CRDB Imelemewa ATM Card hazipatikani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CRDB Imelemewa ATM Card hazipatikani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MVUMBUZI, Nov 14, 2011.

 1. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Hali ni mbaya CRDB kwa kushindwa kuwapa wateja wao ATM kadi zao kwa muda wa wiki tatu kama wanavyowaelekeza
  Kwa sasa nina listi ndefu ya wateja wa CRDB ambao wameshindwa kupata ATM card zao kati ya Agost na November 2011. Kuna wale walio renew ATM card zao na wale wanaotaka mpya na wengine Master card. Inaonyesha wazi CRDB imelemewa na wateja na ukweli wa wazi unadhihirika kwenye orodha ya wateja wanaosubiri ATM kadi tangu Agosti bila kuwepo dalili la kupata.

  Benki za NBC, Stanbik, standard Chartered na Barclay wako juu sana kwa teknolojia ya ATM ila CRDB inakufa kabisa kwani ina teknolojia ya zama za ujima ndio maana mteja atasubiri ATM kwa miezi kadhaa badala ya wiki 3 kama zamani au siku moja kama ilivyo kwa NBC.

  Hali hii inakera mno kwani hii ni dhahiri kwamba wameshindwa au wanakaribia kutoka mashindanoni . Mbaya zaidi hawawaambii wateja ukweli ingawaje wanajua wazi kuwa hawapati ATM kwa siku za karibuni. swali ni kwa nini kama wanajua hilo wasiwaambie wale wanaotaka ATM kadi kwenda kwingineko?
   
 2. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Wateja wamezidi target yao, hivyo wameshindwa kuwahudumia na kawaida huwezi kuwakataa wateja hata kama wamezidi capacity ya bank. Watarecover! Hao NBC unaosemea, hawana huduma zingine mhimu hivyo inapunguza mambo mengine kuyaweka kwenye ATM card wakati wa kuzitayarisha.
   
 3. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Tatizo unapokuwa huna ATM card unalazimika kupanga mstari na hawasemi zitakuja lini hawa
   
 4. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Duh, hapo kazi sasa. Wiki tatu nilizopewa mimi zinaisha tarehe 18 Novemba 2011, manake sasa nihesabu maumivu tu.
   
Loading...