Criminal case iliyotesa hisia zangu

Criminal case iliyotesa hisia zangu

fakhbros

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2013
Posts
388
Reaction score
666
0d34a827777300dc18282f16819d4c7a.jpg

Haikuwa mkoa wa Mara au mkoa wa Shinyanga mikoa ambayo ina record ya matukio ya kinyama hasa matukio ya mauaji kwa vikongwe na albino
Mikoa ambayo ukiishi huwezi kukosa story za matukio ya vifo vya kinyama ambavyo hutendwa na wakazi wa maeneo hayo.

Ilikuwa ni mwaka 2004 baada ya kumaliza mafunzo ya awali katika chuo cha police (CCP)

Nikiwa katika majukum yangu ya kila siku katika kituo cha police wilaya ya mleba mkoani Kagera mida ya saa Tisa za mchana siku hiyo nilikuwa upande wa reception kama ujuavyo reception ya police haina karibu kwa mteja anaefika office hiyo zaidi ya kumuuliza Mgeni wako shida iliyomleta pale..

Kilikuwa nikipindi cha masika katika mkoa wa kagera mvua zenye vipindi vya muda mfupi zilikuwa zinaendelea kunyaa
Hali ya baridi haikuwa hali ngeni kwa mfumo wa miili yetu
Tukiwa katika makoti yetu malefu ambayo hutolewa na Jeshi kwa ajiri yakuwasaidia staff wake hasa katika nyakati za namna hiyo
Story za hapa na pale zikiendelea kama ilivyo katika office zingine za uma hapa nchini Tanzania ghafula tuliowaona vijana wawili wakiwa wamepakizana katika baiskeli huku mmoja akionekana kuwa ni abiria katika usafiri ule
Macho yetu yalibaki kuduwaa kutokana na hali aliokuwa nayo yule raia alieonekana abiria katika msafara ule
Nguo zake alizokuwa amevaa zilijaa damu huku mkono wake wa kuume akibebelea Panga lilojaa damu japo yeye hakuonekana kuwa na jeraha lolote mwili kwake.

Lilikuwa nitukio lilomshutua kila mmoja huku tahadhari kubwa ikichukuliwa kutokana na hali iliokuwa imejitokeza mbele yetu
Huku SMG zikiwekwa tayari ghafula yule kijana alie jaa damu mwilini ilikuwa amesimama mbele ya meza kubwa ya Jeshi la police huku akitamka Maneno ambayo kwa kiasi furani yalijaa hamaki kubwa moyoni mwake

Alikuwa akisema tayari nimekwisha maliza kazi twendeni mkachukue minofu yenu haraka.

Hakuna alietambua bwana huyu alimaanisha nini kutokana na kauli zake hizo naamini kwa jinsi alivyokuwa ungedhani anamaanisha minofu ya Mbuzi au Kondoo sababu pamoja na hamaki aliokuwa nayo hakuonyesha kuwa ametenda jinai

Kama ilivyo kawaida katika Jeshi lolote nchini kabla ya kuchukua hatua yoyote tulimtaka kuweka silaha yake chini kisha tukamuamulu kuchuchumaa chini hakuwa mbishi amri zote alizitii huku akiendeleea kututaka kwenda kubeba minofu yetu..

Baada yakumtia pingu nakujilidhisha kuwa sasa alikuwa katika hali salama

Tulianza kwa kumhoji yule kijana ambae alikuja kampakia huyu mtu ambae alionekana kuchanganyikiwa katika majibiano yetu na kijana huyu alikili kumfahamu huyo mtu sababu alikuwa ni mkazi katika kijiji ambacho kijana huyu alikuwa anaishi lakini hakuwa na record yeyote kutokana na uhalifu ambao ulikuwa umetendwa na jamaa yule
Alitueleza kuwa hata yeye alitekwa na huyo jamaa na kumtaka kumuwahisha kituo cha police kwa usafiri wake wa baiskel akasema hata yeye alipo jaribu kumbishia alimwambia kuwa uhai ulikuwa unahesabika kwa sekundi kabla yakujiunga kuzimu..

Tukiwa bado tunaendelea kumhoji huyu dreva kundi la watu Tisa liliingia ghafula pale kituoni huku mama mmoja akipiga kelele za maombolezo kuhusu kuawa mwanae hapo ndipo tulipogundua tafsiri ya minofu

Aram ya halufu ya kifo ilianza kugonga katika nyoyo zetu
Hisia za tukio la mauaji lilikuwa lipo bayana mbele ya macho yetu japo hatukujua alieuawa lakini tayari tulikwisha muona muaji ndie aliekuwa mbele ya macho yetu
Hatukujua aina ya mauaji yaliokuwa yametendwa na mhalifu yule.
Tulihitaji kuchukua maelezo sahihi kutoka kwa wale raia waliokuja pale huku nguo zao zikiwa zimelowa kutokana na mvua iliokuwa ikiendelea

