the ultimatum
JF-Expert Member
- Dec 16, 2012
- 408
- 118
UTANGULIZI:
Tanzania ni nchi ya watanzania wote bila kujali itikadi zao, dini zao, kabila zao, rangi, kipato, hadhi, nyadhifa wala ukanda anapotokea. Hivyo vyote havijalishi ili mradi ni mtanzania.
Hoja yangu itahusu umoja wa vyama tajwa hapo juu (CUF, NCCR na CHADEMA) kwa mustakbari wa Tanzania ya watanzania wote.
Nianze kwa kusema kuwa mimi ni miongoni mwa watanzania hasa waliokuwa na mawazo kama yangu kuwa kwa kasi na hadhi ya CHADEMA ambayo wamejitengenezea katika jamii pamoja na uungwaji mkono wanaozidi kuupata katika jamii basi hawahitaji kuungana na chama chochote cha upinzani katika kuleta mabadiliko nchini. Niliamini kuwa kwa kasi hii inayoonyweshwa na CHADEMA, wanaweza kuwaunganisha watanzania wote chini ya CHADEMA bila kujali itikadi za vyama vyao, dini wala kanda wanazotoka.
Ni ukweli kuwa kuna kanda ambazo vyama vya upinzani vina nguvu zaidi kuliko kanda nyingine. Kwa mfano kanda ya kaskazini CHADEMA wananguvu, kanda ya Magharibi NCCR wananguvu na CUF wakiwa kanda ya kusini. Kwa hiyo ni mitazamo yangu ya mwanzo kuwa kwa kasi ambayo CHADEMA wanaionyesha wanaweza kuunganisha kanda zote hizi chini ya CHADEMA na kuleta mabadiliko nchini, namaanisha CHADEMA kuongoza dola.
Mawazo yangu hayo yalikuwa yanakwenda sambamba na wazo la kuwa vyama vya upinzani kuungana hakutaleta taswira ya kuwakomboa wananchi baada ya vyama hivyo kuungana na kuongoza dola badala yake italeta taswira ya uchu wa kuongoza dola ambao madhara yake ni uchu wa kupeana nyadhifa mbalimbali serikalini hivyo kupelekea mizozo nchini kama ambavyo baadhi ya nchi yametokea.
Lakini leo hii najitokeza na kutamani muungano wa vyama vya upinzani ambao utaleta mabadiliko nchini kwa sababu zangu zifuatazo:-
1. Chama tawala CCM kinanufaika na tofauti wanazozionyesha miongoni mwa vyama vya upinzani hasa vile vyenye nguvu nchini. Katika hili naomba nitoe mfano. Katika kikao cha juzi tarehe 04/09/2013 mbunge wa CUF Habibu Mnyaa alipokea kimemo kutoka kwa mbunge wa CCM kilichosomeka kwa namna ya kubeza "Leo wewe unawasapoti CHADEMA!!" Taarifa hii ya kwenye kikaratasi aliyoisoma Mheshimiwa Mnyaa ilikuwa na lengo la kumkumbusha Mnyaa kuwa CHADEMA sio marafiki zenu wa kweli na hivyo nawashangaa kwanini leo mnawaunga mkono katika hoja yao. Lakini haikuishia hapo, wabunge wengi wa CCM waliokuwa wakichangia hoja bungeni tangu juzi walikuwa wakiwapiga vijembe wabunge wa CUF kuwa urafiki waliouonyesha CHADEMA kwa CUF ni urafiki wa kinafki, na walifanya hivi kwa muda mrefu bila kujikita katika mjadala uliokuwa unaendelea bungeni. Kutokana na hilo mimi nikahoji kwanini wabunge wa CCM wanakazania hili? Nikagundua kuwa kumbe wanafurahia kutofautiana kwa wabunge wa upinzani hasa bungeni ili kuipa nguvu CCM kupitisha au kupinga hoja mbali mbali bungeni. Kwa mfano kwa hoja ya juzi ya iliyohusu mabadiliko ya katiba, CCM walitegemea kutofautiana kwa vyama vya upinzani kungepelekea hoja ile ambayo kimsingi haikuwa na tija kwa mustakbari wa katiba mpya iweze kupitishwa na kujadiliwa bungeni.
2. Ni kutokana na kutofautiana huku CCM wanaitumia fursa hii ili kuongoza dola kila chaguzi kuu zinapotokea. Nitatoa mfano wa kipropaganda ambao huwa unatumiwa na CCM mara kwa mara katika kuvifanya vyama vya upinzani kuwa dhaifu hivyo kushinda kila chaguzi. Mifano ya propaganda ni Udini, ukabila, ukanda na ugaidi. Hapa nitatoa mifano ifuatayo; katika uchaguzi wa miaka ya 2000 na 2005 tulishuhudia namna gani CCM kupitia dola walipokihusisha CUF na ugaidi na hivyo ni chama ambacho hakipaswi kuungwa mkono. Cha kushangaza mpaka leo hii CUF hakikushitakiwa. Tumeshuhudia namna gani CUF kilihusishwa na propaganda ya udini (Uislam). Propaganda hii iliendelezwa kiasi kwamba makundi na asasi mbalimbali za dini ya kiislam zilikiunga mkono chama hiki kwa nguvu ya aina yake, hivyo kuipa CUF taswira nzima kuwa ni chama cha kiislam. Mimi nasema hapa CCM walifanikiwa kuididimiza CUF na baadae CHADEMA kuibuka kama chama kikuu cha upinzani. Propaganda zile zile za udini na ugaidi zikahamia CHADEMA na safari hii CHADEMA kikaitwa ni chama cha kikristo tena Katoliki. Chama hiki kikaongezewa na mengine mengi zaidi, mambo ya vurugu, ukorofi yakaongezwa kwa CHADEMA. Chakushangaza zaidi safari hii CUF kikawa kinapewa sifa nzuri na CCM in opposing CHADEMA's style of politics. Ukiweza kuhoji vizuri utagundua kitu fulani. Utagundua kuwa CCM wananufaika sana na Divide and rule style ambayo ndiyo kete pekee ya kuongoza dola kwa miaka na miaka.
