CUF Tanganyika itajengwa na nani?

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,269
54,664
..CUF lazima waelewe kwamba wamekalia "mgodi wa almasi" wa mtaji wa kisiasa.

..kwa muda mrefu sana wamekuwa wana-guarantee ya kushinda majimbo yote ya Pemba.

..Prof.Lipumba na CUF wakigangamala huku Tanganyika na kupata hata viti 30 tu vya ubunge wa Muungano wanaweza kuleta mabadiliko makubwa sana ya kisiasa,kijamii,na kiuchumi.

..kwa upande wangu nadhani CUF Tanganyika wanapaswa kujirekebisha haraka sana kwa manufaa ya wa-Tanganyika na wa-Tanzania kwa ujumla.

..naamini mzigo wa kuikuza CUF haipaswi kuachiwa Wapemba peke yao. wameshajitoa mhanga mpaka kupoteza maisha yao, sasa mnataka wafanye nini zaidi?
 
Bro Jokakuu...mada yako ni muhimu sana. kama walengwa Viongozi wa CUF wakiipata hii itasaidia sana...Wakati mwingine unapokubali weakness zako ni sehem ya Kujirekebisha.

Bahati mbaya kama utafanya utafiti utagundua matatizo mengi ya Vyama vya Upinzani yanafanana saana....

Moja ya Matatizo ambayo nayaona ni kuwa wasomi wengi bado hawajaingia ktk Vyama vya siasa, wachache waliopo hawawezi kuleta mabadiliko pekee yao. Na ndani ya wasomi kuna wale wa kale na wale Vijana wa sasa ambao hulka ya Vijana hupenda sana mabadiliko ya haraka...kunapokuwa na Ukinzani wa aina yoyote Vijana wengi wanaloose temper....!!! na huamua kuachana na SIASA...
 
Lipumba apigwe chini toka awe mwenyekiti amefanya nini bara bora alipokuwepo Mapalala.
 
CUF wamekuwa ''wanashiriki'' kila uchaguzi (hasa nafasi ya urais) huku Tanganyika kama formality tu - ili kuwapa support CUF ya Zanzibar na kuonyesha kuwa CUF ipo Tanzania nzima. Prof. Lipumba anatambua fika kwamba hatoweza kushinda urais hata kama katiba ingekuwa safi 100% + tume huru ya uchaguzi.

Kwa kuwa hakuna mwanachama wa CUF anayejari (as it makes no impact or difference)...... Lipumba atagombea tena 2015
 
..CUF lazima waelewe kwamba wamekalia "mgodi wa almasi" wa mtaji wa kisiasa.

..kwa muda mrefu sana wamekuwa wana-guarantee ya kushinda majimbo yote ya Pemba.

..Prof.Lipumba na CUF wakigangamala huku Tanganyika na kupata hata viti 30 tu vya ubunge wa Muungano wanaweza kuleta mabadiliko makubwa sana ya kisiasa,kijamii,na kiuchumi.

..kwa upande wangu nadhani CUF Tanganyika wanapaswa kujirekebisha haraka sana kwa manufaa ya wa-Tanganyika na wa-Tanzania kwa ujumla.

..naamini mzigo wa kuikuza CUF haipaswi kuachiwa Wapemba peke yao. wameshajitoa mhanga mpaka kupoteza maisha yao, sasa mnataka wafanye nini zaidi?

Jokakuu:

Mawazo yako ni mazuri sana mkuu. Lakini wakati mwingine sisi waTanganyika ni wasanii sana. Mtu akitaka kugombea ubunge na hasipopata nafasi kupitia CCM basi atakwenda CHADEMA au CUF. Na akiona mambo sio mazuri anarudi CCM.
 
ya hilo la kafu linawezekana,ni swala la kubadilisha kanuni zetu za uchaguzi ambazo zanazuia vyama vya siasa kuungana na kumsimamisha mgombea mmjoja wa urais hiyo ingeleta tija kwa chama kinachokubalika kuwaeza kumsimamisha mgombea uraisi na vyama vingine vikagombea nafasi za uwakilishi
sijui kama wana jf mnalijuwa hilo la vyama vya siasa haviruhusiwi kuungana kwa ajili ya kumuunga mkono mtu mmoja tu kugombea uraisi na hatuwezi kufanikiwa kwa kuwa na wagombea wengi

mapinduziiiii daimaaaaaa
 
..CUF lazima waelewe kwamba wamekalia "mgodi wa almasi" wa mtaji wa kisiasa.

..kwa muda mrefu sana wamekuwa wana-guarantee ya kushinda majimbo yote ya Pemba.

..Prof.Lipumba na CUF wakigangamala huku Tanganyika na kupata hata viti 30 tu vya ubunge wa Muungano wanaweza kuleta mabadiliko makubwa sana ya kisiasa,kijamii,na kiuchumi.

..kwa upande wangu nadhani CUF Tanganyika wanapaswa kujirekebisha haraka sana kwa manufaa ya wa-Tanganyika na wa-Tanzania kwa ujumla.

..naamini mzigo wa kuikuza CUF haipaswi kuachiwa Wapemba peke yao. wameshajitoa mhanga mpaka kupoteza maisha yao, sasa mnataka wafanye nini zaidi?

