Ni matumaini yangu kuwa nguvu ya cuf bara na visiwani imekwisha na ninamuomba mmiliki pekee wa cuf aliyeko visiwani ajue hilo
Mkuu nakuunga mkono 100%. CUF imekwisha na haina mwelekeo. Iko kwenye dilema, hawajui waelekee upande gani - kilichobaki ni kudandia hoja ovyo ovyo ili waonekane nao bado wapo lakini kimsingi imebaki muflisi. Kuna mambo kadhaa yaliyochangia kukimaliza hiki chama, naomba niorodheshe machache sana:-
(i) UBAGUZI: Hiki chama ni cha kibaguzi uzanzibari na hasa upemba ukiwekwa daraja la juu zaidi ndani ya CUF. Viongozi na wanachama kutoka bara ndani ya CUF wapo wapo tu just kwa matakwa ya kisheria kwamba lazima chama kiwe na idadi fulani ya wanachama Bara na Visiwani.
(ii) GHASIA, FUJO, NA CHUKI: Kwa asili CUF ni chama cha ghasia, fujo, na chuki dhidi ya YEYOTE asiyekuwa "mwenzao"; hili linashabihiana na (i) hapo juu. Wakati wenzao wanahubiri AMANI wao na hasa enzi hizo kikiwa na nguvu kilichochea FUJO. Kauli kama NGANGARI (na hatimaye NGUNGURI za Polisi) au matumizi ya majina mbali mbali yenye kuleta hofu katika jamii haikuwa muafaka katika kujenga image ya chama mbele ya jamii bali kubomoa. Mfano angalia majina ya matawi ya CUF - CHECHNYA, TORA BORA, HAMAS, OSAMA, AL QAEDA, n.k. lengo lake ni nini? Au walitaka kuonesha nini kwa umma? Hivi wangetumia majina ya kawaida ya mahali husika isingefaa mpaka watumie majina ya maeneo ambayo dunia nzima inajua nini kinaendelea huko? Stupid!
(iii) USULTAN: Hili liko wazi, CUF ni ya Maalim Seif na Wapemba wenzie. Akina Lipumba ni kanyaboya tu pale. Tangu mfumo wa vyama vingi wao (Maalim Seif na Lipumba) wamekwa viongozi na wagombea wa kudumu wa urais ndani ya CUF na hakuna dalili kwamba watang'oka hivi karibuni. Hii sio nzuri sana kwa chama na inafifisha demokrasia - matokeo yake ADC.
(iv) MUAFAKA: Muafaka uligeuzwa siri iliyokuja kuzaa "ndoa" kati ya CUF na CCM. Na kwa kuwa sharti siri za ndoa zilindwe na wanandoa, CUF imejikuta katika wakati mgumu katika kuamua isimamie nini/wapi linapokuja suala la kitaifa ambalo linaonekana kumuathiri mwanandoa mwenzake - CCM. Hivyo, badala ya kuwa na maamuzi huru kimekuwa chama cha kufuata mkumbo zaidi - wakati mwingine CCM na wakati mwingine upinzani hasa pale kinapobaidi "wananchi watanionaje" kama hili la Bungeni juzi.
Kwa uchache ni hayo mengine nimeyahifadhi; nikiyafumua hapa milima itatikisika.
Gamba hilo limetumwa