..CUF lazima waelewe kwamba wamekalia "mgodi wa almasi" wa mtaji wa kisiasa.
..kwa muda mrefu sana wamekuwa wana-guarantee ya kushinda majimbo yote ya Pemba.
..Prof.Lipumba na CUF wakigangamala huku Tanganyika na kupata hata viti 30 tu vya ubunge wa Muungano wanaweza kuleta mabadiliko makubwa sana ya kisiasa,kijamii,na kiuchumi.
..kwa upande wangu nadhani CUF Tanganyika wanapaswa kujirekebisha haraka sana kwa manufaa ya wa-Tanganyika na wa-Tanzania kwa ujumla.
..naamini mzigo wa kuikuza CUF haipaswi kuachiwa Wapemba peke yao. wameshajitoa mhanga mpaka kupoteza maisha yao, sasa mnataka wafanye nini zaidi?
JokaKuu
Umetowa changamoto poa kabisa.
CUF ingekuwa imeweza kujenga mtandao mpana kila sehemu ya Tanzania kama CCM wasingetumia hoja ya Udini na Ugaidi dhidi ya CUF.
CCM wanatumia hoja ya Udini na uvunjivu wa amani dhidi ya CHADEMA sasa hivi.
Kwa hiyo, kila Chama kinachochipuka kuwa tishio kwa CCM kinaandaliwa mikakati kabambe ya kukivuruga.
Kuna suali zima la nyezo, hapa nyenzo kuu ni fedha na wanachama wa vyama hivyo kujitolea kuhakikisha wanapata wafuasi wengi. Muamko wa wananchi wengi wa kisiasa ni mdogo sana sehemu nyingi za Tanzania. kwa hiyo ni imani yangu kuwa vyama vya upinzani vitapanuwa mitandao yao kwa kadiri watakavyopata nyenzo. Uelewa wa sera za vyama kwa watanzania wengi ni mdogo, wananchi hawajapatiwa elimu ya uraia (civic education) ya kutosha ya kuweza kujuwa haki zao na wajibu wao na hivyo wanapiga kura kimazoea au kwa wasifu wa mgombea siyo kwa uchanganuzi wa sera za vyama . Sio kila mwananchi anataka awe ni mwanachama wa chama cha siasa, lazima kuwe na nafasi pia ya independent voters!
Uchaguzi uliomalizika umeipatia CUF wabunge ingawaje ni wachache huku bara so call that a step forward hata kama ni leap- frog step!
CHADEMA wamepata wabunge wengi kuliko wapinzani wengine. Mafanikio haya yasiwavimbishe kichwa CHADEMA ,lakini still ni kidogo katika ujumla ya idadi wa wabunge bungeni. wajitahadhari,Wajiandae na rungu la CCM kama walivyofanywa NCCR 1995,CUF 2000 na 2005.
Sina nia ya kusema kuwa CUF au CHADEMA au Chama chengine chochote cha upinzani waridhike na mafanikio waliyoyapata ila iwe chachu ya kuona kuwa watanzania wanataka mabadiliko ya kweli.
That brings me to the point which I think is very important, wapinzani waelekeze nguvu zao kuidondosha CCM.Viache siasa za majitaka baina yao. Lakini la muhimu zaidi ni kudai Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi na kupeleka ujumbe kwa vyombo vya umma na dola kuwa viwe neutral, vijielewe kuwa hivyo ni vyombo vya umma si vyombo vya vyama. Hivi sasa vyombo hivi vinafanya kazi kama vile viko chini ya mfumo wa chama kimoja.