CUF watema cheche wilayani Tunduru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF watema cheche wilayani Tunduru

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Stephano Mango, May 7, 2012.

 1. S

  Stephano Mango Verified User

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Na Steven Augustino, Tunduru

  WAKULIMA wa Mpunga Wilayani Tunduru wametakiwa kuukataa kuuza mpunga wao kupitia mfumo wa Stakabadha gharani na kugoma kulipa ushuru kulingana na maelekezo yaliyotolewa na Halmashauri ya wilaya hiyo .


  Pamoja na wito huo wakulima wa mazao hayo pia wamehimizwa kuwa na mshikamano wa kugomeaa tozo za ushuru ambao umedaiwa kutozwa na Halmashauri ya Wilaya hiyo hata kwa wakulima wanao ingiza mazao yao kutoka shambani.


  Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Viongozi waandamizi wa Chama cha wananchi CUF wa Wilaya ya Tunduru kwa ushirikiano wa viongozi wa chama hicho kutoka Mkoani Mtwara wakati wakiongea na wananchi katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya baraza la Idd mjini hapa.


  Akifafanua hotuba hiyo Mgeni rasmi katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chama cha wananchi Cuf Wilaya ya Tandahimba na Mgombea wa Ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 Katani Mohamed alisema kuwa ukosefu wa wataalamu wabunifu na uvivu wa kujituma kwa viongozi katika halmshauri hiyo ndiko kuliko wasukuma kuandaa utaratibu huo huku
  wakifahamu wazi kuwa mpango huo unalenga kuwaibia wakulima hao.


  Huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo Katani aliwahimiza kudai haki zao bila kuogopa jambo lolote kwani vitendo hivyo vya unyonyaji ni hatari kwa ustawi wa jamii

  Katani aliendelea kueleza kuwa kinachowafanya viongozi hao kufikia hatua hiyo ya kuchukua maamuzi bila kuwashirikisha wananchi kinatokana na wanatunduru wenyewe kulala usingizi wa pono na akatumia nafasi hiyo kuwataka waamke kudai haki zao vinginevyo watajikuta wameuzwa katika maeneo yao.


  Alisema wakati viongopzi hao wakifikilia kuingiza zao hilo katika mfumo huo viongozi hao bado wameendelea kuwa kero katika utoaji wa msaada kwa wakulima wakorosho ambao pia waliingizwa katika mkenge huo bila kuwepo kwa makubaliano.


  Akizungumzia tozo kwa wakulima wa mpunga alisema ingawa viongozi hao wanafahamu maelekezo na miongozo ya tozo hizo iko wazi kuwa anayetakiwa kulipa ushuru ni mtu yeyote au mfanyabiashara anayeondoka na shehene ya chakula kutoka ndani ya wilaya husika.


  Wakitoa salamu kutoka mkoani Mtwara Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Cuf Taifa Reherma Mautuka, Katibu wa Cuf Wilaya ya Tandahimba Shaban Namaneha,Katibu wa Cuf Mtwara Mjini Said Mdoya na Mkurugenzi wa haki za binadamu Wilaya ya Tandahimba Alfonce Andrew walisema kuwa mikikimikiki ambayo imekuwa ikijitokeza katika Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara imetokana na kuchoshwa na vitendo vya unyanyasaji kutoka kwa viongozi wao.

  Awali akimkaribisha msemaji mkuu katika mkutano huo mwenyekiti wa CUF
  Wilayani humo Abdalah Mtalika alidai kuwa kitendo cha kuwatoza wakulima Ushuru huo wakati wakiingiza mazao yao kutoka Shambani ni cha uonevu kwavile wakazi wote wa mji huo hulima vijijini.
  Mwisho   
 2. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hiki chama bado kina exist
   
 3. Suzie

  Suzie JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 1,264
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Picha tu ndo suluhisho hatusomi dessertations hapa
   
 4. M

  Molemo JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  CUF bana! Bado mnang'ang'ana tu.
   
 5. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Go 2 hell CUF, mlifanya makosa makubwa pale mwanzo mlipoacha ungangari wenu na kukubali kuposwa na CCM kwa ajili ya watu wachache 2, Tunamshukuru Mungu wa peoples ambaye ameyaruhusu yote haya ili CHADEMA tupate mfano kutoka kwenu CUF ili tusije tukajikwaa kama nyie.

  Shardcole@Tabora1
   
 6. ijoz

  ijoz JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 661
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 80
  Mi nafikiri what is needed ni kuondoa gamba kwny dola so watunduru kuchange their mentality toward CCM is a good start.
   
 7. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Cuf.....!!!!?????
   
 8. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  R.I.P CUF,naskia Mtatiro anatimkia ccm
   
Loading...