CUF yatoa onyo kali. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF yatoa onyo kali.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHIBUU, Oct 29, 2012.

 1. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  SERIKALI INAUKUZA MGOGORO ULIOPO BADALA YA KUUDHIBITI
  Ndugu Waandishi wa Habari,
  Kwanza napenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwenu kwa kukubali wito wa kuja kutusikiliza. Sisi Chama cha Wananchi, CUF, tunatambua na tunathamini mchango wenu mkubwa na jitihada zenu nyingi, katika kusaidia kuhamasisha hali ya amani na utulivu ndani ya nchi yetu. Ni katika kuendeleza hali ya amani na utulivu ndani ya Nchi, suala lililopelekea kukuiteni leo hapa na kukuelezeni kile ambacho sisi tunakiona kuhusiana na hali tete inayoendelea hapa Zanzibar, na Tanzania kwa ujumla.

  Ndugu Waandishi,
  Naamini mnatambua kuwa Msingi mmoja, Mkuu wa Chama cha CUF, ni kulinda, kusimamia na kutetea haki za binadamu pamoja na kuleta amani, umoja, mapenzi na mshikamano miongoni mwa wananchi wote baada ya kuchoshwa na hali ya uhasama, chuki, migogoro, mifarakano, mapambano na ugomvi wa kisiasa uliodumu kwa muda mrefu hapo kabla. Mpasuko wa kisiasa uliokuwepo, ulisababisha kutokea maafa na mauwaji makubwa ya wananchi na Wana-CUF, wasiokuwa na hatia, zaidi ya 45 mnamo Jjanuari, mwaka 2001, yaliyotekelezwa na Jeshi la Polisi la Tanzania na Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, SMZ.

  Kupitia Maridhiano ya Wazanzibari, yaliyoasisiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya Sita ya Uongozi wa Zanzibar, Dr Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa Chama cha CUF, ambaye pia kwa sasa ni Makamo wa Kwanza wa Raisi wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, November 5, 2009 ndipo Zanzibar Mpya ya amani, utulivu, umoja na mshikamano ikazaliwa.

  Ndugu Waandishi,
  Ndiyo matarajio yetu sote bila shaka kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, SMZ, pamoja na majukumu yake mengine, inawajibika kuwajali, kuwathamini, na kuwalinda Wananchi wote, na mali zao, chini ya Misingi ya Hikma, Haki, Sheria, na Uadilifu. Matumaini hayo ya umma yamekuwa yakizorota na kutoweka kabisa, usoni mwa kila mwenye hisia za kibinaadamu na mpenda haki, ndani na nje ya Visiwa vya Unguja na Pemba, kadiri siku zinavyokwenda, licha ya Nchi kupita katika wimbi la machafuko, hivi karibuni.


  Ndugu Waandishi,
  Kiini na chanzo cha hali hiyo bila shaka kinaeleweka, ambapo kama ilivyoripotiwa kutoka baadhi ya Mamlaka za Serikali, machafuko hayo, pamoja na sababu nyengine, yametajwa kutokana na fujo za tarehe 17 na 18 Oktoba, 2012 zlizofanywa na baadhi ya watu au vikundi ambavyo kimantiki kufanya hivyo ni kwenda nje ya busara na utiifu wa Sheria. Fujo hizo zimesababisha uharibifu mkubwa wa mali za umma, wananchi mmoja mmoja na hata vyama vya siasa. Miongoni mwa vitendo hivyo ni kuvunjwa kwa maduka, vyombo vya usafiri, kukatwa miti ovyo na nguzo za umeme, uharibifu wa miundombinu zikiwemo barabara, pamoja na kuchomwa moto Maskani za CCM. Matukio mengine ya kusikitisha na kuhuzunisha zaidi kupitia vurugu hizo ni kuuwawa kikatili kwa Askari Polisi, Koplo Said Abdulrahman, na watu wasiojulikana pamoja na kuuliwa kwa risasi kijana Salim Hassan Mahoja katika maeneo ya Amani Fresh na watu waliotajwa kuwa wahusika wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

