Uchaguzi 2020 CUF kuwasaidia wananchi kuondokana na maafa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba, amesema atakapopata ridhaa ya kuwaongoza Watanzania, serikali yake itashirikiana na Jumuiya ya Umoja wa Kimataifa ili kuweza kuwekeza katika mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Profesa Lipumba ameyasema hayo wakati akihutubia wananchi wa Kijiji cha Kipindimbi, Kata ya Njinjo, jimbo la Kilwa Kaskazini ambapo amesema serikali ya CUF kwa kushirikiana na wananchi itahakikisha wananchi wanaondokana na maafa ya mafuriko.

''Pana tatizo ambalo linaweza kuwa la muda mrefu tatizo la mabadiliko ya tabia nchi ni tatizo ambalo tayari limeshatufikia, nchi zilizoendelea zimekuwa zikizalisha hii hewa ukaa ambayo imeongeza joto Duniani tunahitaji tuwe na serikali makini yenye huruma itakayoshirikiana na wananchi na Jumuiya ya Kimataifa ili kuweza kukabiliana na tatizo hilo la mabadiliko ya tabia nchi", amesema Profesa Lipumba.

Pamoja na hayo Profesa Lipumba amesema kuwa atakapoingia Ikulu ataanza kujenga barabara ya kutoka Nangurukuru - Liwale kwa kiwango cha lami ili kuwafungulia uchumi wakazi wa maeneo hayo na maeneo mengine.
 
Huoni hata aibu kuleta Post kwa vitu vilivyokufa.
Mwambie Lipumba akale alikopeleka mboga?
 

Attachments

  • 2368793_2024173_IMG_20190329_072747_1.jpeg
    2368793_2024173_IMG_20190329_072747_1.jpeg
    16.4 KB · Views: 1
Anayetakiwa aone aibu ni yule Msaliti wa Nchi kutoka ubeligiji, ambaye tayari amekata tikiti ya kurudi kwao ubeligiji baada ya kuona Watanzania wamamkataa
Huoni hata aibu kuleta Post kwa vitu vilivyokufa.
Mwambie Lipumba akale alikopeleka mboga?
 
Back
Top Bottom