CRDB Is this stupidity or lack of caring?

This is bull shit men...inabidi tufike pahala hata ATM card tusitumie....unaingiza tu namba za siri.....
 
Pole sana mkuu, lakini inaelekea CRDB hawana umakini.
Mimi nina huduma kama hiyo Exim Bank, hamna tatizo.
 
Daah yaani CRDB ni bureee kabisa aisee ni wa kuachana nao tuu, Mimi nlitoa hela kutoka kwenye M pesa katika ATM ya CRDB pesa hazikutoka kwenye mashine huku mpesa wakituma sms kuwa hela imeenda CRDB, sasa kuwasiliana nao wakajibu ndani ya saa 72 pesa itarudi ila sasa ni mwezi na hela hazijarudi na kila ukiwasiliana na customer care kupitia call center ni viswahili kila leo, mara tatizo lako litashughulikiwa ndani ya siku 10, mara mwengine tatizo lako halijaripotiwa mara mwengine tutakupigia simu kabla ya saa kumi, wengine kampuni inayohusika na kurudisha izo hela ipo kenya so mpaka waconfirm, yaan hawajielewi na hawajui nn wanafanya... kama mimi ndo ningekua na hela zao nawazungusha mwezi mzima wangenielewa? CRDB waache kufanya kazi kwa mazoea izo ni pesa za watu na mpaka mtu anafuata huduma kwao ujue anadharula
 
Pole sana, hao ni kama tigo, customer service ni zero, tigo niliwahama nikatumia halotel, CRDB nikahama nipo exim now, makato makubwa kidogo kuliko CRDB lakini huduma afadhali.... Funzo:Tusiwe wagumu kubadilisha brand kwa faida yetu.
 
Huu uozo sio CRDB tu, mimi nimekutana nao TRA Mwenge. Nimeenda kuulizia taratibu za kufanya De registration ya chombo cha moto. Mama niliyemkuta Inquiry Desk akaniuliza kwa kustaajabu...'de registration?, ndio nini sasa?' in such a way watu wawili wakaniuliza kwa pamoja 'au umekosea kutamka kaka?' Aliponishangaza, alinipuuza na kuendelea na watu wengine. Nikamsisitiza huo utaratibu upo na hata kwenye tovuti yenu upo ila page ni nzito sana haifunguki, hapo ndio akaniambia basi nenda dirisha la magari ukaulize huko
 
Imenipa hasira..manake si CDRB tu,kila pahala pana aina ya huo usumbufu,
 
Unprofessional workers is the big challenge to our giant bank here in Tanzania.
 
Kwa haya majibu uliyoyapata kiongozi pole sana.
Inatia hasira mi nimekusoma tu nimekasirika je wewe ilikuaje!?[emoji23] [emoji23]
 

He, yaani nimetokewa na exactly scenario kama yako na wamenijibu hivyo hivyo. Kwa hiyo ndivyo wanavyokula? Wanaiba hela yetu kidogo kidogo na kusitisha kutuma taarifa drawing inapofanyika! Mbona at time 'T' watakamatwa tu? Labda washirikiane na audit team.
Kaaazi kweli kweli, ukienda ku draw hela yako wawatonye majambazi, hela yetu wadokoe mh
 
Tatizo wanapeana ajira kwa kujuana bila kujali professional ya mtu ndo chanzo chanzo cha hayo yote
 
Sasa ulilipwa mkuu?
Ofcourse, walitaka kunipiga dana dana za sijui eti network ya kuangalia statement hakuna, ooh sijui andika barua, ooh sijui kamuone manager, ooh sijui manager hayupo.., ghafla wakashangaa macho yangu yanaanza kuwa mekundu, ghafla nikaanza kuwa mwekundu mwili mzima na kuhema kwa spidi sana.., niliwaka kidogo nimchomoe yule jamaa wamapokezi nimtoe nje tukaongee vizuri, bila kuwafanyia fujo watakuzungusha hadi basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…