na sio kwa viongozi)

5/Kuibuka kwa machafuko ya kisiasa(Wananchi watatafuta sauti zao zisikike kwa nguvu)

6/Kuongezeka kwa uhasama wa kisiasa baina ya CUF na CCM.

7/Mgogoro wa Kikatiba katika kuendesha serikali(Katiba ya sasa ya Zanzibar inatamka kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ni lazima atokane na Chama cha CUF au CCM na baraza la Mapinduzi(mawaziri) liwe na wajumbe kutoka CCM na CUF katika uwiano unaokaribiana sana)
Wewe wacha kudanganya watu katika katiba na kuhusu serikali ya mseto haikutajwa CUF wala CCM kasomo vizuri bali ni chochote kitakacho pata 10% ya kura kama kuna vyama vitano vimepata 10% basi vina haki ya kuingia serikali ya mseto.
Na kwa akili zako ndogo kuna vyama Zaidi ya 14 vua upinzani Tanzania na chama cha CUF ni kimoja kati ya hivyo sasa kutoshiriki kwa CUF kuna vyama vyengine Zaidi ya 13 vitashiriki sasa hiyo legitimacy yako sijui itatoka wapi na kwa vigezo vipi.Hiyo 4 na 3 1995 ilitokezea na tuliweza kuishi na hata kama wakikatisha misaada people in znz wataenelea kuishi na kitu kizuri CUF pia wamo kwenye jahazi hilo.
Na kuhusu uhasama serikali ya mseto haikufanikiwa kupunguza huo uhasama just wali wali pretend kila kitu kiko sawa kwani mshirika mmoja wa serikali alikuwa ana subbotage kila kitu.
 
Back
Top Bottom