Cross roads

Status
Not open for further replies.

Billions

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
2,851
2,000
Nawasalim nyote...kwa waislam wenzangu Asalam Aleykum, na pia kwa wakristo wenzangu mana hata nyie ni wenzangu, Tumsifu Yesu Kristu, Bwana Yesu apewe sifa. Na wengine jaman habar zenu.

Baada ya salamu naomba nianze hivi...

Mwanaume huyu alipendana na msichana yule na mwanzo wa mahusiano walipeana ahadi kedekede za maisha yao ya badae na zaidi sababu msichana yule alikua virgin hivyo bas mwanaume huyu alizidisha upendo na msichana yule alimuahidi kujitunza na pia alisisitiza kua watafanya lile tendo takatifu la ndoa hadi watakapofunga ndoa. Maisha yakaendelea.

Msichana yule alikua hana kazi kwaio mwanaume huyu alikua anambeba kama mtu wake lakini sio kama mzazi wake(mambo ya ada na nini hayahusiki, ni mambo madogo ambayo alikua anayasettle mwanaume huyu).

Maisha yakaenda mwanaume huyu kibarua kikaota nyasi, huku msichana yule bahat akapata kazi inayomlipa vizuri tu(maana hutaweza kufa njaa ama kuishi kwenye mapango au kuvaa nguo zilizochakaa). Viashiria vya kushangaza na mabadiliko yalianza kuonekana hapa. Kumbe kuna "kiumbe" alikuwa tayari yuko katika "radar". Anyway tuendelee.

Mwanaume huyu na msichana yule ikawa ugomv here and there, na mwanaume huyu aliona dhahiri shahiri kwamba sababu ilikua inatafutwa ili mwanaume huyu atamke "its over" lakin mwanaume huyu alikua mara nyingi anajitahidi kuweka mambo katika msawazo lakin wakati mwingine ilikua ikifanikiwa na wakati mwingine haikufanikiwa.

Hali hii ikawa inamuumiza sana mwanaume huyu, japo alijipa faraja kua hakuna marefu yasiyokua na ncha kwamba ipo siku ukwel utajulikana lakin alishaona "dalili" na "viashiria" vya kusalitiwa.

Hatimaye mwisho wa siku uzalendo ukamshinda mwanaume huyu akaamua aanze kuutafuta ukweli mana hali ilizidi kua tete, pia kumbukeni bado mwanaume huyu hana kibarua chochote ndio alikua anaanza kujinyanyua mana kazi iliyoota nyas ndo kwanza alikua anaanza, ilikua kwa miez michache tu ndipo akaondolewa(hakuiba jaman mana msifikiri fisadi, ni mambo ya redundancy). Kwaio msichana yule ndo angepswa awe mfarji wake.. lakini...My God .

Kazi ya kuutafuta ukweli ikaanza rasmi, na haikuchukua muda sana akawa amepata majibu, japo niseme njia aliyotumia mwanaume huyu haimpendezi Mungu lakini aliona hana jinsi mana HE WAS SUFFERING INSIDE.
Kifupi ana MTU(naomba tumpe tu jina hilo MTU) mwingine, kwaio msichana yule alikua anamsaliti mwanaume huyu, akaonyeshwa yote na akaambiwa yote walivokua wanafanya mambo yao machafu. Ushahidi hajaupata bado wa kushika mkononi ila wa macho "ameonyeshwa" na "bwana mmoja" ambae aliona amsaidie ili mwanaume huyu asiendelee kuteseka bure.

Inavosemekana msichana anampenda mwanaume huyu KIMAPENZI ILA AMESHINDWA KUVUMILIA KWA KUWA MPENZI WAKE HANA KITU. Na huyo MTU mwingine ambae yuko nae katika mahusiano alitumia kishawishi cha PESA.

Hali ya mwanaume huyu baada ya kupata hayo yote sio nzuri japo sio kiafya bali kisaikolojia. Hivi waungwana unawezaje kuuza utu na thamani yako ya mwili kwa ajili ya pesa? Na ilihali unajishuhulisha na kazi ina mana msichana yule kashindwa kutosheka na anachokipata? Msichana yule alikua bas anatumia mbinu za hali ya juu sana kum-blind mpenz wake ili ajue nothing is going on lakini embu angalia anavoenda kuumbuka.

Na kipindi hiki magonjwa mengi watu wanatembea na HIV mfukoni, anakudanganya anakupa pesa na unamvulia nguo, je at the end anakuachia nini?

Naomben comments zenye advice.

TIP: period of relationship 4yrs.
 

Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
1,773
2,000
huyo jamaa alikuwa "fala" sana, msichana sio wa kujionesha mstaarabu sana machoni pake, mfanyie ustaarabu moyoni ila si machoni, unadhani wanaume wote wanaoomba kuduvua mademu zao kabla ya ndoa ni wajinga? duuh namuonea huruma sana yani.., now where is the virginity? it's gone to hell... MVUMILIVU HULA MAJIVU!
 

pistmshai

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
1,315
2,000
Kuna uwezekano mkubwa sana huyo msichana hakuwa bikira, anyway, hajalishi sana..
Nampa pole kwa pigo alilopata la kumpoteza mtu aliyempenda kwa matumaini makubwa sana ya baadae.
Ila ingawa kapoteza vitu vingi kwa ajili ya huyo bitch, ashukuru mungu amemtambua kuwa ni mtu asiyemfaa kabla hajamuoa. Pia hajaachiwa magonjwa,
Wapo wazuri kuliko huyo Slut. Atulie arekebishe mambo yake kwanza halafu ndio afikirie namna ya kuanza upya.
 

Billions

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
2,851
2,000
Time will tell...
Mwisho wa fadhaa utafka tu..hakika inauma sana... Jinsi wanawake wanavyotunyanyasa dah! haisemeki maumivu yake..tunabaki tu kuvumiliana!!@
Thanks brothers on behalf of our fellow brother, u felt our fellow brother pain meaning you understand.
jappo kuna wanaume watamcrush our fellow brother na kumkejeli lakin a real man and matured one anajua what am talking about (pain), japo najua bado kuna watoto humu so hata ushauri wao utaonekana tu ni wa kitoto, so please kama ni mtoto ni bora ukae mbali,
 

Billions

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
2,851
2,000
Kuna uwezekano mkubwa sana huyo msichana hakuwa bikira, anyway, hajalishi sana..
Nampa pole kwa pigo alilopata la kumpoteza mtu aliyempenda kwa matumaini makubwa sana ya baadae.
Ila ingawa kapoteza vitu vingi kwa ajili ya huyo bitch, ashukuru mungu amemtambua kuwa ni mtu asiyemfaa kabla hajamuoa. Pia hajaachiwa magonjwa,
Wapo wazuri kuliko huyo Slut. Atulie arekebishe mambo yake kwanza halafu ndio afikirie namna ya kuanza upya.
Thanks brother on behalf
 

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,155
2,000
Pole sana kwa ndugu yetu huyo
Mwambie hakuna marefu yasiyo na ncha, amwachie Mungu , huyo mwanamke hajui kua maisha yanaweza kubadilika ndani ya nusu saa tu, aachane nae huyo Mungu, Karma na Destiny ndivyo vitamlipia kisasi
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom