CUF wataka serikali ya umoja wa kitaifa bara

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,742
Claud Mshana

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema matatizo ya kiuchumi yanayoikabili Serikali yatamalizwa kwa kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. CUF imesema Serikali ya Rais Jakaya Kikwete imeelemewa na majukumu ya kuongoza na hivyo kuhitaji msaada kwa kuundwa serikali hiyo kama ilivyo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, visiwani.

Tamko la Baraza Kuu la Uongozi Taifa la chama hicho lililotolewa jana na Makamu Mwenyekiti wa Cuf taifa, Machano Khamis Ali lilisema Serikali ya CCM kushindwa kutatua matatizo makubwa yanayolikabili taifa ni dalili za kuwepo kwa ombwe la uongozi.

Ali alitaja matatizo hayo kuwa ni kuyumba kwa uchumi, kushuka kwa kiwango cha mapato ya serikali, kuporomoka kwa shilingi na mfumuko wa bei na matatizo ya ajira. “Baraza Kuu linaona njia pekee ya kulitoa taifa hapa tulipofikishwa ni kwa rais Jakaya Kikwete na CCM kukubali kusaidiwa dhamana ya kuongoza nchi kwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Ali.

Aliongeza kuwa hatua hiyo pia itaisaidia nchi kuvuka salama katika mchakato wa kuandika katiba mpya ambayo itasaidia kuyapatia ufumbuzi matatizo hayo. Ali alisema serikali ya CCM imeshindwa kutatua tatizo la upatikanaji wa nishati ya umeme na kuongeza kuwa tatizo la nishati hiyo linachangiwa na kuingizwa siasa na si utaalamu au rasilimali fedha.

“Miaka 50 baada ya kupata uhuru, hatuna sababu ya kutokuwa na umeme wa uhakika, serikali imeshindwa kutatua tatizo hili na kusababisha nchi kupata hasara kubwa kwa kudhoofisha uchumi wa nchi,” alisema. “Baraza Kuu linaitaka serikali ya CCM kufanya maamuzi mazito ya kuwashughulikia wahusika wote wa uzembe huu kwa kuwachukulia hatua zinazofaa,” aliongeza Ali.

Alifafanua kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar imefanikiwa katika kipindi cha mwaka mmoja kwa kusimamia uendeshaji wa shughuli za serikali katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupanda kwa bei ya zao la karafuu.

Katiba mpya Kuhusu mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya, chama hicho kilisema rasimu mpya ya muswada huo bado inakasoro kwani bado umeweka madaraka na mamlaka makubwa kwa rais katika kudhibiti na kuamua mchakato wa kuandika katiba mpya.

“Hili linavunja msingi mmoja wa madai ya katiba mpya ambayo ni kupunguza madaraka makubwa ya rais,” alisema na kuwataka wabunge wa Cuf kuhakikisha wanasimamia marekebisho yake ndani ya Bunge linalotarajiwa kuanza keshokutwa.

chanzo: http://mwananchi.sekenke.com/
 
CUF imebadilisha nini Zenj kuwa kwenye serikali ya kitaifa? Hakuna watakachoweza kubadilisha bara kwani watacheza tu ngoma ya CCM. Maalim kaona utamu ws madaraka kamnong‘onezea Lipu ashinikize bara. japo cwapendi ccm lakin najua Cuf hawawezi kuleta mabadiliko ya maana bara bora hata znzb
X[QqUOTE=MziziMkavu;2766624]Claud Mshana

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema matatizo ya kiuchumi yanayoikabili Serikali yatamalizwa kwa kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. CUF imesema Serikali ya Rais Jakaya Kikwete imeelemewa na majukumu ya kuongoza na hivyo kuhitaji msaada kwa kuundwa serikali hiyo kama ilivyo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, visiwani.

Tamko la Baraza Kuu la Uongozi Taifa la chama hicho lililotolewa jana na Makamu Mwenyekiti wa Cuf taifa, Machano Khamis Ali lilisema Serikali ya CCM kushindwa kutatua matatizo makubwa yanayolikabili taifa ni dalili za kuwepo kwa ombwe la uongozi.

Ali alitaja matatizo hayo kuwa ni kuyumba kwa uchumi, kushuka kwa kiwango cha mapato ya serikali, kuporomoka kwa shilingi na mfumuko wa bei na matatizo ya ajira. “Baraza Kuu linaona njia pekee ya kulitoa taifa hapa tulipofikishwa ni kwa rais Jakaya Kikwete na CCM kukubali kusaidiwa dhamana ya kuongoza nchi kwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Ali.

Aliongeza kuwa hatua hiyo pia itaisaidia nchi kuvuka salama katika mchakato wa kuandika katiba mpya ambayo itasaidia kuyapatia ufumbuzi matatizo hayo. Ali alisema serikali ya CCM imeshindwa kutatua tatizo la upatikanaji wa nishati ya umeme na kuongeza kuwa tatizo la nishati hiyo linachangiwa na kuingizwa siasa na si utaalamu au rasilimali fedha.