4. Ni ukwali usiopingika kuwa CHADEMA mpaka muda huu wameshatumia rasilimali nyingi sana ikiwemo muda na fedha katika kujiimarisha kuliko chama kingine chochote cha upinzani tangu kuisha kwa uchaguzi mkuu mwaka 2010. Kwahiyo inaweza kujengeka hoja kuwa kwanini leo hii vyama vingine vya upinzani vijitokeze kuunganisha nguvu na kuiondoa CCM madarakani!? Hapa CHADEMA wanaweza kuona kuwa kutokana na kazi waliyofanya ni sehemu ndogo sana imebaki kukamilisha azma ya kuiondosha madarakani CCM. Itapendeza sana kama azma hii itatimia, lakini isipotimia wasiwasi wangu tutarudi kule kule 'vyama vya upinzani ni vyama vya msimu' hili litatukatisha sana tamaa. Itakuwa mbaya zaidi tukija kutambua kuwa kushindwa kwa uchaguzi mkuu kwa CHADEMA kutatokana na kutoungwa mkono na baadhi ya wananchi wanaoshabikia vyama vingine vikuu vya upinzani (CUF na NCCR), mawazo haya yatakuja tukiwa tumechelewa sana na tukiokatishwa tamaa baada ya kazi kubwa walioifanya CHADEMA.
5. Pamoja na mambo mengine mara nyingi utawala unakuwa mgumu sana kwa chama tawala kama chama hicho hakitaungwa mkono na makundi mbalimbali, pamoja na asasi mbali mbali za kiraia hali ambayo inaikumba leo hii CCM. Naomba hapa niongelee CHADEMA kama wataamua kubaki consistence na msimamo wao wakutoshirikiana na vyama vingine vya upinzani na kwa bahati nzuri wakafanikiwa kuongoza dola. Kutakuwa na wasiwasi mkubwa wa kutoungwa mkono na makundi mbalimbali hasa asasi za kidini za kiislamu ambazo ni typically pro islamist against CHADEMA, wao CUF ni chama pekee kitachowatetea waislam. Wasiwasi wangu hapo mbele kama imani ya CHADEMA ya kuwa wataongoza dola itatimia basi watakutana na changamoto kubwa sana ya kukabiliana na kundi hili.
6. Hebu tuangalie umoja ulioonyeshwa na wapinzani kupinga muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba uliotokea juzi bungeni. Ni ukweli kuwa uminywaji wa demokrasia kwa vyama vya upinzani bungeni katika kuchangia muswada huu ulichukua nafasi kubwa sana. Pia ni kweli kwanga kuna vifungu ambavyo vilipingwa kwa nguvu zote kwenye muswada wa awali na wabunge wote bungeni miaka miwili iliyopita vimerudishwa kwenye muswada. Ni kweli kuwa kwa mamlaka makubwa ambayo rais amepewa katika muswada huu katika uteuzi wa bunge maalumu la katiba huenda usipelekee kupatikana kwa katiba ya watanzania wote bali ya kundi fulani la watu (CCM na serikali yake). Ni kutokana na sababu hizo pamoja na nyingine wabunge wa upinzani walionyesha umoja wa kuupinga muswada ule na wote kwa pamoja wakatoka nje ya ukumbi wa bunge (it is just a part of democracy hivyo naunga mkono). Kwasababu katiba ni kitu muhimu zaidi katika utawala wowote wa kidemocrasia na kwa sababu katiba tunayoitengeneza leo tunategemea itadumu kwa miaka hamsini mpaka mia moja hivyo ni heli katiba hii ikawa ina sura ya watanzania wote wa sasa na wa vizazi vinavyokuja. Muungano wa vyama vya upinzani katika hili umeonyesha sense of patriotism, spirit of national hood and love for the nation.
MWISHO:
Kwangu mimi kuna umuhimu mkubwa sana kwa vyama vya upinzani tajwa kukaa meza moja na kuamua kuunganisha nguvu ili kupambana na CCM kuelekea chaguzi zinazokuja kwa ajili ya Tanzania na watanzania wote. Kama hoja itakuwa ni mgawanyo wa madaraka kwa viongozi wa vyama hivyo vitapoungana na kuchukua dola vitapelekea mitafaruku kwenye serikali na hivyo kusahau kuwatumikia watanzania ndiyo hoja kuu ya kukwamisha kuungana huko, najuliza swali lifualtalo:-
JE, kuacha kugawanywa hivi na CCM kwa vyama vya upinzani ambayo ndiyo kete imara ya kuendeleza utawala wa CCM kwa miaka na miaka, na vyama vya upinzani kuungana na kuongeza nguvu ya mapambano dhidi ya CCM kipi bora? Na je, kipi ni bora kati ya kuendelea kuwepo madarakani kwa CCM na kuruhusu chama imara cha umoja wa vyama vya upinzani kuingia madarakani na kutoiogopa changamoto ya mgawanyo wa madaraka mbeleni?