CUF yaomba fedha za kampeni kwa mafisadi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF yaomba fedha za kampeni kwa mafisadi?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by EL+RA=UFISADI, Sep 16, 2010.

 1. E

  EL+RA=UFISADI Member

  #1
  Sep 16, 2010
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  CUF yaomba fedha za kampeni kwa mafisadi?

  Kuna tetesi kuwa Mbunge wa kuteuliwa wa Chama Cha Wananchi (CUF), Ismail Jussa, wiki hii amekutana na mtuhumiwa mkubwa wa ufisadi hapa Tanzania, Yusuf Manji, kwa lengo la kukiombea CUF msaada wa pesa kwa ajili ya kampeni zinazoendelea za uchaguzi mkuu.
  Manji ni mmiliki wa kampuni ya Quality Group Limited inayohusishwa na ukwepaji mkubwa wa kodi za serikali na ufisadi wa pesa za umma kupitia mifuko ya pensheni ya umma – NSSF na PSPF.
  Jussa ameonekana akiwa na mazungumzo na Manji Kempinski Hotel na haikuweza kufahamika mara moja nini hatma ya mazungumzo haya.
  Ni kawaida kwa vyama vya siasa nchini kuomba msaada wa pesa kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa.
  Tajiri wa Kihindi, Mzee Sabodo (ambaye hana tuhuma zozote za ufisadi), tayari ametoa 200 million/- kwa CCM na 100m/- kwa CHADEMA kwa ajili ya uchaguzi mkuu.
  Chama cha upinzani kama CUF kinapopewa pesa na watuhumiwa wakubwa wa ufisadi kama Manji, Rostam Aziz, Subhash Patel na wengineo kweli ni jambo jema?
  Tunaijua CCM ndiyo siku zote iko karibu na mafisadi na imekuwa ikipokea pesa nyingi kutoka kwao. Sasa inapofika hatua ambayo hata chama cha upinzani kama CUF kinaomba msaada wa fedha kwa mafisadi ujue kuwa taifa hili la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kweli limeuzwa.
  Huyu Jussa, ambaye ni msaidizi wa karibu wa Maalim Seif Shariff Hamad kule Zanzibar, anajulikana kuwa na rafiki wa karibu wa Rostam Aziz.
  Wengine wamediriki kusema kuwa Rostam ndiye alisaidia kumshauri swahiba wake, Rais aliyemaliza muda wake, Jakaya Kikwete, amteuwe Jussa kuwa mbunge.
  Kuna taarifa za muda mrefu sana kuwa Rostam Aziz amekuwa akitoa msaada kwa CUF tangu zamani kupitia kwa Jussa.

  HII NDIYO NCHI YETU NA HAWA NDIYO VIONGOZI WETU!
   

  Attached Files:

 2. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 251
  Trophy Points: 180
  MH.kweli tetesi...hauna kidhibitisho kabisa??
   
 3. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kuwa unakuja na vitu vya maana hapa.....
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Si kesha sema tetesi? Inatakiwa wenye data zaidi waotoe.
  My take: Haitashangaza kwa CUF kuomba hela kutoka kwa akina Manji na RA, kwani Jussa ni swahiba mkubwa sana wa RA. Aidha Prof Lipumba alishawahi kutumika kwa hawa akina RA, pale alipomkandia hadharani Mzee Mengi baada ya kutoa majina ya mafisadi papa, akiwemo RA, Manji na wengineo. Vipi Lipumba kuonekana kuwatetea hao mafisadi?

  Aidha Lipumba huyo huyo aliwahi kutetea ununuzi wa mtambo chovu na wa kifisadi wa Dowans La mwisho: Katika kampeni hizi Lwakatare amepanga kuzungumzia kile kilichomtoa CUF. Ni ushirikiano wa kifisadi baina ya baadhi ya viongozi wakuu wa CUF na hao mafisadi.
   
 5. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kuna watu humu ndani watoe maelezo msaana hii ina pande mbili, kwanza inawezekana si vibaya kwa watu kuwa na mahusiano, lakini pili inategemea mahusiano ya malengo gani.

  Nakumbuka kuna watuhumiwa wawili ambao kwa kiwango kikubwa wamekuwa wakitoa michango ya siri kwa wapinzani na huku wakijitangaza kuwa wanasaidia CCM hadharani. Pamoja na kuchangia upinzani wamekuwa wakitoa hata mipango mahususi kwa wapinzani, lakini pia kuna watu wanaotaka kuua upinzani na hasa Chadema hasa baada ya kurudi tena kwa hoja ya Kagoda na EPA... wanaona kama ssa ile "ahadi" ya kufa kwa tuhuma za EPA imevujwa?
   
Loading...