CUF watishia kwenda ICC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF watishia kwenda ICC

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Rutashubanyuma, Dec 30, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,711
  Trophy Points: 280
  CUF watishia kwenda ICC Wednesday, 29 December 2010 20:52

  Sadick Mtulya na Elias Sichalwe CHAMA cha Wananchi (CUF) kimetishia kwenda Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kuwashitaki viongozi wa Serikali kutokana na kile kinachodai kuwa ni ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na Jeshi la Polisi nchini.

  CUF wanalalamikia polisi kuwakamata wafuasi wake 40 kwa tuhuma za kushiriki maandamano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi kwa lengo la kuwasilisha rasimu sifuri ya Katiba kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani.
  Maandamano hayo yalifanyika wakati kukiwa na marufuku ya Jeshi la Polisi inayozuia kutofanyika kwake na polisi hao kuyaita kuwa ni batili kutokana na kufanyika bila kibali chao.


  Jana, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria wa CUF, Salim Bimani aliliambia Mwananchi kuwa “Kama polisi wataendelea na ukiukwaji wa haki za binadamu, CUF ipo tayari kulifikisha suala hili ICC kuwashtaki viongozi wa nchi kwa ukiukwaji huo’’.

  Kwa mujibu wa Bimani, polisi hawakuwa na mamlaka ya kuwakamata waandamanaji hao kutokana na ukweli kwamba maandamano ni haki ya kikatiba ya kila mwananchi.

  Alisema katika maandamano hayo, watu 40 walikamatwa na kuhojiwa kwa saa kadhaa na wengine kuachiwa huru muda mfupi baadaye.
  "Hadi saa 6:00 mchana wanachama 40 waliokamatwa, lakini wamachama 36 waliachiwa baadaye hivyo ninavyozungumza hapa bado kuna watu wanne wako mahabusu,"alisema Bimani.

  Bimani alimtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha kuvidhibiti vyombo vya usalama kwa kuwa vingi, vinafanya kazi kinyume na taratibu na vinakiuka haki za binadamu. Awali akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya CUF jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Julius Mtatiro alisema rasimu ya katiba iliyowasilishwa jana wizarani ina sura 16 na ibara 131.

  “Rasimu hiyo ya Katiba imeandaliwa na wadau mbalimbali ikiwamo kunakiliwa kutoka kwenye katiba zaidi ya 30 za nchi mbalimbali duniani zikiwemo za Afrika na Ulaya,’’ alisema Mtatiro. Kwa mujibu wa Mtatiro, Sura ya tano, ibara ya 32 ya rasimu hiyo inahusu uwepo wa Rais wa Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania ambaye atakuwa mkuu wa nchi, kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.

  Juzi majira ya saa 2:00 asubuhi polisi wenye silaha walifika ofisi za CUF kudhibiti maandamano ambapo waliwatangazia wananchi hali ya hatari na kuwataka wajifungie majumbani mwao huku wakifyatua risasi za moto na kurusha mabomo kuwatawanya.

  Mara baada ya tangazo hilo, wananchi walianza kukusanyika kwa wingi nje ya makao makuu ya chama hicho wakiwa na mabango mikononi na vitambaa vilivyoandikwa ujumbe mbalimbali wa kudai katiba mpya. Baada ya hapo, magari hayo ya polisi yaliyokuwa yamesheheni askari wenye silaha nzito za moto na mabomu ya kutolea machozi, yaliondoka na kwenda kuegeshwa katika makutano ya barabara ya Uhuru na barabara ndogo inayoingilia Makao Makuu ya CUF eneo la Rozana.

  Baadaye waandamanaji walianza maandamano na walipofika Rozana, magari ya polisi yaliondoka na kwenda kuegeshwa katika kituo cha mabasi cha Buguruni Malapa, ambako gari maalumu la kumwaga maji ya kuwasha maarufu kama deraya, lilikuwa limeegeshwa.

  Baada ya kuona hivyo waandamanaji walijipa moyo na kuona labda polisi wanawaogopa na hivyo kuingia moja kwa moja katika Barabara Kuu ya Uhuru kuelekea mjini. Lakini, walipofika Malapa, walikumbana na kizuizi cha magari ya polisi zaidi ya sita ya FFU na deraya nyingine. Hapo ilikuwa kama mchezo wa kuigiza baina ya FFU na waandamanaji, baada ya kila upande kumtunishia msuli mwingine. Wakati polisi wakiwataka wanachama hao wasalimu amri na kusitisha maandamano yao, wanachama hao wanajibu "Kuandamana ni haki yetu kikatiba.

  " Wakiwa wanatunishiana misuli katika kituo cha mabasi cha Malapa, gari moja la FFU lilikaa katikati ya barabara na dereva wake alitangaza tena “Tafadhali hili gari usilipite, ukilipita hili gari unatafuta shari.” Lakini pamoja na tangazo hilo, wanachama hao waliendelea kulipita gari hilo na mkuu wa operesheni ya polisi hao akaruhusu gari la maji ya kuwasha kuanza kuwarushia maji.

