Sasa mnachoogopa ni nini? Kwani Mangu akimkamata (arrest) Seif si atampeleka mahakamani. Na kama hana hatia si mahakama ndiyo itakayoamua kama hicho anachokifanya ni halali kwa mjibu wa sheria zinazotawala nchi yetu na hivyo mahakama itamruhusu aendelee kufanya hicho ambacho Mangu anaona ni kinyume na sheria zetu.
Hii ndiyo kazi ambayo Mangu ameajiriwa kufanya - kuwezesha utekelezaji wa sheria za nchi kwa kuwafikisha wale wote wanaozaniwa wamekiuka sheria. Hivyo hili likifanyika hii chapter ya malalamiko na misononeko kuhusu kilichotokea katika uchaguzi mkuu wa Zanzibar itakuwa imefungwa na wananchi wa Zanziba watatulia.
Acha sheria za nchi zichukuwe mkondo wake. Acha mihemuko. Maneno mengi yote haya uliyoandika ya nini? Unaogopa nini? Kwani Mangu na jeshi la polisi watamudhuru Maalimu?