Sniper
JF-Expert Member
- Mar 8, 2008
- 2,008
- 949
Hii CRDB mnatutendea vibaya sana! 😡 Jana mmekata hela kutoka kwenye akaunti yangu bila idhini yangu. Hata mbaya zaidi, nimetuma hela kwenda M-Pesa na hazijafika wala kurudi tena kwenye akaunti yangu. Hii ni dharau kubwa kwa wateja wenu.
Hivi mnajua maisha yalivyo magumu huku chini? Kila senti tunayoitafuta ni kwa shida, halafu ninyi mnachezea jasho la watu namna hii? Tunawaamini muweke na kutunza fedha zetu salama, siyo kuzichezea kama mchezo wa kamari.
Tunauliza maswali na hatupati majibu. Hivi hii ndiyo huduma mnayosema ni ya “kibunifu na ya uhakika”? Sasa mtu akipotezewa hela hivi ataendelea kuwa na imani na benki kweli?
Mnatufanya tufikirie mara mbili kama kweli ni salama kuweka fedha zetu CRDB. Rudisheni hela zetu, na muache kuwakandamiza wananchi mnaotegemea ili muendelee kuwepo! 😡