CUF yaishauri CCM isiondoke madarakani...

CUF yaishauri CCM isiondoke madarakani...

sosoliso

Platinum Member
Joined
May 6, 2009
Posts
8,543
Reaction score
9,478
Naibu katibu mkuu wa CUF Julius mtatiro ameitaka serikali kuacha kupuuza suala la mfumuko wa bei, kwani limekuwa janga kwa wananchi na kwamba, linaweza kuleta athari kubwa kwa uchumi wa nchi.

Akizungumza kwenye ziara ya kuimarisha chama mkoani tabora juzi, mtatiro alisema imefika wakati kwa serikali ya CCM kulitizama upya suala la mfumuko wa bei kwa sababu linaweza kuiondoa madarakani.

"Suala la maisha ya watanzania siyo suala la kisiasa, kwani bila ya kusema ukweli jinsi hali ya uchumi ilivyo sasa… serikali inatakiwa kuliitafutiea ufumbuzi suala hili na kama imeshindwa iseme" alisema mtatiro na kuongeza: "kwa sasa kila bidhaa ipo juu jambo ambalo linasabisha baadhi ya wananchi kushindwa kumudu bei hizo, hali ambayo inapelekea kuanza kuishi maisha magumu ikiwamo kuombaomba.

Pia mtatiro alisema suala hilo linatokana na baadhi ya viongozi wa serikali kulifumbia macho na kuliona kama siyo tatizo, kwa sababu wanapata wepesi kutokana na fedha za walipa kodi.

"CUF inasisitiza kwamba suala la mfumuko wa bei linatakiwa kutafutiwa ufumbuzi wa haraka kwani bila ya kufanya hivyo wananchi ambao ndiyo wanaoteseka watachoka kuvumilia" alisema mtatiro na kuongeza: "kama sukari, mchele, maharagwe, unga vinazidi kupanda bei, ina maana itafika wakati wananchi ambao ni wapiga kura wao watapoteza mwelekeo wa maisha kutokana na serikali kushindwa kudhibiti hali hiyo"

Naibu katibu mkuu wa CUF Julius Mtatiro ameitaka serikali kuacha kupuuza suala la mfumuko wa bei, kwani limekuwa janga kwa wananchi na kwamba, linaweza kuleta athari kubwa kwa uchumi wa nchi.

Akizungumza kwenye ziara ya kuimarisha chama mkoani tabora juzi, mtatiro alisema imefika wakati kwa serikali ya CCM kulitizama upya suala la mfumuko wa bei kwa sababu linaweza kuiondoa madarakani.

"suala la maisha ya watanzania siyo suala la kisiasa, kwani bila ya kusema ukweli jinsi hali ya uchumi ilivyo sasa… serikali inatakiwa kuliitafutiea ufumbuzi suala hili na kama imeshindwa iseme" alisema mtatiro na kuongeza: "kwa sasa kila bidhaa ipo juu jambo ambalo linasabisha baadhi ya wananchi kushindwa kumudu bei hizo, hali ambayo inapelekea kuanza kuishi maisha magumu ikiwamo kuombaomba.

Pia mtatiro alisema suala hilo linatokana na baadhi ya viongozi wa serikali kulifumbia macho na kuliona kama siyo tatizo, kwa sababu wanapata wepesi kutokana na fedha za walipa kodi.

"CUF inasisitiza kwamba suala la mfumuko wa bei linatakiwa kutafutiwa ufumbuzi wa haraka kwani bila ya kufanya hivyo wananchi ambao ndiyo wanaoteseka watachoka kuvumilia" alisema mtatiro na kuongeza: "kama sukari, mchele, maharagwe, unga vinazidi kupanda bei, ina maana itafika wakati wananchi ambao ni wapiga kura wao watapoteza mwelekeo wa maisha kutokana na serikali kushindwa kudhibiti hali hiyo"

Source: Mwananchi

My take..
ni vizuri sasa wameanza kujitambulisha rasmi kwamba CUF ni sehemu ya CCM
 
VINEGA hoyeeee! Heading na contents haziendani!
 
Umemuwekea Mtatiro maneno ambayo HAJAYASEMA kutoka kinywani mwake;mtendeeni haki mtuhuyu hata kama sera zake hazikufurahishi!

Mtatiro na wengine wanukuliwe kwa yale waliyoyasema tu;haya unayoyasema ww yafungulie thread mpya maana ni mawazo yako ww na tutayaheshimu!
 
