CRDB Simbanking na Airtel Money, M-pesa

Goodrich

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2012
Posts
2,091
Reaction score
1,179
CRDB Simbanking wakati inaanza kulikuwa na huduma ya fund transfer kwa wateja wa Airtel Money na M-pesa ie ilikuwa inawezekana kuhamisha fedha kutoka CRDB Account kwenda Airtel Money au M-pesa.
Hii ilikuwa inawasaidia sana wateja wa CRDB waliopo sehemu ambazo hazina Benki kwani waliweza kuchukua fedha zao kutoka kwa mawakala wa Airtel Money na M-pesa hata vijijini.
Huduma za aina hiyo kwa sasa hazipo tena kwa wateja wa Airtel, na kila ukiuliza wanasema wanashughulikia itarejea punde. Sasa ni zaidi ya mwaka.
Mnaofahamu kinachoendelea tujulisheni maana kwa sasa benki ni nyingi just a matter of choice !
 
Mkuu, juma lililopita nilihamisha pesa kutoka CRDB kwenda M-Pesa bila chenga. Labda ujaribu tena!
 
Mkuu, juma lililopita nilihamisha pesa kutoka CRDB kwenda M-Pesa bila chenga. Labda ujaribu tena!

Nadhani kwa M-pesa huwa haisumbui sana, tatizo ni kuhamishia Airtel Money.
 
Reactions: SMU
Mkuu, juma lililopita nilihamisha pesa kutoka CRDB kwenda M-Pesa bila chenga. Labda ujaribu tena!

Hujamwelewa! Anachosema ni kwamba siku hizi huwezi kuhamisha pesa toka CRDB kwenda Airtel Money.
 
naomba pia kujua. hivi nikiwa nimesajili crdb simbanking kwa line ya tigo kisha nataka kuhamisha fedha kwenda line nyingine ya vodacom kwa Mpesa mbona huwa inakataaa? au mpk huduma zote uwe umesajili mtandao mmoja?
 
Huwezi kufanya hivo Mkuu. kama ulisajili kwa tigo then tumia tigo pesa, voda ni m-pesa. ni kwa mtandao ule tu uliosajilia
 
Niliwahi kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti kwenda airtel money lakini haikufika licha ya akaunti kuonyesha fedha imetoka. Fedha hatimae ilirejeshwa baada ya kufuatilia kwa siku kadhaa na nilikatwa charge. Baada ya hapo nilitaka kutapeliwa na mtu alitepiga simu akidai ni mfanyakazi wa benki akitaka password ili nisipate tena shida iliyonipata. Nilimshtukia na kuijulisha benki nao wakadai huyo mtu atakuwa wa Airtel. Nilishangaa huyo tapeli kujua shida niliyokuwa ninepitia.
 
Ukitoa password kwa mtu yeyote kwa njia ya simu UJUE UMEBUG MEEEEN!!!!![/

MIZAMBWA
NABII MTARAJWIA!!!
 
Hilo tatizo hutokea sana. Fedha inakatwa na haiendi unakohamishia ukifuatilia unasumbuliwa then baaadaee ndio wanarudisha wkt charge zimekatwa na transfer transaction haijafanyika
 
Kifupi pamoja na promo zote,airtel money ni majanga matupu

Airtel money si wa kulaumiwa katika hili. Inconveniences zote hutokea from within the CRDB - Simbanking department
 
Airtel money si wa kulaumiwa katika hili. Inconveniences zote hutokea from within the CRDB - Simbanking department

Sidhani kama CRDB ndiyo tatizo! Ingekuwa hivyo uhamishaji kwenda M-PESA ungekuwa kizungumkuti, nimehamisha punde tu toka CRDB kwenda M-PESA bila chenga. Airtel Money inaweza kuwa ndiyo tatizo, cheap is sometimes expensive.
 
Jana nimewauliza CRDB tatizo. Wanasema wamesitisha mkataba na Airtel. Taarifa ndio hiyo
 
Wameweka vifanyakazi fulani vijizi vina tamaa ya kuwa na maisha ya juu kwa muda mfupi. Hata pesa ikihamishwa kule toka CRDB ilikuwa kuitransfer shughuli mpaka wakutafute wakuulizie password yako kila mara ili wajaribu kuiba mpaka zilikuwa zinarejeshwa kwenye account ya CRDB baada ya wiki mbili. Naona labda ndiyo maana CRDB wamesimamisha huduma.
Kifupi pamoja na promo zote,airtel money ni majanga matupu
 
Huwezi kufanya hivo Mkuu. kama ulisajili kwa tigo then tumia tigo pesa, voda ni m-pesa. ni kwa mtandao ule tu uliosajilia

labda kama siku hizi wamebadilisha, mi nilijisajili na crdb simbanking kwa kutumia tigo na nilikuwa nanunua muda wa maongezi kwenda voda,pia nilikuwa nahamisha ela kwenda m-pesa. Sema niliamua kuiblock baada ya mwizi mshamba kunipgia simu eti nimpatie pasword. Nilimtajia ya uongo
 
Huwezi kufanya hivo Mkuu. kama ulisajili kwa tigo then tumia tigo pesa, voda ni m-pesa. ni kwa mtandao ule tu uliosajilia

Acha kupotosha wenzako.
Simbanking unaweza kuhamisha kwenda mtandao wowote mradi huduma au mtandao upo kwenye menu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…