Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,611
Dar es Salaam. Thamani ya mauzo ya hisa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) yalipungua kwa asilimia 35 wiki iliyopita huku Benki ya CRDB ikinufaika kutokana na kupanda kwa bei.
Hisa moja ya CRDB iliuzwa kwa Sh180 siku ya Jumatatu lakini ilipanda na kufikia Sh 205.
“Mara nyingi hisa za CRDB zikishuka mpaka Sh 170, mahitaji yake sokoni yanaongezeka na ikifikia hatua hiyo, bei yake hupanda na hicho ndicho kilichotokea sokoni wiki iliyopita,” alisema Ofisa wa Fedha wa Kampuni ya udalali wa soko la hisa ya TIB Rasilimali Limited, Makurwe Mauna.
Alisema CRDB imekuwa na wanahisa wa kudumu katika kipindi cha miaka miwili kutokana na bei ya hisa zake kuwa za gharama nafuu.
Jumla ya Sh 3.9 bilioni zilipatikana kutokana na mauzo ya hisa za kampuni mbalimbali wiki iliyopita huku CRDB ikiingiza Sh 3.5 bilioni, sawa na asilimia 90 ya mauzo yote.
Chanzo: mwananchi