AMRI YA OCD
Baada ya meelezo yasiojitosheleza kutolewa Mkuu wa police wilaya alituamuru kufika eneo la tukio japo gari la police halikuwa na Mafuta yakutufikisha eneo la tukio mbinu mbadala zilihitajika ili kuweza kutekeleza Kazi ya viapo vyetu katika fani hii ya kulinda rai na Mali zao ilituchukua masaa mawili kupata mafuta hasa baada yakuangalia record za wahalifu waliokuwa Rock up kupitia Mali walizokuwa wameoredhesha counter
Si haba kiasi cha shilingi 35000/= kilipatikana kutoka chanzo hicho cha mapato

Msafara wetu haukumuhusu yule tuliokuwa tukimuhisi kuwa ndio muaji Bali tuliwabeba wale raia Tisa huku muaji na mateka wake tukiwasweka rockup ili waweze kutusaidia katika upelelezi wetu.

ENEO LA TUKIO.
Sikuwahi kuona tukio la mauaji ya kinyama kama tukio nililokuwa nikilishuhudia kupitia macho yangu ilihitaji moyo wa ujasiri kuendelea kuangalia tukio lile halikutafautiana na matukio ya mauaji ya Kimbali ambayo yalikuwa yakionyeshwa katika television mbalimbali ulimwenguni

Muuaji alikuwa amemua mama ambae alikuwa ni mjamzito pamoja na bint ambae umri wake yapata miaka 14 ambae alikwenda kwenye familia ya marehem ili kusukwa nywele zake lakini baada ya muuaji kumua yule mama mjamzito alilipasua tumbo la mama yule na kumtolea kile kichanga tumboni kisha nacho alikicharanga mapande mapande kama namna alivyo wacharanga wale wengine wawili..

Baada ya muaji kutimiza lengo lake la mauaji inasemekana aliipakia miili ya wale marehem katika mkokoteni uliokuwapo pale kisha akawa anajaribu kuipeleka miili ya marehem kituo cha police kabla ya kumteka mtu alie mleta kituo cha police..

Baada ya kuitoa miili ya wale marehem na kuifikisha hospital nilipewa Kazi ya kuchukua maelezo kwa yule mtuhumiwa na OC-ID

Moyo wangu ulikuwa umejaaa simanzi usiku kucha sikupata usingizi kutokana na picha ya mauaji niliokuwa nimeiona mchana wake tokea niangaze Kazi hii ya upelelezi toka nimalize mafunzo yangu pale CCP Moshi hii ilikuwa ni kesi ngumu sana kwangu nilikuwa nikijiuliza namna gani ningeanza kuchukua maelezo kutoka kwa yule mtu ambae alionekana dhahiri kuchanganyikiwa kutokana na lile tukio alokuwa ametenda

Japo nilihisi mbinu za kimabavu zingeweza kunisaidia katika kupata ukweli toka kwa kiumbe yule
Lakini nilijisemesha moyoni kama njia hii ya mabavu ingetumika ningeweza kukosa ushilikiano kutoka kwa huyo mtuhumiwa
Nilijisemea moyoni kuwa mabavu haikuwa suruhu katika kupata ukweli

Asubuhi yake baada tu yakuingia offisini nilikwenda kuongea na Mkuu wangu wa Kazi nakutaka kupata njia sahihi za kumhoji yule mtuhumiwa

Nilimkuta Mkuu akiwa tayari amekwisha ingia ofisini kwake ofisi ya Mkuu ilijaa faili mbalimbali za matukio ya kiharifu pale wilayani huku kukiwa na meza kubwa chakavu iliozungukwa na viti vitatu mbele yake huku kiti kimoja akikalia mwenyewe.

Baada ya kuingia alinikaribisha kwa bashasha huku Sharubu zake zikionekana wazi kuwa Jana yake alikua ametumia rubisi

Aliinita kwa jina langu akiniita Aloyce vipi Kazi yako umefikia wapi
Kuhusu mauaji ya jana?

Nilimwambia kuwa nimefika pale ofisini ili kupata namna sahihi ya kuipeleleza kesi hii

Mkuu aliniangalia kama mtu aliekuwa akinihurumia huku akiniambia umepewa jukumu - jukumu ambalo matokeo utakayo yapata ndio yatatumika kama sheria na matokeo hayo ndio yatakayo amua mustakbari wa uhai wa mtu wa nne lakini kutokana na mazingira ya tukio hili naamini upelelezi wako ndio utakao ifanya mahakama itoe uamuzi uliosahihi
Kumbuka umebeba haki na batili katika kichwa chako ni busara zako ndizo zitakazo kufanya kuchagua namna sahihi katika kupata ukweli.

