CUF: Maandamano yetu yako pale pale

CUF: Maandamano yetu yako pale pale

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
[h=2][/h]





Mtatiro-Cuf.jpg



Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro



Chama Cha Wananchi (CUF), kimesema maandamano ambayo awali kilipanga kufanya Juni 29, mwaka huu kuelekea Ikulu lakini yakaahirishwa kutokana na ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama yako pale pale.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, alisema kwa sasa viongozi wengi wa chama wapo mikoani, lakini watakaporudi jijini Dar es Salaam chama kitafanya mkutano utakaopanga lini maandamano hayo yafanyike.

“Hatujakutana bado. Wajumbe wengi tupo mikoani. Sasa tutakaporejea Dar es Salaam tutapanga siku ya kukutana. Halafu tutapanga siku ya maandamano na tutawajulisha,” alisema Mtatiro.

Kwa mujibu wa CUF, maandamano hayo yana lengo la kumfikishia ujumbe Rais Jakaya Kikwete, kwa kile wanachodai kuwa vitendo vya ukatili, wizi, ubakaji na mauaji vinavyofanywa na polisi mkoani Mtwara na kutaka uchunguzi kuhusu matukio ya Arusha.

Hata hivyo, kuahirishwa kwa maandamano hayo kulikuja baada ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, kuyapiga marufuku na kuonya kwamba polisi wangepambana na yeyote ambaye angekaidi amri hiyo.




CHANZO: NIPASHE
 
si wanadai kuwa maandamano yanahatarisha amani na kufukuza watalii?Kwa mujibu ya taaluma za mchumi number moja.Mchumi aisyejua kuna utalii wa kutembea mujini na vijijini na milimani..Na kuna watalii wengi tu activists wanapenda tembelea na kushiriki maandamano mbalimbalia duniani.Hata waliberali wapo tayari tembea dunia nzima kudai ahaki ya waliberali wengine...so tutawaona wakija waunga mkono CUF na prof wao aliyeamua kunyonyoa nywele masikioni.
 
Ni haki yao CUF kwenda IKULU napenda kuwashauri POLISI waache kuingilia NDOA za watu sasa mtu anataka kwenda kwa MMEWE kwa nini kumwekea vikwazo????.
 
Tanzania bila maandamano inawezekana ! Kwani hata wakiandamana Hakuna atakayewasikiliza ! Wangeachiwa waandamane ujumbe wao utawekwa kwenye makabati tu ! Kuondoa kero kwa njia ya maandamano ni
Njia bora lakini ingekuwa bora zaidi kabla janga halijatokea yaani mnaandamana kuzuia janga si kuandamana janga limeshatokea ! Hapo itakuwa ngumu kueleweka Kama ilivyo vigumu serikari kuhamia Dodoma.
 
Tunasubiri kuona hilo linatokea,Tunalisubiri kwa hamu kubwa SANA...
 
Ni haki yao CUF kwenda IKULU napenda kuwashauri POLISI waache kuingilia NDOA za watu sasa mtu anataka kwenda kwa MMEWE kwa nini kumwekea vikwazo????.

Mkuu umenvunja mbavu..!daaah haya bhana yetu macho!
 
mtaandamana kwenda kwenye bomba lagesi au mtaenda baharini inakopatikana gesi.
 
kwani mandamano ndiyo sera gani hizi mimi zinanishangaza kweli kumbe taifa linaweza kuongozwa kwa kufanya mandamano.
 
waende wakapewe chai make ndo zao njaa zikiwazidi wanatafuta jinsi gani watakunywa chai na rais huku wanaulizwa habari za bugurini
 
Mtatiro-Cuf.jpg



Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro
HE

CUF BURUDIKENI NA WIMBO WA MAALIM GURUMO


Tuliwaambia na Mapema ,Kuwa Mchumba wako ni Mlevi ,
Hukutaka kutusikiaaaa[hukutaka kutusikia eeeeee]
Leo Umeyaona Mwenyeweeeee..mwanetu weeeeee
Nenda kwa wazazi wake ,Muweo Ukawaeleze ........