  Ndugu Waandishi,

  Jeshi la Polisi likishirikiana na Vyombo vyengine vya Ulinzi na Usalama, vikiwemo Vikosi vya SMZ, limeanzisha oparesheni inayoitwa ya kuwasaka wahalifu na wafanya fujo za tarehe 17 na 18, Oktoba, mwaka huu. Katika kile ambacho kinashangaza sana, ni jinsi oparesheni hizo zinavyoendeshwa na kusimamiwa katika maeneo mbali mbali ya manispaa ya Zanzibar, hususan katika Mkoa wa Mjini Maghribi. Bila shaka pahala popote duniani panapohitajika kufanywa Oparesheni za kuwasaka wahalifu wa aina yoyote, mamlaka husika ndizo zinazobeba dhamana na jukumu la kutumia utaalamu, mafunzo na mbinu zinazoepusha ukiukaji wa haki na kufanikisha lengo lililokusudiwa, kwa kufuata Sheria. Hatimaye ni kuwashika wahalifu na kuwafikisha katika vyombo vya sheria ili sheria ichukue mkondo wake na anaefikishwa katika vyombo hivyo hutakiwa apate fursa ya kusikilizwa.

  La kushangaza zaidi, Jeshi la Polisi upande wa Zanzibar, likishirikiana na Vikosi vya KMKM, KVZ na JKU wamekuwa wakiliendesha zoezi hilo la kuwasaka wahalifu kwa uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu, vitisho, unyanyasaji wa raia na mauwaji. Matukio ya Zanzibar hayana tofauti kubwa na matukio ya kule Mwanza na Dar es Salaam. Kule Mwanza kamanda wa polisi wa Mkoa huo Libertus Barlow aliuliwa kwa kupigwa risasi siku ya tarehe 13, Oktoba 2012 na hatukuona serikali ikiwaamuru askari wake kufanya uvamizi wa vijiji, uvunjaji majumba, upigaji kiholela wa watu, maonevu ya wanawake, wizi na uharibifu wa mali na mauwaji kama inavyofanyika hivi sasa hapa Zanzibar. Kilichofanyika Mwanza ni msako ulifanyika kitaalamu kwa taratibu za kiupelelezi na kiasi cha watu watano tayari wamekamatwa kwa lengo la kufikishwa katika vyombo vya sheria na kuripotiwa katika vyomba vya habari.

  Halkadhalika katika matukio ya Dar es Salaam hivi karibuni, tuliona jeshi la polisi likishirikiana vyombo vya ulinzi na usalama likitumia mbinu kadhaa kukabiliana na waandamanaji na kuwakamata watuhumiwa wa fujo hizo. Hatukuona vitendo vya uvamizi na mateso ya watu wasio na hatia kwa muda wa siku nne mfululizo kama inavyofanyika hapa Zanzibar. Hatusemi serikali isiwasake waliofanya fujo na wahalifu waliomuua Coplo Said Abdulrahman, iwasake na iwafikishe wahusika wote katika vyombo vya sheria lakini sio watumie kisingizio hicho kufanya hujuma, mateso, unyanyasaji na muwaji kwa wasio na hatia ambao wengi ni wafuasi wetu wa CUF.

  Ndugu waandishi,
  Tokea tarehe 25 Oktoba 2012 jeshi la polisi na vyombo vyengine vya ulinzi na usalama kwa hali ya utumiaji mkubwa wa nguvu limekuwa likivamia maeneo ya Amani, Magogoni, Daraja-bovu, Mwanakwerekwe, Mtoni, Kinuni, Kwamtipura, Mboriborini, Kilimahewa, Mpendae, Mikunguni, Nyerere, Kwarara, Tomondo na Nyarugusu ambapo hufanya msako nyumba hadi nyumba, na barabarani, kuwapiga, kuwatesa, na kuwakamata raia wasiokuwa na hatia bila ya kujali na kuiheshimu Sikukuu ya Iddi. Majumba yanavunjwa na waliomo ndani kuvamiwa na kuteswa. Kituo cha ushoni cha kuwaendeleza mayatima Bububu (JUDAMA) kilivamiwa na watoto wa kike mayatima kupigwa vibaya. Wengine walipigwa na kuchukuliwa wakiwemo Khalid Shindano na Suleiman Kichwa. Wengine walikamatwa na kunyolewa ndevu zao hadharani. Pia yuko aliepigwa hadi kupoteza maisha. Waliokamatwa na kunyolewa ndevu ni pamoja na Khamis Khatibu na Moh’d Omar wote wa Fuoni.