JokaKuu
Umetowa changamoto poa kabisa.
CUF ingekuwa imeweza kujenga mtandao mpana kila sehemu ya Tanzania kama CCM wasingetumia hoja ya Udini na Ugaidi dhidi ya CUF.
CCM wanatumia hoja ya Udini na uvunjivu wa amani dhidi ya CHADEMA sasa hivi.

Kwa hiyo, kila Chama kinachochipuka kuwa tishio kwa CCM kinaandaliwa mikakati kabambe ya kukivuruga.

Kuna suali zima la nyezo, hapa nyenzo kuu ni fedha na wanachama wa vyama hivyo kujitolea kuhakikisha wanapata wafuasi wengi. Muamko wa wananchi wengi wa kisiasa ni mdogo sana sehemu nyingi za Tanzania. kwa hiyo ni imani yangu kuwa vyama vya upinzani vitapanuwa mitandao yao kwa kadiri watakavyopata nyenzo. Uelewa wa sera za vyama kwa watanzania wengi ni mdogo, wananchi hawajapatiwa elimu ya uraia (civic education) ya kutosha ya kuweza kujuwa haki zao na wajibu wao na hivyo wanapiga kura kimazoea au kwa wasifu wa mgombea siyo kwa uchanganuzi wa sera za vyama . Sio kila mwananchi anataka awe ni mwanachama wa chama cha siasa, lazima kuwe na nafasi pia ya independent voters!

Uchaguzi uliomalizika umeipatia CUF wabunge ingawaje ni wachache huku bara so call that a step forward hata kama ni leap- frog step!

CHADEMA wamepata wabunge wengi kuliko wapinzani wengine. Mafanikio haya yasiwavimbishe kichwa CHADEMA ,lakini still ni kidogo katika ujumla ya idadi wa wabunge bungeni. wajitahadhari,Wajiandae na rungu la CCM kama walivyofanywa NCCR 1995,CUF 2000 na 2005.

Sina nia ya kusema kuwa CUF au CHADEMA au Chama chengine chochote cha upinzani waridhike na mafanikio waliyoyapata ila iwe chachu ya kuona kuwa watanzania wanataka mabadiliko ya kweli.

That brings me to the point which I think is very important, wapinzani waelekeze nguvu zao kuidondosha CCM.Viache siasa za majitaka baina yao. Lakini la muhimu zaidi ni kudai Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi na kupeleka ujumbe kwa vyombo vya umma na dola kuwa viwe neutral, vijielewe kuwa hivyo ni vyombo vya umma si vyombo vya vyama. Hivi sasa vyombo hivi vinafanya kazi kama vile viko chini ya mfumo wa chama kimoja.
 
Hakuna atakaye ijenga mpaka Sultan anayemiliki KAFU atakapo anza kuwa na mapenzi na Tanganyika!! Kwa sasa KAFU inamilikiwa na Wapemba wakiwashirikisha Waunguja wachache pamoja na Wanyamwezi tu. Wanyamwezi wameingizwa KAFU kwa sababu kule unguja kuna wanyamwezi waliopelekwa na Waarabu kama Watumwa, hivyo wanahitaji kura zao kwa Zanzibar na wala si vinginevyo!!! Mwenye Chama anataka kuitawala Zanzibar tu kwa gharama yoyote hata kama ni kuuza uhuru wa chama chake, hana haja na Tanganyika wala na huo Muungano wenu!

Anayebishia hili au akaliita kuwa ni jambo la kishabiki aniambie kwa nini KAFU haijawahi kuongozwa na mtu yeyote wa Tanganyika kwa nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au Katibu Mkuu ambaye si Mnyamwezi!!? Aniambie kwa nini mwenye chama Maalim Seif hajawahi kuja Bara ( ingawa amekuwa akiishi huku zaidi wakati Komandoo Salimin alipokuwa madarakani) kupiga kampeni kwenye uchaguzi mkuu au chaguzi ndogo ndogo? Waliongozwa na Mapalala, waliposhindwana wakamtaka Chifu Fundikira akawatolea nje ndipo wakamuokota na kuanza kumfundisha Siasa profesa wa watu!
"Kweli mzigo mtwishe Mnyamwezi" - Wapemba.
 
..CUF walitoa tathmini yao wakati wa kampeni za uchaguzi kwamba wa-sweep viti vya ubunge kwa ukanda wa pwani na kusini.

..sasa matokeo yamekuja tofauti na walivyobashiri. naamini hapo ni mahali pa kuanzia ktk kukijenga chama chao.

..pia nadhani kuna umuhimu wa Prof.Lipumba na viongozi wengine kuwa active hata baada ya uchaguzi.

..CUF hawajajibu HOTUBA ya JK bungeni, hawatoa critique yao kuhusu BARAZA LA MAWAZIRI, hawajatoa tamko kuhusu DOWANS..sasa CCM wakidai kwamba vyama vya upinzani ni vyama vya msimu hamuoni kuna ukweli fulani hapo?

..KUISHA KWA UCHAGUZI, NI MWANZO WA KAMPENI ZA UCHAGUZI UNAOKUJA. CUF na vyama vingine vya upinzani lazima wazingatie hilo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom