Cuf ikishinda zanzibar - nchi itatawalika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Cuf ikishinda zanzibar - nchi itatawalika?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mukuru, Aug 10, 2009.

 1. Mukuru

  Mukuru Member

  #1
  Aug 10, 2009
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa najiuliza hivi CCM na watu wake wako tayari kukubali sehemu moja ya muungano kutawaliwa na serikali ya upinzani? Ikitokea hali kama hiyo ndo itakuwa mwisho wa muungano? Nadhani CCM wako tayari kuzuia hali hiyo isitokee kwa gharama yoyote ile. Wana JF hii imekaaje?
   
 2. M

  Mundu JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mkuu Mukuru, hicho ni kizungu mkuti. CCM hawako tayari na hawatakuwa tayari kuona CUF inatawala Zanzibar. Na ndio maana Zanzibar hadi leo inakaliwa kimabavu na Serikali ya CCM. CUF walishinda chaguzi zote tatu kuu kisiwani humo, lakini kiko wapi? Hadi leo wanapigwa domokrasia tu.

  CCM sijui wanahofu kitu gani kwa CUF kutawala Zanzaibar, mbona kuna Halmashauri tatu kwa fasta fasta bara zinatawaliwa na CHADEMA na maisha yananyoka tu? Tarime, Karatu na Kigoma mjini mbona watoto wanaenda shule kama kawa? Hata Zanziabar ikitawala CUF au chama kingine, maisha yatakuwa juu ya mstari tu!!
   
 3. K

  Kinyikani Member

  #3
  Aug 11, 2009
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 65
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kutawala Cuf Zanzibar ndio mwisho wa CCM ndio maana haiko tayari kuona Cuf ina chukuwa nchi watafanya kila njia lakini cuf wasichukue nchi. hebu niambie vipi itakuwa rais Tanganyika CCM na Zanzibar ni CUF.
   
 4. F

  Falconer JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2009
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  nimesikitishwa sana na kauli yako. Hivi maana ya demokrasia unaijua?. Au ndio mmoja katika wale walionyweshwa maji kijani kibichi. Yaani hamuamini kama kuna watu wanaweza kutawala nchi isipokuwa CCM?. Ole wao CCM wameimaliza nchi kwa wizi wa mchana. CUF itashnda na muungano hautoivunjika sababu CUF ni chama cha bara na visiwani. Ulaji ndio unawababaisha wana CCM.
   
 5. M

  Mwanaluguma Member

  #5
  Aug 11, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Actually even the constitution itself isn't clear on the issue. We will experience a lot of problems if the opposition wins in Zanzibar.
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  CUF kamwe haiwezi kushinda huko visiwani...
   
 7. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Ukoloni ungelikuwapo nasi mpaka leo basi!!!
  "Kila zama na mambo yake" by Mzee Ruksa(Mwinyi)
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Aug 11, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hata kama hamtaki kukubali, 'zama' zenu bado hazijafika, na itachukua muda mrefu sana kuwadia iwapo mtaendelea na mikakati mliyonayo hivi sasa
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mfanyabiashara Maarufu, Mohamed Raza akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.
  Mfanyabiashara maarufu, ambaye pia, ni mshauri wa zamani wa masuala ya michezo wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour, Mohamed Raza, amepinga wazo la kuanzishwa serikali moja katika mfumo wa Muungano wa Tanzania akisema jambo hilo ni uhaini kwa vile linalenga kufuta utaifa wa Wazanzibari.