Mwanetu kaza moyo Uishi na Mumeo ...[ Mumeo huyooooooo ...]
Ni weewe mwenyewe uliyempendaaaa [usimkataeee]
Mwanetu Kaza MOYO ishi na mumeo [mumeo huyo]
Ni wewe mwenyewe uliyempendaaaa.....


Tuliwaambia na Mapema ,Kuwa Mchumba wako ni Mlevi ,
Hukutaka kutusikiaaaa[hukutaka kutusikia eeeeee]
Leo Umeyaona Mwenyeweeeee..mwanetu weeeeee
Nenda kwa wazazi wake ,Muweo Ukawaeleze ........



KUUNGANA AU KUINGIA UBIA NA CCM IMEPOTEZA SANA NGUVU ILIYOKUWA NAYO NA KUWACHIA VYAMA VINGINE KAMA JAHAZI,[UAMSHO]., NA CHADEMA ...KUCHUKUA NAFASI ....WATU WENGI NDANI YA CUF NA NJE YAKE WALIKUWA WAKITILIA SHAKA HUU USHIRIKIANO......NA CUF WAMEKUJA KUSHTUKA TAYARI WAKO NDANI YA NDOA NA WAMESHAJIFUNGUA MTOTO....INA BIDI WAKAZE MOYO TU WAISHI NA MUME
 
[h=2][/h]






Mtatiro-Cuf.jpg



Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro



Chama Cha Wananchi (CUF), kimesema maandamano ambayo awali kilipanga
kufanya Juni 29, mwaka huu kuelekea Ikulu lakini yakaahirishwa kutokana
na ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama yako pale pale.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, alisema kwa sasa
viongozi wengi wa chama wapo mikoani, lakini watakaporudi jijini Dar
es Salaam chama kitafanya mkutano utakaopanga lini maandamano hayo
yafanyike.

“Hatujakutana bado. Wajumbe wengi tupo mikoani. Sasa tutakaporejea Dar
es Salaam tutapanga siku ya kukutana. Halafu tutapanga siku ya
maandamano na tutawajulisha,” alisema Mtatiro.

Kwa mujibu wa CUF, maandamano hayo yana lengo la kumfikishia ujumbe Rais
Jakaya Kikwete, kwa kile wanachodai kuwa vitendo vya ukatili, wizi,
ubakaji na mauaji vinavyofanywa na polisi mkoani Mtwara na kutaka
uchunguzi kuhusu matukio ya Arusha.

Hata hivyo, kuahirishwa kwa maandamano hayo kulikuja baada ya Kamanda wa
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, kuyapiga marufuku
na kuonya kwamba polisi wangepambana na yeyote ambaye angekaidi amri
hiyo.




CHANZO: NIPASHE

wapigwe hao cuf
 
Julias, ningependa kushiriki pia, ila tatizo la CUF maandamano yenu lazima yawe siku ya Ijumaa na yaanzie misikitini baada ya swala ya ijumaa. hapo ndipo mnaponichanganya kabisa.
 
Julias, ningependa kushiriki pia, ila tatizo la CUF maandamano yenu lazima yawe siku ya Ijumaa na yaanzie misikitini baada ya swala ya ijumaa. hapo ndipo mnaponichanganya kabisa.

Duhh!!!
 
Waliberali nao wana mambo lakini halahala yasiwe ijumaa
 
Hii ni kuwarahisishia CCM kuwa CUF ni chama cha UDINI,Falsafa hii ilikuwa wimbo uliokolea kwa CCM lakini najua CCM na CUF wanajuana kwa vilemba hapa wanatuzuga tu lakini ikifika USIKU lao moja
Julias, ningependa kushiriki pia, ila tatizo la CUF maandamano yenu lazima yawe siku ya Ijumaa na yaanzie misikitini baada ya swala ya ijumaa. hapo ndipo mnaponichanganya kabisa.
 
Back
Top Bottom