Kwa mara ya kwanza Mtatiro anatuambia na kufanya kazi ya upinzani "Kushauri Serikali" sio kupinga hata mazuri
 
Mtatiro sikio la kufa halisikii dawa. CUF udini mtupu........
 
Umemuwekea Mtatiro maneno ambayo HAJAYASEMA kutoka kinywani mwake;mtendeeni haki mtuhuyu hata kama sera zake hazikufurahishi!

Mtatiro na wengine wanukuliwe kwa yale waliyoyasema tu;haya unayoyasema ww yafungulie thread mpya maana ni mawazo yako ww na tutayaheshimu!

mkuu najua hupendi lakini mie cijamlisha mtatiro.. nimecopy & kupaste hapa.. soma mwananchi la leo ukurasa wa 12.. kumbuka mesenja hauwawi.. wala kuchukiwa..

Tangu lini mke akakubali ndoa ivunjwe wakaozee jela?
 
Kwa mara ya kwanza Mtatiro anatuambia na kufanya kazi ya upinzani "Kushauri Serikali" sio kupinga hata mazuri
Upinzani hauko kuishauri Serikali iliyo madarakani... hii ni nortion ya Watanzania masikini wa ufahamu. Kuna vyombo kibao vya kuishauri Serikali, mfano asasi za kirai, mabaraza ya wazee, Bunge, n.k. Nje ya Bunge ukiona upinzani unaanza kuishauri Serikali basi ujue wameanza kujigeuza kuwa vyombo hivyo.

Lengo kuu la chama cha upinzani ni kutoka kwenye upinzani na kuchukua dola. Huwezi kufikia lengo hilo kama utaishauri Serikali... what if wakifanyia kazi ushauri wako? Lazima chama cha upinzani kikosoe na kutoa approach yao juu ya tatizo.
 
"Akizungumza kwenye ziara ya kuimarisha chama mkoani tabora juzi, mtatiro alisema imefika wakati kwa serikali ya CCM kulitizama upya suala la mfumuko wa bei kwa sababu linaweza kuiondoa madarakani"

Yanazidi kutimia "CCM "B"
 
Sosoliso kwa heading hii unafaa kuandikia gazeti la shigongo,kha!
Pamoja na kwamba tumechoshwa na udhalimu wa serikali ya ccm, haituzuii kuikosoa na kuonya. Huwezi ukanyamaza hadi hali iwe mbaya kabisa, hata kama CUF ikichukua madaraka wakati hali ni mbaya kupita maelezo na wananchi wako hoi, haitamsaidia yeyote kaiti ya CUF na wananchi! Hizi ndo siasa tunazotaka. Hata kama itabaki CCM, ila hali yetu iwe nzuri!
 
mkuu king'asti.. ninashukuru kwa ushauri bt nimeibeba kama ilivyo toka kwa huko ilikokuwa.. so uciangalie sana kichwa cha habari.. angalia maudhui yaliomo..
 
Mimi binafsi ninawaona CUF kuwa waliwekewa tundu lenye mfuniko unaojifunga kwa nje ukiingia na wao wakaingia.

Serikali ya umoja wa kitaifa lilikuwa wazo zuri ila kitendo cha maalim Seif kukubali kutangazwa mshindi wa pili katika uchaguzi alioshinda kilikuwa ni cha usaliti kwa wapiga kura wengi. Wapiga kura wengi leo hii wanamuona kuwa alikuwa ni mtu wa masilahi binafsi na si mtu wa kuwatetea. CUF isingekubali matokeo 2010 leo hii ingekuwa chama imara sana.

Kibaya zaidi kilichowaumiza huku bara ni kitendo cha Maalim Seif kutoa maelekezo kuwa wabunge wa CUF wafanye kazi na CCM badala ya CDM. Hiyo ilikuwa another self inflicted wound. Watanzania wanapigia kura upinzani si kwa sababu ya kuwafanya wapate vyeo vya title bali wanataka kuondokana na CCM labla mambo yao yatakuwa mazuri. Sasa mtu yeyote au chama chochote kinapoondoa imani ya watanzania kuindoa CCM anawakataisha tamaa wananchi na hivyo kuondoa relevancy yake. Ndiyo maana nilipiga mwafaka wa CCM na CDM Arusha. Miafaka ipatikane kwenye sanduku la kura na si kuvuruga taratibu halafu mkae mezani. CUF is almost dead Bara sooner or later It will be dead Zanzibar.
 
Back
Top Bottom