Frey Cosseny
JF-Expert Member
- Feb 4, 2015
- 1,984
- 1,405
THE CIVIC UNITED FRONT
CUF - Chama cha Wananchi
CUF - Chama cha Wananchi hakina sababu ya kumjibu Mtatiro na Genge lake, bali kwa kua kumeibuliwa hoja inayohusu Viongozi halali wa Cuf, tunaona Kuna haja ya kutoa ufafanuzi Kuhusu Jambo hili.
Chama cha Wananchi kinaongozwa na Utaratibu wake wa Kikatiba. Kwa hivyo anaejiona kua ni Kiongozi wa Kitaifa wa Chama hiki ni vyema aje kwenye Vikao vya Chama ili aweze kupata ufafanuzi wa hoja hii badala ya kulalama kwenye Vyombo vya Habari. Katibu Mkuu wa Chama hiki ni Maalim Seif Shariff Hamad na Mwenyekiti wa Chama hiki ni Prof Ibrahim Haruna Lipumba. Ni kweli Cuf tumeomba Fedha zetu za Ruzuku ili ziweze kutusaidia kwenye Uchaguzi huu wa Madiwani katika Kata 20 kwa upande wa Tanzania Bara.
Ni vyema Watanzania wakafahamu kwamba kupitia kwa Shaweji Mketo, upande wa Maalim Seif Shariff Hamad umetamka bayana kwamba haujasimamisha Mgombea kwenye Kata yoyote katika Uchaguzi huu Mdogo unaotarajiwa kufanyika January 22 Mwaka huu. Upande wa Bara Cuf imesimamisha Wagombea kwenye Kata 14 kati ya Kata 20 zinazopaswa kurudia Uchaguzi.
CUF, Chama cha Wananchi upande wa Bara hatuwezi kuacha kusimamisha Wagombea na kuamua kuunga Mkono Wagombea wa Chadema kama ilivyoelekezwa na Katibu Mkuu tu, kupitia Shaweji Mketo. Kuhusu suala la Ruzuku ni kweli kwamba Ofisi ya Msajili ilisimamisha Ruzuku kwakua, ilipokea Malalamiko toka kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa na baadhi ya viongozi Kuhusu kuvurugika kwa Mkutano huo kulikotokana na ukiukwaji wa Katiba ya Cuf. Kwa sasa Mgogoro huo haupo, kwa hivyo sisi tumeomba Ruzuku hiyo ambayo ni Haki yetu kama Chama, na kwakua Mgogoro umekwisha, Msajili hana sababu ya kuendelea kusimamisha Ruzuku hiyo.
Ni kweli pesa hizo zimeingizwa kwenye akaunti ya Chama na zinatumika kwenye Shughuli za Chama ikiwa ni pamoja na Uchaguzi wa Udiwani unaorudiwa katika Kata 20 hapa Tanzania Bara. Lakini Maalim Seif Shariff Hamad na Genge lake kama wakweli, basi waeleze pia kua Mwezi October wametoa Milioni 86 kwenye akaunti ya NBC bila ya kuhusisha upande wa pili wala kumuhusisha Naibu Katibu Mkuu Bara Magdalena Sakaya ambae ni Mmoja ya watia saini kwenye akaunti hiyo. Kwa upande wetu hatukuona shida pamoja na kutojuliswhwa kwakua tunajua kua pesa hizo zinaenda kwenye Uchaguzi wa Jimbo la Dimani. Mtatiro hawezi kuyafahamu haya kwakua si Kiongozi wa Chama hiki.
Tunawataka Wanacuf kupuuza kelele hizo kwakuwa zinalenga kuwatoa kwenye Harakati za kutafuta ushindi wa Chama na Wagombea wetu kwenye Uchaguzi huu wa Madiwani. Si kosa na wala hakuna shida yoyote kwa Ofisi ya Msajili kutupatia Ruzuku hiyo na kama Kuna Kiongozi yeyote ambae yupo kwa mujibu wa Katiba yetu na anataka kujua Matumizi yake basi asubiri Vikao vya Chama.
Abdul Kambaya
Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
HAKI SAWA KWA WOTE