Tofauti na matawi mengine ya CRDB hapa hakuna dirisha special la watu wanaokuja ku-deposit hela zaidi ya millioni 10,matokeo yake foleni ni kubwa mno kwa ajili ya watu kusubili mtu mmoja au wawili wanao deposit mamilioni ya shilingi,mbaya zaidi kuna madirisha manne ya ma teller lakini yanayotoa huduma ni mawili tu,mmoja wa tatu kafungua kidogo kisha kafunga na kuweka kibao hakuna huduma,nilikuwepo mwenyewe leo hii na nadhani pia uzito wa wafanyakazi wa tawi ili unachangia huduma hafifu na foleni kubwa.