“Miaka 50 baada ya kupata uhuru, hatuna sababu ya kutokuwa na umeme wa uhakika, serikali imeshindwa kutatua tatizo hili na kusababisha nchi kupata hasara kubwa kwa kudhoofisha uchumi wa nchi,” alisema. “Baraza Kuu linaitaka serikali ya CCM kufanya maamuzi mazito ya kuwashughulikia wahusika wote wa uzembe huu kwa kuwachukulia hatua zinazofaa,” aliongeza Ali.

Alifafanua kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar imefanikiwa katika kipindi cha mwaka mmoja kwa kusimamia uendeshaji wa shughuli za serikali katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupanda kwa bei ya zao la karafuu.

Katiba mpya Kuhusu mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya, chama hicho kilisema rasimu mpya ya muswada huo bado inakasoro kwani bado umeweka madaraka na mamlaka makubwa kwa rais katika kudhibiti na kuamua mchakato wa kuandika katiba mpya.

“Hili linavunja msingi mmoja wa madai ya katiba mpya ambayo ni kupunguza madaraka makubwa ya rais,” alisema na kuwataka wabunge wa Cuf kuhakikisha wanasimamia marekebisho yake ndani ya Bunge linalotarajiwa kuanza keshokutwa.

chanzo: http://mwananchi.sekenke.com/
[/QUOTE]
 
CUF wanachohitaj huku bara ni wao wapite na ving'ora kama seif huko zenji
 
hawana jipya hawa cuf-sitaki hata kuwasikia
 
Ni gumu sana kulikubali hili kama tunavyo wafahamu hawa jamaa, eg Walishauliwa sana kuunda baraza dogo la mawaziri kama walivyo jamaa zetu wa Rwanda, ili kuepusha mzigo wa uendeshaji kwa WALIPA KODI lakini kinyume chake baraza ni kubwa tena zaidi ya lile la kwanza

Wameunda wizara ambazo hazina hata mashiko eg sijui wizara Mahusino hii ya Bw. Tyson Jiulize hivi kama hakuna mahusiano mazuri baina ya viongozi wa CHADEMA waziri ata kwenda kusuruhisha
(kama alivyo fanya kwa UVCCM-Arusha) mbona hakufanya hivyo wakati wa mgogoro wa madiwani Arusha.

Matatizo tunayo yapata sisi ni ukubwa wa baraza la mawaziriambao hawajui hata wajibu wao hata wakipewa semina elekezi ngapi hii ndiyo maana inaonyesha kuwa Tz tuna mawaziri kama wawili hivi yaani Dr. Magufuli na Pro. Tibaijuka
 
CUF sasa c wa kuwatilia maanani, achaneni nao 2015 hamtawasikia tena!
 
Ivi bado tu hawajapata mtoto katika ndoa yao?nasikia jana ndo ilikuwa inatimiza mwaka mmoja.
 
Wamefanikiwa kwa kuongoza kijiji eeehh.!!? CuF kwa sasa hawana dira wanatapatapa tu kila kukicha..!!?
 
Serikali ya kikwete haijaelemewa na majukum bali imeelemewa na mafisadi wasitudanganye hawa cuf
 
Naona Mahaba ya pwani yamewakolea. Do they reall mean, Dr Slaa, Mbowe, Lissu, Mnyika et al wakae cabinet moja na kina Mwigulu, Nape, Chenge et al.

MAFUTA HAYACHANGANYWI NA MAJI.

Wewe hujawaelewa. Wana maana Lipumba, Mtatiro, et al wakae kwenye cabinet moja na hawa vikongwe wa CCM akina Wassira. Mimi naona poa tu. Kama Zanzibar imewezekana why not Tanganyika?
 
Serikali ya mseto zanzibar imefanya nini?
Hivi kuna serikali ya bara?
 
CUF imefilisika kisera wamegundua hawawezi kuingia madarakani kwa njia ya kura sasa wanategemea kupata ulaji kupitia mgongo wa mabwana zao wa CCM, mimi nililiona mapema na kuamua kuwakimbia na kujiunga na makamanda wa chadema
 
Naona Mahaba ya pwani yamewakolea. Do they reall mean, Dr Slaa, Mbowe, Lissu, Mnyika et al wakae cabinet moja na kina Mwigulu, Nape, Chenge et al.

MAFUTA HAYACHANGANYWI NA MAJI.

well said.
 
.........teh teh teh, CUF wamezoea kunyonga, vya kuchinja watawezea wapi, hii sio Zenji bana
 
ile ajali ya Islander hiyo SUK imesaidia nini? acha ujinga wewe mmeshindwa kuing'oa CCM kwenye sanduku la kura sasa unalilia undugu! Fikra mbovu hizi...
 
Back
Top Bottom