CUF mambo magumu Bukoba


A

Asha Abdala

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2007
Messages
1,134
Likes
5
Points
0
A

Asha Abdala

JF-Expert Member
Joined Mar 21, 2007
1,134 5 0
CUF mambo magumu Bukoba

na Ashura Jumapili, Bukoba


CHAMA cha Wananchi (CUF) katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kimeendelea kupoteza umarufu wake siku hadi siku kufuatia kuondokewa na mmoja wa viongozi wake waandamizi, Wilfred Lwakatare aliyehamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Hali hiyo imejidhihirisha katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Mashujaa mjini hapa ambapo watu waliojitokeza ni wafuasi wa CHADEMA na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akihutubia katika mkutano huo, diwani wa Viti Maalum wa chama hicho Manispaa ya Bukoba, Zainabu Marijan alisema amepokea ujumbe wa simu yake ya mkononi uliokuwa ukisema CUF imekufa tofauti na ilivyozoeleka miaka ya nyuma.
Mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho ngazi ya wilaya, ulilenga zaidi kufanya kampeni huku viongozi wakitumia muda mwingi kumshambulia Lwakare, kitendo ambacho baadhi ya wananchi walisikika wakisema kuwa kiongozi huyo alikuwa nguzo kuu ya kisiasa.
Naye Katibu wa chama hicho, Swahibu Maghayane aliwaeleza wananchi kuwa chama chao kimejipanga kuhakikisha kinawasimamisha wagombea wenye sifa na vigezo vya upinzani ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Maghayane alisema kuwa tayari chama hicho kinao wagombea watano ambao watagombea katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
 

Forum statistics

Threads 1,251,749
Members 481,857
Posts 29,783,591