  Wakati hayo yakiendelea, daladala na magari yote yanayotoka na kwenda Buguruni yalikuwa yamezuia kupita na kupaki pembeni ama kwa amri au kwa hofu yao wenyewe. Baada ya kuona kizuizi hicho waandamanaji hao waliamua kuingia mitaani na kwenda kuibukia katika mitaa ya Amana na Ilala Boma na kuendelea na safari ya kuelekea wizarani. Wakati huo polisi walikuwa wameachwa Malapa.

  Polisi hao walisituka kwamba maandamano yanaendelea wakati waandamanaji hao walipokuwa tayari wamefika eneo la Karume na Mchikichini. Maandamano yalipofika kati ya mitaa ya Ilala Boma na Karume, polisi hao ambao walikuwa tayari wameshajawa na hasira kwa mchezo wa sinema waliokuwa wakichezewa na waandamanaji, waliamua kufyatua risasi za moto kuwatawanya.

  Pia mabomu kadhaa ya kutoa machozi yalilipuliwa katika mitaa hiyo jambo ambalo lilisababisha waandamanaji hao kuanza kupoteza mwelekeo huku baadhi ya viongozi wao, wakifanikiwa kupita kwa gari la chama lenye bendera. Baadaye maandamano hayo yalifanikiwa kufika ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria ambako viongozi wa CUF walikabidhi rasimu yao ya katiba. Mwisho
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,711
  Trophy Points: 280
  Serikali ya umoja kule Zanzibar kumbe sasa mwafahamu kilikuwa ni kiini macho...............
   
 3. N

  Nonda JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  haya maandamano ya katiba hayakufanyika Zanzibar.
  kule walibadilisha katiba yao baada ya kura ya maoni.

  CCM wanajulikana kwa mazingaombwe na kiini macho lakini CUF ni chama at least kinachoonesha uthubutu. Wanaonesha njia kwa wapenda mageuzi.
  CCM wameufanya umma wote wa Tanzania makondoo.

  CUF wametoka mbali. Let us give credit when they deserve it and let us criticise them when they deserve critics.

  Not only blames all the time!! Just because they are CUF.
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,711
  Trophy Points: 280
  CUF yamuonya Nahodha


  na Asha Bani


  [​IMG] CHAMA cha Wananchi (CUF) kimemuonya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha, kwamba anaweza kuwa waziri wa kwanza wa Tanzania kushtakiwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Uhalifu (ICC) kwa kuvunja haki za binadamu. Akizungumza na waandishi wa habari jana Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Sheria, alitoa onyo hilo kwa Nahodha baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kutumia nguvu ya silaha katika kuwasambaratisha wafuasi wa chama hicho walioandamana juzi jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwasilisha rasimu ya Katiba mpya.
  Alisema ingawa Nahodha katika wizara hiyo ni mgeni lakini anatakiwa kuwa makini na jeshi lake ili yasijejirudia yale yaliyotokea mwaka 2001 ambapo kwa mujibu wa tume iliyoongozwa na Hashim Mbita watu 31 walipoteza maisha.
  Alisema endapo vitendo hivyo vya kutumia nguvu vitaendelea bila viongozi wenye dhamana kuingilia kati Nahodha atashtakiwa akifuatiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutokana na kuliacha jeshi likimwaga damu bila sababu.
  Hata hivyo, Bimani alisema katika wanachama 40 waliokamatwa jana, tayari wanachama 35 wameachiwa huru huku watano wakiwa bado wameshikiliwa na jeshi hilo.
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,711
  Trophy Points: 280
  Point noted........................lakini kama CCM wapo pamoja na CUF kwenye serikali ya umoja..........don't you think that CUF deserves some respect from CCM too, in acknowledgement of sacrifices offered in Zanzibar?

  Hoja ya kuwa CUF wametoka mbali ni ya kweli lakini uongozi wa Prof. Lipumba na Seif umechangia sana kuwaondoa kwenye chati hususani bara na hili limejionyesha kwenye kura za 2010.......................CUF kilikuwa Chama Kikuu cha upinzani sasa Chadema has taken over..................................kisa demokrasia ni finyu sana ndani ya CUF yenyewe............................

  Iweje Lipumba tu ndiye anayeteua viongozi wote wa juu wa chama hicho.............yaani anapanga safu za marafiki zake tu.....................na hata hiyo katiba yao kwani imepitishwa na vikao gani ndani ya CUF ukiwauliza waliokuwa wanaandamana ni lini waliipitisha?

  Ukiwauliza walioandamana hivi mapendekezo ya rasimu yanasemaje wafikiri hata wanajua?

