Cuf yajiandaa kuzirudisha ofisi za chama zilizoporwa na Maalim Seif

Dunia yakoo

Senior Member
Nov 23, 2019
139
214
Mnamo mwaka tarehe 18 march 2019 mahakama kuu kandaa ya Dar es salaam ilitoa hukumu ya kesi ya msingi ambayo chama cha cuf kilishtakiwa na maalim seif na baada ya mahakama kuamua kesi hiyo upanda wa maalim seif kushindwa kesi huyo hivyo waliamua kujiunga na chama cha Act wazalendo na kufanya uharibifu wa mali za CUF. ikiwa ni pamoja na kuchoma bendera na kushusha bendera kwenye ofisi za chama cha cuf huko visiwani unguja na pemba zilizojengwa kwa michango ya wabunge kwa ujumla wao au mbunge mmoja mmoja na kuzipaka rangi ofisi hizo.


Huku ofisi ya mlezi wa vyama vya siasa ikishikwa na kigugumizi na kuacha uharibifu wa uchomaji wa bendera na nembo za CUF ukiendelea hadharani.

viongozi wa cuf wamesema bila shaka maalim seif sharif ambae ni mshauri mkuu wa chama cha Act na wafuasi wake ndiyo hasa wanaotumiwa na Dr Bashiru na serikali ya ccm kwa ujumla wake.

Mshauri huyo mpaka leo anapokea 18000,000/ kila mwezi matibabu,usafiri wa ndani na safari za nje ikiwa ni moja na kumuandikia Dr shein kuomba amuidhinishie baadhi ya mambo yake huku akiwahadaa wazanzibari kuwa hamtambui Dr shein kama Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar. wakati akiwahadaa wafuasi wake serikali hii ni haramu lakini kwake yeye ni halali kwa mahitaji yote ikiwa ni pamoja na mshahara na mahitaji yote ya maisha.

Viongozi hao wamesema kama kila ahamae chama huondoka na alichochangia chamani, Babu Duni alipohamia chadema aliondoka na ofisi ?

Ofisi hizi ni za chama chetu tunaendelea na utaratibu wa kuzirejesha na serikali iache kukubali vitisho vya mtu mwenye ubinafsi kupindukia na asiejali ummoja na mshikamano wa Taifa letu.

zzz.jpg
 
Back
Top Bottom