CUF imeimarika Zanzibar...

Wateule

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
390
368
Maombi yaendelee kufanyika na wa ZNZ (sio wapemba peke yao, kwani Wazanzibari wengi wakekerwa na dhulma ya October, 2015) ili mtoa haki wa kweli (MUNGU) afanye yake kabla ya 2020. Lakini, sikubaliana na wewe kwamba CUF walishinda kwa "mbinu" na hivyo walikuwa hawana sababu ya kuogopa kushiriki ule uchaguzi wa March, 2016. Katika hii hoja, nitarejea kwenye swali la msingi ambalo hata Maalim Seif mwenye amekuwa analiuliza mara kwa mara na mara zote sioni wala sisikii akipewa jibu la maana....hivi unafikiri na kuamini kwamba CCM walifuta uchaguzi wa October 25, 2015, ili wafanye mpya na kushindwa tena???

Wote tunajua kwamba majeshi, mabomu, vifaru, na mizinga vilikuwa vinatiririka ZNZ kuelekea huo unaoitwa "uchaguzi wa marudio" wa March, 2016 ili kuhakikisha ZNZ inabaki kuwa mali ya CCM na vibaraka wake kule ZNZ. Katika mazingira kama yale, ingekuwa ni ujinga na usaliti kwa Maalim Seif kama anavyopenda kusema "kuweka kichwa na kuchinjwa" wakati anajua atachinjwa tu. Katika uchaguzi ule wa zao la dhulma, CCM walishajiandaa "kushinda" kwa gharama yeyote, na pia walikuwa tayari kumpa Seif nafasi wanayotaka na kumchagulia wao, ambayo ni umakamu wa kwanza wa rais. Narudia tena, kitendo cha CUF kususia uchaguzi ule wa March, 2016 ni cha kijasiri na kizalendo kwani kwa kufanya hivyo wameonyesha kwamba hawakutaka kuweka maslahi ya vyeo vya kisiasa mbele na badala yake wamezingatia principle (ya kutohalalisha dhulma) na maslahi mapana ya ZNZ.

Wewe (Paskali) na wengine mnaona CUF wamekosea kwasababu mnaangalia kinachoendelea sasa kule ZNZ kwa CCM kufanikiwa kulazimisha Shein kuwa madarakani. Lakini, kwasisi tunaoona mbali, CUF imeimarika zaidi ZNZ kwa uwamuzi ule. Na kama Mungu hajafanya yake kabla ya 2020, basi CCM watakuja kushangaa nguvu waliyoiongezea CUF kwa kitendo chao cha kuidhulumu ushindi wake halali. Waliodhulumiwa ambao kimsingi ni wananchi wa ZNZ wapo, na wao sio wajinga wa kutokuelewa maamuzi ya CUF. Kunapo uhai, tukutane tena hapa 2020 ili kujadili tena uhai na nguvu ya CUF kule ZNZ ambayo itakuja kuwashangaza wengi mnaoona na kufikiri masafa mafupi (short sighted thinking). Ukweli na haki siku zote hushinda hata kama ushindi huo utaonekana umechelewa.
Asanteni.

Muhimu:
Nimeshawishika kuweka bandiko hili barazani kutokana na bandiko la Paskali hapa: Ukweli Mchungu Zanzibar: Hakuna Mgogoro Wowote wa Kisiasa, Shein ni Rais Halali, Uchaguzi ni 2020!
 
Ile dhuluma waliyofanyiwa CUF kwenye Uchaguzi wa Oktoba 2015 haitafutika kamwe..
Jecha analo hili mpaka Israeli atakapomchukua.
 
Ni kweli cuf imeimarika sana Zanzibar. Lkn ccm ndiyo hivyo hawataki kuachia madaraka. Hata hiyo 2020 ccm inaweza ikapata kura kiduchu sana lkn hawataachia madaraka.

Swali kwako ndg mleta mada, hamuoni kwamba muda umefika wa cuf kubadili mbinu ya kuitoa ccm madarakani baada ya hii ya sanduku la kura kushindikana ? .
 