  It is true CUF has come a long way but from where?

  That is a question begging for an introspective response.................
   
 6. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Hawa ccm-b nao.............sasa wanahangaika nioni wakati kuna mwafaka?.................wasiutupotezee muda
   
 7. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Ninapokitazama CUF naona wamejitahidi kuleta demokrasia Tanzania japo kama ni kwa hatua ndogo.

  Wengi tunafikiri CUF ingeacha isikubali serikali ya umoja wa kitaifa na sababu kubwa tunasema damu iliyokwisha mwagika Pemba. Tumejiuliza hao Wazanzibari hususan Wapemba wenyewe wanalichukuliaje suala hilo? Kwa mujibu wa viashiria nitavyoviainisha ninaona CUF wametenda kile Wazanzibari walichokuwa wanakitaka na sio kujichukulia madaraka kama tunavyotaka kuamini.

  1. Kura za maoni zilizopigwa zimeonyesha kuwa Wazanzibari wanataka serikali ya Umoja wa Mataifa na hivyo kwenda kwenye uchaguzi wakijua kuwa matokeo ni Serikali ya Umoja wa Kitaifa bila ya kujalisha mshindi(kwa kujua kuwa CUF itashinda na kura zitaporwa)

  2. CUF imepata majimbo zaidi Zanzibar (imekubalika zaidi)

  3. Asilimia ya watu waliopiga kura Pemba ni kubwa

  4. Kura zilizopata CUF Pemba (huko damu ilikomwagika) ni nyingi sana kulinganisha na CCM ikimaanisha kuwa watu licha ya kujua kuwa kutakuwa na serikali ya Umoja wa Kitaifa waliendelea kuipigia kura CUF. (Asilimia 70 tu ya watu walipiga kura katika Jimbo la Kiembe Samaki ambayo imetajwa kuwa ni ngome ya CCM ikiashiria kuwa hawa hawakuridhika na vyama vyote viwili na SUK)

  5. Ikiwa ni mwezi tokea kumalizika kwa uchaguzi hatujasikia Wazanzibari hasa Wapemba kulalamika kuwa 'damu yao ilimwagika bure' hadi hivi sasa.

  Sasa ikiwa hicho ndicho raia walichotaka tulitaka CUF waache kutumia fursa hiyo na wang'ang'anie ushindi, watu zaidi wafe, na raia wawashangae?
   
 8. N

  Nonda JF-Expert Member

  #8
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Tanzania ina serikali mbili.

  Na kama tujuavyo CCM si binadamu..... hata sijui ni kina nani!!!???
  Kule Zanzibar pia watasabotage huo muafaka ili kuzuia kitu kama kile kisije huku bara.
  kwa hiyo, CCM respect no one and they have no mercy.
  Ukiwapa nafasi wanakutwangwa nyundo yao, ukigeuka upande wa pili wanakulamba kwa jembe. that is CCM.

  Inawezekana CCM wanataka repeat ya same process ilivyotokea Zanzibar ijirudie bara.
  Mogogoro kwanza, mpasuko uje kwanza, watu wauwawe kwanza halafu vikao vya chama ,tena ndio ije suluhu au muafaka..itakuwa miafaka mingi kabla ya kuutekeleza japo mmoja.
  Demokrasi ndani ya Chama haiko kwa chama chochote hapa TZ, mkuu.

  Ama lini waliandika rasimu au nani aliipitisha hapo sina jibu ila nafikiri zamani Upinzani waliwahi kuandaa rasimu, labda wameifuta mavumbi tu.
  Hata hivyo mkuu, unazifahamu vyema siasa za Tanzania!! Usitake nipayuke hapa....
   
 9. N

  Nonda JF-Expert Member

  #9
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  mkuu,

  nyimbo yako ni nzuri..nani amekufunza? au unakariri tu ,unayoyasikia?
  soma historia ya vyama vya siasa TZ...
  anzia 1977....1992 hadi leo.

  Uone kama utakuwa na msimamo huu ulionao leo.

  Waswahili husema asiyejua maana ..haambiwi maana.
  nimekusaidia mkuu, usifuate mkumbo, usiongengee kwa ushabiki pekee.

  Nenda library ujielimishe kidogo kuhusu siasa za TZ na vyama vya siasa.
  Kila la heri,mkuu.
   
 10. C

  Chuma JF-Expert Member

  #10
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kuna watanzania wengi tu Katiba ya sasa hawaijui...na nimeona facebook kuna mtu ka-amecomment....kuwa watanzania wangapi wanajua RANGI tu ya Cover ya Katiba ya sasa? lkn leo hii madai ya Katiba MPYA yamekuwa mengi...?

  ...Hivi wote tumesoma katiba ya sasa au tunafuata upepo wa wanasiasa? Usiwalaumu tu wafuasi wa CUF...!!!
   
Loading...