  Ndugu waandishi,
  Chama cha CUF kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kijana aitwae Hamadi Ali Kaimu,mwenye umri wa miaka 22, mkaazi wa Nyerere. Kijana huyu akiwa yuko katika shughuli za kulisha ng’ombe wake huko kwao Nyerere alivamiwa siku ya Ijumaa ya tarehe 26/10/2012 siku ya Idi Mosi na vikosi hivyo vya ulinzi na usalama wakiendeleza zoezi lao la kusaka wahalifu. Kijana Hamadi alipigwa vibaya sana hadi kupoteza maisha. Baada ya wazee wake kumtafuta katika vituo mbali mbali vya polisi hawakufanikiwa kumpata ndipo walipokwenda kumtafuta katika hospitali kuu ya Mnazi mmoja. Baada ya kukosa taarifa zake sehemu ya mapokezi lakini walielekezwa wende chumba cha maiti na ndipo walipogundua kijana wao, Hamad Ali Kaimu ameshafariki huku mwili wake ukiwa na majeraha sehemu mbali mbali.

  Walioathirika na vipigo vya uvamizi huo mpaka siku ya Jumapili ya tarehe 28/10/2012 ni wakiwemo hawa wafuatao:
  Baadhi ya waliovamiwa na kupigwa vibaya​
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="width: 49"] [/TD]
  [TD="width: 270"]JINA[/TD]
  [TD="width: 252"]PAHALA ALIPOPIGWA[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]1.[/TD]
  [TD="width: 270"]Juma Abdi[/TD]
  [TD="width: 252"]Dukani Bububu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]2.[/TD]
  [TD="width: 270"]Khamis (Mshona viatu)[/TD]
  [TD="width: 252"]Dukani Bububu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]3.[/TD]
  [TD="width: 270"]Asma na watoto wake[/TD]
  [TD="width: 252"]Ndani ya nyumba yao Bububu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]4.[/TD]
  [TD="width: 270"]Juma na mke wake[/TD]
  [TD="width: 252"]Dukani Bububu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]5.[/TD]
  [TD="width: 270"]Kocha Taibu[/TD]
  [TD="width: 252"]Dukani Bububu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]6.[/TD]
  [TD="width: 270"]Muuza magazeti[/TD]
  [TD="width: 252"]Barabarani kazini kwake Bububu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]7.[/TD]
  [TD="width: 270"]Ali Yussuf Choki[/TD]
  [TD="width: 252"]Dukani Bububu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]8.[/TD]
  [TD="width: 270"]Ubwa na wateja wake[/TD]
  [TD="width: 252"]Gareji Bububu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]9.[/TD]
  [TD="width: 270"]Shamis Amiri[/TD]
  [TD="width: 252"]Dukani Bububu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]10.[/TD]
  [TD="width: 270"]Mtoto mdogo wa miaka mitatu (3) wa Bi Salma Faki[/TD]
  [TD="width: 252"]Nyumbani kwao Bububu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]11.[/TD]
  [TD="width: 270"]Zahor Khalfan[/TD]
  [TD="width: 252"]Bububu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]12.[/TD]
  [TD="width: 270"]Ahmed[/TD]
  [TD="width: 252"]Bububu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]13.[/TD]
  [TD="width: 270"]Mashavu Mbarouk[/TD]
  [TD="width: 252"]Bububu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]14.[/TD]
  [TD="width: 270"]Khalfan Moh’d[/TD]
  [TD="width: 252"]Bububu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]15.[/TD]
  [TD="width: 270"]Suleiman Ali Alawi[/TD]
  [TD="width: 252"]Bububu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]16.[/TD]
  [TD="width: 270"]Ali Suleiman[/TD]
  [TD="width: 252"]Bububu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]17.[/TD]
  [TD="width: 270"]Said Suleiman[/TD]
  [TD="width: 252"]Bububu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]18.[/TD]
  [TD="width: 270"]Salma Abdalla[/TD]
  [TD="width: 252"]Bububu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]19.[/TD]
  [TD="width: 270"]Raya Moh’d (Robo)[/TD]
  [TD="width: 252"]Bububu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]20[/TD]
  [TD="width: 270"]Ali Abdalla Saleh[/TD]
  [TD="width: 252"]Bububu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]21[/TD]
  [TD="width: 270"]Salum Raza[/TD]
  [TD="width: 252"]Bububu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]22.[/TD]
  [TD="width: 270"]Khalfan Abdalla Ali[/TD]
  [TD="width: 252"]Bububu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]22.[/TD]
  [TD="width: 270"]Nayadi Moh’d[/TD]
  [TD="width: 252"]Kikwajuni[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 49"]23.[/TD]
  [TD="width: 270"]Miraji[/TD]
  [TD="width: 252"]Jang’ombe[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Ndudu waandishi,
  Chama cha Wananchi, CUF kinalaani kwa nguvu zake zote vitendo vya fujo na uvunjifu wa amani vilivyofanywa siku ya tarehe 17 na 18 Mwezi huu viliyoambatana na mauwaji ya Coplo Said Abdulrahman, sambamba na hilo kilanaani kwa nguvu zote na kusikishwa mno na mauwaji, vipigo, uonevu, unyanyasaji, mateso kwa raia wasio na hatia, kurejeshwa kwa hali ya chuki, uhasama, kupaliliwa kwa vitendo vya ubaguzi baina ya uunguja na upemba. CUF inalaani azma ya kuwanyanyasa wananchi na hujuma hizo zilizopindukia mipaka zinazohamasishwa na baadhi ya Watendaji wa Vikosi na Vyombo vya Dola, kwa utashi na maslahi binafsi. Tunaamini vitendo hivi vinatoa fursa pana kwa wale ambao hawautaki umoja wa wazanzibari na kutoitakia mema Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar.

