CUF watoa Tamko kali juu ya mauaji ya Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF watoa Tamko kali juu ya mauaji ya Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Keynes, Jan 8, 2011.

 1. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Mh. Prof lipumba kajieleza vizuri sana kuhusu mauaji ya arusha. Kama viongozi wa siasa wote watakua na umoja kama huu lazima mabadiliko yatapatikana tu.
  source;
  Nukuu just kipengele.
  Hivi tujiulize kama kweli pana tishio la ugaidi iweje mechi za mpira ziendelee bila kuzuiwa na polisi? Mikusanyiko yote inafanyika isipokuwa maandamano ya vyama vya siasa tu? Hawa magaidi walio tishio kwa jeshi la polisi wanaotaka kulipua maandamano peke yake wametokea wapi? Kwa nini nchi hii iendeshwe kisanii na kiujanja ujanja namna hii? Kwa nini serikali inaogopa maandamano?

  CUF inalaani ukatili waliofanyiwa wakazi wa Arusha katika maandamano ya CHADEMA na kuwa ukatili huo hauvumiliki na unahatarisha amani na utulivu wa kweli wa nchi yetu.

  H@ki Ngowi
   
 2. m

  miradibubu JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 313
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mh prof amenena vema kwani anazidi kuonesha ukomavu wa kisiasa
   
 3. N

  Nonda JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Huo ni ukomavu wa kisiasa, pia ni utamaduni ambao vyama vya upinzani vinatakiwa viujenge.
  Pia kwa wale wanaokiita chama cha CUF, CCM-B watapata somo hapo. CUF wangeisifia jeshi la Polisi na serikali au vipi!!???
  Kila chama ambacho ni tishio kwa CCm kinachezea nyundo ya CCM kivyake vyake. Kuna haja ,upinzani kushirikiana katika kuleta mabadiliko ya kweli TZ! NCCR pia wametoa kauli..ni mwanzo mzuri.
   
 4. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Haya ni maneno ya busara sana kutoka kwa Prof. Lipumba. Nimekuwa nikimfuatilia hata pale ambapo wabunge wa CUF walipolaani CDM kutoka bungeni; yeye hakuonekana kufagilia. Anaheshimu mshikamano wa upinzani. Siku zote kauli zake ni za busara. Hata kwa hili ameonyesha ukomavu mkubwa sana.
   
 5. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Maandamano ni haki ya wananchi. Ni watu wendawazimu tu ndio wanaoogopa maandamano ya haki. Yaliyotokea Arusha ni funzo kwamba demokrasia wanayoitaka inataka kila mtu asonge mbele nayo. Siyo sound na blah blah tu.
   
 6. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #6
  Jan 8, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  wana Jf tunakusanyika makanisani,misikitini,misibani,kwenye harusi,vituo vya mabus hakuna fujo!fujo inaanza pale utakapo waambia polisi waje watulinde ktk mkusanyiko wetu wa siasa kwa nini?hiyo ni dalili kuwa waliopo madarakani hawataki uongozi wa kupokezana kwa kuwa siasa kwa nchi zenu ndio ugali wao na familia zao!hawapo kuwatumikia wananchi
   
 7. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Opposition parties have 1 common 'enemy' that is CCM.I hope hali hii itaendelea siku zote.bravo CUF,TLP and NCCR for the positive opinions about Arusha killings.
   
 8. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  good words,
  aliongea kama Lipumba au CUF?
  Anyway bado hainifanyi nisahau CUF walichokifanya Zenj na kugombania siti bungeni. Sijasahau pia Hamad Rashid vs Freeman Mbowe. Na post kadhaa za Mwiba!

  Again good words, but is CUF divided?
   
 9. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,274
  Trophy Points: 280

  I can't buy that story, Lipumba anatafuta public sympathy ambayo imepotea kwake. hebu twende taratibu ili tuelewane vizuri bila kuleta ushabiki wa namna yeyote.
  1. kwenye uchaguza wa spika wa bunge, wabunge wote wa CUF walimpigia kura mgombea wa CCM.
  2. kwenye uchaguzi wa meya wa mwanza juzi tu madiwani wa CCM walikuwa 13 wa cuf 2 CHADEMA 17, kura zilipopigwa Meya wa Chadema alishinda kwa kura 17 na CCM walipata kura 15, je kura za madiwani wa CUF walimpigia nani? hili haliitaji degree kulitambuwa, CUF ni CCM B period. mwenye hoja yenye mashiko na ailete kama siko shihi niko yayari kukosolewa,ila asichangie hoja hii mtu yeyote anaetumia makalio kufikiria au anaetumia tumbo kufikiria badala ya ubongo.
   
 10. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Kaka hilo nalo neno....But kwa kipindi hiki cha mauaji tusiangalie mambo ya kuwania viti sana sana tuangalie uvunjivu wa sheria unaofanywa na polisi bila kujali wao wanatakiwa kuwa chombo ambacho ni neutral.
  Polisi wanatumia katiba/sheria kulinda ccm badala ya wananchi wote.....mbona wananchi wanapolipa kodi hakuna ubaguzi wa vyama? Iweje wao watubague wakati kodi zetu zinazowalipa mishahara hazina vyama!!!!!!!!!
   
Loading...