CUF Wachapana Makonde Dar! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF Wachapana Makonde Dar!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Jun 21, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Jun 21, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  MCHAKATO wa ubunge wa Viti Maalum jimbo la Segerea kupitia Chama cha Wananchi (CUF), juzi uliingia dosari baada msimamizi wa uchaguzi huo kutoweka na masanduku ya kupigia kura huku baadhi ya wanachama wakichapana makonde.
  Tukio hilo, lilitokea usiku wa kuamkia jana katika ukumbi wa Ukonga Hill Tec uliopo Banana Dar es Salaam, mara baada ya zoezi la kupiga kura, ambapo inadaiwa wagombea wawili katika kinyang’anyiro hicho, Asha Bani na Ashura Mustafa walikuwa wakisubiri matokeo na mara ghafla uliibuka mzozo wa kutaka matokeo yasitangazwe kutokana na kile kilichodaiwa Bani ameibuka na ushindi.

  Mashuhuda wa tukio hilo waliliambia Tanzania Daima kuwa msimazi wa uchaguzi huo aliyefahamika kwa jina moja la Zumba, alishindwa kufanya hivyo kutokana na idadi ya kura kuzidi.

  “Kulikuwa na vurugu kubwa, msimamizi alidai kura tano zimezidi kutoka kwa wajumbe na kudai hawezi kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, na kukimbilia makao makuu kwa ajili ya ufafanuzi zaidi,” walisema.

  Kwa mujibu wa mashuhuda hao, msimamizi huyo alifika makao makuu, alishauriwa kuhesabu kura hizo, ambapo alishindwa kutii amri hiyo na kushikilia msimamo wake.

  Hata hivyo, Tanzania Daima ilipowasiliana na Zumba alikiri kutokea kwa matukio hayo, na kudai alishindwa kutangaza matokeo kutokana na sababu za msingi zikiwemo za kuongezeka kwa kura tano za wajumbe huku idadi kamili ikiwa 110.


  Source: Tanzania Daima.
   
 2. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  ngunguli jino kwa jino, jicho kwa jicho, bichwa kwa bichwa. wanatuchafulia upinzani hawa jamaa.
   
 3. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  mapema hiviiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii??????????????????????????????????????????
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  bado duni haji atwangane makonde na maalim seif
   
Loading...