  Raza, alitoa kauli hiyo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana na kusisitiza kwamba wazo hilo pia ni utovu wa maadili, ukiukwaji wa sera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Katiba ya nchi na pia ni hatari kwa mustakabali wa CCM, kwani inaweza kupoteza kura zote, ikiwamo kura yake Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu mwakani.
  Alisema viongozi wa serikali ya Muungano wamekuwa wakidai kuwa serikali ya Tanganyika imefutwa, lakini ukweli ni kwamba, bado ipo na kwamba, imejificha ndani ya Tanzania.
  Alisema sera ya CCM inatambua serikali mbili katika mfumo wa Muungano, na si moja wala tatu na kuongeza kuwa suala la kiongozi wa serikali ndani ya Muungano kutaka kuanzishwa serikali moja, ni ishara kwamba, wamepotoka kimaadili.
  "Ndio maana G55 (kundi la wabunge 55) ilipokuja na hoja ya kuanzishwa serikali tatu, Mwalimu Nyerere alisimama na kuipinga kwa nguvu zake zote kwa vile sera ya CCM na Katiba ya nchi inazungumzia serikali mbili. Kuzungumza serikali moja ni uhalifu sababu unataka kumfutia mtu utaifa wake. Ninahofu sana ushindi kwa CCM.
  Kama chama hakijawekwa sawa halafu tunakwenda kwenye uchaguzi, ni hatari. Wallahi leo CCM iseme kuna serikali moja, tuone kama watapata hata kura moja Zanzibar, yangu ikiwamo," alisema.
  Hata hivyo, alisema kama kumeonekana hapana budi kuanzishwa serikali moja katika mfumo wa Muungano, ni vema wananchi wakatangaziwa mgogoro wa Katiba na kwa sababu hiyo, hata kamati iliyoundwa kushughulikia kero za Muungano, Wazanzibari hawawezi kuwa na imani nayo.
  Hata hivyo, alisema ili kuimarisha Muungano, Watanganyika waiachie Zanzibar ijitegemee kiuchumi ambapo alisema: "Hata Dubai kuna Muungano wa Umoja wa Nchi za Kiarabu (UAE), unaoziunganisha nchi kama vile Sharja na nyinginezo, lakini kila moja inajitegemea."
  Alisema wanachokitaka Wazanzibari ni "kuheshimiana, kuvumiliana na kujadiliana" inapokuja hoja kuhusu Muungano na kusisitiza kuwa hakuna anayetaka kuvunja Muungano.
  Alisema jambo lingine analopinga, ni kundi la watu kudhani kwamba lenyewe tu ndilo linaweza kuongoza nchi au wanafikiria wao ni bora wa kuongoza nchi.
  Alimtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kueleza walikofikia wanasheria wa pande mbili za Muungano katika kushughulikia utata wa hoja ya kama Zanzibar ni nchi au la. "Mmetamka hadharani, iko wapi ripoti?," alihoji Raza.
  Juzi akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Culture, Vuga Mji Mkongwe, Zanzibar, Maalim Seif alisema kauli ya Pinda aliyoitoa bungeni mjini Dodoma hivi karibuni kwamba anatamani kuwe na serikali moja sio ngeni na kwamba mpango huo upo siku nyingi, kama ambavyo Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi alivyowahi kusema siku za nyuma
   
 10. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Hakika ni vigumu sana CUF kupewa nchi hata kama watashinda uchaguzi wa Zanzibar. Hiyo inatokana na mfumo wa katiba ya Tanzania ikiwa pamoja na ile ya Zanzibar. kwani zote zinakataa kabisa mfumo wa vyama vingi zimeundwa na zinaendelea kuukumbatia mfumo wa chama kimoja kitawale.

  hata kula zenu mnazopiga ni kiini macho
   
 11. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135


  Kibunango na Pinda ni watu wawili ambao huteremshiwa wakhai kutoka mbinguni kama ilivyokuwa wakati wa Mitume ,kibunango anasema kamwe Cuf haiwezi kushinda, CCm mmoja kwa jina la Borafia alifika kutakabari na kusema kuwa Mmungu hana uwezo wa kujenga nchi siku mia seuze Cuf ,na pinda alisema kuwa zanzibar ikijitowa katika Mungano basi itapata tabu kimaisha, kauli ya pinda ilinishanga kutokana na sisi waisilamu Mmungu anasema hakumuweka malaika wa kutowa riski, kazi hiyo anaisimamia mwenywe lakini pinda inaonekana kwa uwaziri wake ana aksesi ya mamuzi yanayotokana na Mmungu kama vile alivyonayo Kibunango ,ijapokuwa Mmungu anasema hakuna binadamu yeyote anaejuwa nini kitamtokea ndani ya second moja ijayo, lakini wezetu mungu amewapa uwezo wakuelewa hali ijayo,pia naimani ipo siku penye uhai watatueleza ni siku gani yatawadia mauti yao .
   
 12. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  CUF haitoweza kushinda Zenj na kuunda serikali, hili lipo wazi na litendelea kuwa hivyo hadi pale chama hicho kitakapo kuwa cha kitaifa zaidi ya kipemba
   
 13. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hata Waarabu waliyasema hayo kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar? Ni kipi cha kuzuia kutokea hilo iwapo wananchi wameshafikishwa pahala wasipojuwa nini kesho ya visiwa hivi. Amini Mungu ipo siku wananchi watasema kuwa safari hii tunataka anaeshinda kweli atangazwe
   
 14. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Unakusudia kushinda au kupewa madaraka?
  Nafikiri huko sahihi kwa yote. Kushinda CUF wana uwezo wa kushinda kwani harakati za udanganyifu wa CCM zinaonyesha namna kura halali za CCM zinavyokuwa chache kulinganisha na zile zinazobanwabanwa za CUF
  Kuhusu kupewa madaraka naamini kuwa kweli ina nguvu zaidi kuliko wizi.
   
Loading...