Watanganyika na wazanzibari inabidi tukae chini tutafute njia mbadala ya kuitoa ccm madarakani maana njia ya kura wanapora ushindi
 
Ni kweli cuf imeimarika sana Zanzibar. Lkn ccm ndiyo hivyo hawataki kuachia madaraka. Hata hiyo 2020 ccm inaweza ikapata kura kiduchu sana lkn hawataachia madaraka.

Swali kwako ndg mleta mada, hamuoni kwamba muda umefika wa cuf kubadili mbinu ya kuitoa ccm madarakani baada ya hii ya sanduku la kura kushindikana ? .

Ya sanduku la kura bado haijashindikana. Ili kuepuka njia mbadala ya kuingia msituni na kupambana kwa mtutu, ambayo itatuletea hasara kubwa zaidi na ya muda mrefu. Maoni yangu ni kwamba CUF ishiriki uchaguzi wa 2020. Lakini, ishiriki uchaguzi huo ikiwa imejiandaa zaidi kuyalinda na kuyatetea matokeo ya ushindi wao.

Ninaposema kujiandaa zaidi namaanisha kushawishi au kuiruhusu (kama vijana wa CUF huwa wanadai wanasubiri ruksa) jamii ya Wazanzibari kuingia mtaani na kupinga kwa sauti kubwa. Ninaposema kuingia mtaani, najua hofu yetu kubwa na ukweli ni kwamba CCM wataleta majeshi yao kudhibiti na hata kuua.

Lakini, hatua hiyo itawaweka uchi kabisa mbele za jumuiya ya kimataifa na hatimaye suala la ZNZ kupewa uzito inaostahili kimataifana, na mwishowe haki kupatikana. Kwa hapa tulipofikia kwa hila na vibweka vya CCM visivyoisha, huu ni ukweli ambao upo mioyoni mwa watu wengi lakini wanaogopa/ tunaogopa kuusema kwa hofu ya kuitwa majina ya kila aina, likiwepo lile maarufu la "mchochezi."

Historia ya dunia inaonesha, jumuiya ya kimataifa haisaidii watu ambao hawapo tayari kujitokeza kwanza na kujisaidia wenyewe labda tu maslahi ya nchi kubwa (Marekani, Wingereza, ufaransa, nk) katika jumuiya hii yatakuwa yameguswa moja kwa moja (mfano wa karibu zaidi, ni nchi ya Iraq ya Saddam).

Kwa bahati mbaya katika ukanda wetu wa Afrika Mashariki (masafa mafupi ya Jumuiya ya kimataifa) bado hatuna ECOWAS kama ile ya Afrika Magharibi iliyofanya Yahya Jameh kufungasha virago vyake. Ukanda wa Afrika Mashariki umesheheni walafi wa madaraka kama CCM (Kagame, Museveni, Nkurunziza, nk). Hivyo basi, masafa marefu ya jumuiya ya kimataifa inabidi yategemewe zaidi.

Kila uchaguzi kule ZNZ unapofanyika na matokeo kuchakachuliwa, CCM wamekuwa wanatisha watu kwa vifaru na mizinga ili wasidai haki yao na hufikia hata kuua watu kadhaa na hatimaye watu hurudi nyumbani na kutulia. Safari ijayo, ni kwenda nao sambamba mpaka nusra ya Mwenyezimungu kupitia masafa marefu ya jumuiya ya kimataifa itakapo wafikia Wazanzibari.

Kwa kumalizia, Zanzibar itakombolewa na Wazanzibari wenyewe kupitia sanduku la kura, lakini kwa masikitiko makubwa nasema kwamba kuna gharama kubwa italipwa ili kulinda heshma na haki ya kura zao.
 
CUF iko upande wa haki, ila kwa CCM, CUF kuwa upande wa haki means nothing.
So,CUF wajue kuwa kwenye siasa haitoshi tu kuwa upande wa haki. HAKI HAIOMBWI!
 
Back
Top Bottom