CUF: Ni hatua nzuri CHADEMA kuwafuta uanachama Wabunge 19 wa Viti Maalum. Tunashukuru kuungwa mkono

Teeheee... Mbona lipumba alikubali kurubuniwa akapindua meza 2015? Tamaa na umaskini wake umeisha nowdays??
 
Andiko la CUF ni makini na la weledi mkubwa.

Cha muhimu, tusimchukie Lipumba kwa sababu ni Lipumba bali kwa yale ayafanyayo. Vivyo hivyo tusimshangilie Mbowe kwa sababu ni Mbowe bali kwa yale ayatendayo.

Katika kuupinga udhalimu, udhulumati na uharamia wa CCM, serikali yake na vyombo vyake kama polisi, nec, n.k; moaka sasa CUF imesimama imara, CHADEMA ilikuwa na mtihani mgumu lakini imeushinda. Tunasuburia ACT.

Madhira na dhuluma huwaunganisha hata maadui. Sasa ni wakati wa kuunganisha nguvu za umma kupitia CHADEMA, ACT, CUF na hata NCCR, kulikomboa Taifa kutoka kwa maharamia wauaji na waporaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nachongoja kwa hamu ni maamuzi ya ACT-Wazalendo chini ya Mwamba wa siasa za Zanzibar,Maalim Seif! Nikisikia Mwamba huyu amekataa uhayawani wa CCM nitajua Upinzani licha ya kunyanyaswa na Utawala wa Kidikteta bado ni imara.
Seif hawezi kuchomoa.
Na yeye njaa na mbinafsi kama Halima.

Halima wa kufanya mambo haya kweli???
Si ndiyo huyu na Esther walikuwa wanawatukana Silinde na Lijualikali?
 
Back
Top Bottom