Baada ya hapo Mkuu alinitaka nikaendelee na Kazi na baada ya weak nimpatie report

Siku ya tatu toka tukio litokee nilimuomba mtuhumiwa kutolewa rockup ili niweze kumsahili tayari mchoro kamili na history ya mtuhumiwa nilikuwa nayo katika file langu hivyo nilihitaji uthibitisho wake yeye

Hakuwa mtata katika maelezo yake lakini nilipofika katika kutaka kujua chanzo cha yeye kufanya unyama huo nilimuona akilia na kuniambia kuwa ameua watu wasiokuwa na hatia

Chanzo cha mauaji hayo alisema ni mme wa marehem kuzini na mkewe wakati yeye akiendelea na shughuli zake za uvuvi na nia ya kufika nyumbani kwa marehem nia yake nikumua mwanaume lakini bahati mbaya baada ya kumuuliza mkewe alijibiwa vibaya ndipo alipo amua kumua mwanamke kisha akamue mwanaume ambae ilisemekana alikuwa Imam pale kijijini

Mahakamani.
Kesi hii ilipitia katika mikono y Jarge watatu ila kila alieanza kesi hii alijitoa

Report ya mkemia:
Japo ilichelewa sana kufika ofisi ya RCO mkoa wa kagera lakini report hiyo ilisema kuwa baada ya kupima sample za damu katika nguo za marehem na mtuhumiwa matokeo hayakuonesha uhusiano sababu damu ya wale marehem ilikuwa ni damu ya mwanadamu huku sample za damu zilizokutwa kwenye nguo za muaji na damu ya iliokutwa katika panga ilikuwa ni damu ya myama kwa. Matokeo haya hapakuwa na ushahidi mwingine wakumtia mtuhumiwa katika hati japo kwa aslimia 75% niliamini kuwa huyo ndie muaji halisi..

Nilijilaum sana upelelezi wangu kushindwa kumtia hatiani yule jamaaa.

Ila kila nikiwaangalia watuhumiwa waliojazana magereza huku wafungwa wengine wakifungwa vifungo ambavyo hakuna mwanadamu anaeweza kuishi umri huo
Pia mamlaka husika kushindwa kutimiza wajibu wake hasa wafungwa ambao tayari mahakama zilisha wahukum vifo na hukumu hizo kutokufanyika

Naamini endapo sheria ya kifo ingezingatiwa idadi ya matukio ya mauaji ya kinyama ingepungua katika Jamiii yetu
Lakini kutokusimamiwa kwa sheria hii ya kifo matukio ya aina hii katika jamii hayawezi kukoma.

By. Rs Mchunguzi
 
Vita ni vita muraa ..
panga kwa pangaa..
 
Vipi hiyo confession statement aliyofanya, alikuja kuikana?? AU wewe mwenyewe ulitaka kuthibitisha mashitaka yako kwa kutumia damu pekee?? Hakukuwa na mashahidi??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daah, jinsi ulivyo simulia kwa ujuzi ni kama unashuhudia hilo tukio. Mkuu unafaa kuandika vitabu, au kuandika script za filamu kama ukiongezea kidogo ujuzi wa kazi za kutengeneza script za filamu.
 
Chanzo chote ni uzinzi. Mke wa mtu ni sumu.
Tendo la lisaa 1 unapoteza mke na mtoto.
Wengi wanaotembea na wake za watu hufa kizembe sana na wengine hubaki kuwa vilema vya maisha hata kupoteza ndugu.
Rizika na mkeo
 
Mbona kama umekubali kushindwa mapema ivo? Ushahidi sio wa forensic peke yake. Jitahidi umpate muhusika na afikishwe mbele ya sheria, utapata thawabu mbele za Mungu na utawapa familia za marehemu closure
 
Mkuu fakhbros,nimekuja kishtuka kuwa ni "tungo" baada ya kufika tamati na kusoma michango ya wana jamvi. Kongole kwa umahiri mkubwa katika utunzi.
 
Mbn maelezo hayajitoshelez mkuuu???nin kilitokeaa baada ya kugundua kuwa sampuli za damu ya muaji na dam ya marehem hazicolereti???incomplete explanation na ndomana hatupnda bong muvi mana kumalizia kwao ni shida yan anaharib kila mahali kama wew ulivofanya axee ,,, ,bora niend korea tuu

Ni miMi CHalIIiiii Ya "R"
 
Hatari aisee.
Ila naamini kama msimuliaji ni polisi hawezi kujidisclose kiasi hiki.
 
Ina maana mkemia Alitoa taarifa ya uongo au kuna mtu hapo kati alibadirisha nguo aka weka wenye damu ya mnyama ili kupoteza ushahidi? Vipi ushahidi mwingne nao haukufanya kazi ,hakukuwa na eye witness,confession ya mtuhumiwa kwa nini haikuoewa uzito au ilikuwa repudiated?
 
Back
Top Bottom