  Ndugu waandishi,
  Chama cha Wananchi, CUF, kinalaani azma na vitendo vyote hivyo vinavyoiweka haiba ya Nchi katika hali ya machafuko, wakati ambao Wananchi wamekuwa watulivu licha ya hali tete ya kisiasa. Wazanzibari wengi tayari wameshapoteza maisha huko nyuma tutokako na wengine kuachwa na ulemavu wa maisha kupitia hujuma kama hizi zinazofanywa na askari wetu kwa visingizio hivi na vile. Sisi tunadhani hayo yametutosha na ndio tukaamua kuingia katika enzi mpya ya Maridhiano, yaani kuishi kwa amani, utulivu na kuheshimiana. CUF inaamini Vitendo hivyo bila shaka havitatui mgogoro na tatizo lililojitokeza bali ni uvunjifu wa haki za binadamu na vinapalilia zaidi hasama na kushawishi mwendelezo wa uvunjaji wa amani.

  Chama Cha wananchi CUF, kinamtaka Kamishna wa Jeshi la polisi Zanzibar, Bwana Mussa Ali Mussa kuhakikisha anakomesha vitendo vyote vya unyanyasaji vinavyofanywa na vyombo vya dola dhidi ya raia wasio na hatia na hapo hapo kuwachukulia hatua wale wote wanaotenda unyanyasaji huo. Chama cha wananchi CUF kinamtaka waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Mhe Mohammed Aboud Mohammed kuhakikisha serikali inaheshimu haki za raia wake chini ya misingi ya utawala bora.

  Pamoja na kuiwacha Sheria ichukue mkondo wake, ni vyema Serikali na Vyombo vyake vya Dola kutekeleza wajibu na majukumu yao kwa kuzingatia sheria, haki, hikma na uadilifu, bila kuwahujumu na kuwasumbua Wananchi wasi na hatia, ikieleweka kuwa wao ni sehemu muhimu ya maisha na raia halali wa Nchi hii.

  Naomba kuwasilisha.
  HAKI SAWA KWA WOTE
  Salim Bimani
  [​IMG]Baba wa Marehemu Hamadi Ali Kaimu aliyeuliwa na vipigo vya jeshi la polisi siku ya Idi mosi
  [​IMG]Mkurugenzi wa Haki za binadamu, habari Uenezi na mahusiano na umma

  Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono taarifa hii ya CUF.Inasikitisha sana.
   
 3. bhikola

  bhikola JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 457
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  tena ilitakiwa wanyolewe mpaka ma.vu.zi maana inasemekana wingi wa nduvu ni sawa na wingi wa hayo makitu kwa hawa jamaa. for any reason, having those shts in uchafu
  anyway turudi kwenye mada, kwanza poleni sana kwa yanayowapata, alkini nanyi ni wajeuri sana maana kwanini muharibu miundombinu tunayowajengea? polisi wawapige taratibu tu mpaka mseme aliyenyuma yenu ni nani
   
 4. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,875
  Trophy Points: 280
  Unailalamikia Serikali ambayo na wewe unaiongoza?
   
 5. J

  Jembe_Ulaya Senior Member

  #5
  Oct 29, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 154
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Enough is enough!! Mmeanzisha wenyewe sasa mnalia nini.. Mmemchinja askari mnategemea nini?
   
 6. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kwani CUF sio serikali huko Zanzibar?! Nchimbi tandika kabisa hao kwa sababu walituchomea makanisa yetu.
   
 7. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ndoa ni kuvumiliana katika shida na raha, ukiolewa na mkurya usiogope vipigo
   
 8. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mbona hawajalaani kuchomwa Makanisa?
   
 9. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,093
  Likes Received: 505
  Trophy Points: 280
  Nyie CUF kupitia uamsho mmeanzisha fujo wenyewe kupitia uamsho,mkachoma makanisa na kuharibu mali za watu sasa mnalalamika nini? Siungi mkono mauaji ya mwanadamu yeyote ila naunga mkono vichapo vya polisi kwa wahalifu kama uamsho....
  Nampongeza sana Dr.Shein ama kwa hakika hikma yake imedhihirika..Kusema ukweli sikuwa namjua kuwa yuko strong kiasi hicho pale alipokuwa makamu wa Tanzania,kumbe kivuli cha JK ndicho kilichokuwa kinamfifisha asing'are....
  He is tough in decision japokuwa anaonekana ni mvumilivu sana....

  Uamsho a.k.a tawi la CUF washughulikiwe pasipo kurudi nyuma...
   
 10. C

  CUF Ngangari JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 273
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  udhalimu una mwisho wake, kibao kinageukaga, ipo siku nao wataonja chungu.
   
 11. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nilikuwa namwangalia Shein wakati wa Eid El Hadji. Alikuwa akitoa Onyo huku akimwangalia Sefu na Sefu akawa anajishtukia.
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa nini CUIF inatumia 'nguvu' nyingi kulaani hatua za polisi kusaka waalifu lakini hatukuona nguvu kama hiyo kulaani waandamanaji walipopiga watu,m kuwanyanyasa, kuharibu mali na kuua askari polisi? Hata kwenye taarifa hii, kuna mistari michache tu ya maneno kulaani uhuni huo wa Uamsho lakini maneno lukuki kulaani hatua zinazochukuliwa na vyombo vya dola kudhibiti hao wahuni!
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mambo ya ajabu kabisa haya!
   
 14. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  CUF walijifanya wao si Uhamsho, Serikali ikafanya kama mtu anayetupa jiwe gizani ili waone ni nani atalia ng'wee!!! Sasa Wananchi tumeshawajua Uhamsho ni nani. Watulie hivyo hivyo kama walivyojikausha mwanzoni waendelee kula kibano.
   
 15. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  it means unaunga mkono wauwaji dhidi ya raia,kichwa cha utomvu
   
 16. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Huwezi kulinganisha maafa ya sasa hivi na hapo katika maandamano,unajua watu wangapi washakufa na walojeruhiwa toka msako wa police wa kunyanyasa raia uwanze ? think think
   
 17. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Una akili ya mnyama.
   
 18. Indian

  Indian JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 27, 2012
  Messages: 749
  Likes Received: 542
  Trophy Points: 180
  Ivi kwani seif ali iddy na viongozi wengine wa ccm waznz hawajui wanapoishi? Haya sio mambo ya kulalamika ni kujibu mapigo inawezekana kabisa hata hawa viongozi wote wa ccm znz wakatekwa na kupewa kipigo
   
 19. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  kila siku tunaomba waonje machungu mkuu lakini haitokei....yawezekana hizi dua zetu zikawa ni dua za kuku......
   
 20. Mabreka

  Mabreka JF-Expert Member

  #20
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 29, 2012
  Messages: 709
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  jibu hoja kwa hoja,
  hiz ni dalili za uvivu wa kufikiri/ finyu
   
Loading...