CRDB Bank mpaka kanisani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CRDB Bank mpaka kanisani!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ng'wanamakamya, Dec 24, 2011.

 1. n

  ng'wanamakamya Member

  #1
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 35
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jumapili ya tarehe 18 Desemba, 2011nilibahatika kusali misa ya kwanza katika Kanisa Katoliki la Mt. Patrice, Morogoro. Niliona maajabu ua kituko hali iliyonilazimu kuandika katika Jamii Forum ili niweze kuwashirikisha na kupata ushauri ma maoni ya wadau. Issue yenyewe ni kwamba benki ya CRDB Mkoani Morogoro waliomba misa ya shukrani kwa ajili ya wateja wao! Ulikuwa ni mjumuiko wa matawi yote yaliyoko Morogoro. Misa iliongozwa na Askofu Mkude.

  Katika mahubiri, Askofu Mkude alionyesha kushangazwa kwake na benki kuomba misa! Inakuwaje benki waombe misa. Pia aliwashukuru kwa kumtanguliza Mungu katika shughuli zao za kibenki na kuwaasa wafanye kazi kazi zao kwa uadilifu. Na hatimae CRDB bank wakatoa vipaji wakiwa ndani ya T-Shirts zao za CRDB Family Day.
  Wakati wa kutoa Vote of Thanks, mwakilishi wa benki alieleza kuwa wameomba misa kumshukuru Mungu kwa kuwa benki bora kwa mwaka huu na kwashukuru wateja wao kwa kuwasupport. Na kwamba walikuja kanisani kwa "umoja wao" bila kujali itikadi ya dini zao!
  Wasiwasi wangu: Kwa mwenendo huu tutatarajie nini kwenye nyumba zetu za ibada? Je, Yesu hakupindua pindua meza za watu waliokuwa wakifanya biashara katika sinagogi? Ninavyoona (kwa mtazamo wangu) si ajabu siku zijazo tutakuwa tukisikia kuwa Misa ya Kwanza imedhaminiwa na ya Tigo, Misa ya pili NMB na misa ya watoto NBC Ltd!
  Waumini tunayapeleka wapi makanisa haya? Je, CRDB watadhubutu kwenda msikitini pia kuwashukuru Waislamu kwa kuwa wateja wao kwa "umoja" wao bila kujali itikadi zao kama walivyofanya Morogoro katika kanisa Katoliki?
  Nawasilisha.
   
 2. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Hawawezi kuja msikitini.Sababu ziko wazi. Mfumo wa uchumi wa kikristo unakubaliana na masuala ya riba ambapo kwa Uislam ni haramu. Labda waje kutuambia nao wameanzisha akaunti zinazofuata shariah!
   
 3. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  GT amehamishia uislam wake kwenye benki anayoingoza ya NBC, huko wameanzisha kitengo cha ISLAMIC BANKING!!
   
 4. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Taarifa Muhimu sana hii, na yatatimia
   
 5. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Je,huo ndio mwisho wako wa kufikiri? Kama sio,jipange uje na comment nyingine.
   
 6. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ndiyo maana tunaamua kusali kwenye makanisa strong, huo ni upuuzi usiokuwa na pingamizi. Subiri uone kinachofuata hapo! me kimyaaaa
   
 7. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #7
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwanza siamini, na pili kama ni kweli yametokea basi ni ushauri tu kwamba ni vyema wakati mwingine viongozi wetu wakipotoka tuwakumbushe kwamba waendako siko vinginevyo na kuendelea kkufumbia macho suala kama hili tutaitwa wasafiri vipofu.
  Kwa uzoefu wangu pale ambapo masuala ya mikusanyiko yanapogongana na masuala ya imani kama kwenye sherehe pale ambapo ni lazima kuonyesha kwamba tunamkumbuka mungu kwenye kila jambo masuala ya dina kuu mbili (Ukiristo na Uislam) vyote huzingatiwa na hapa sio suala la madhehebu ndio maana nimetumia "dini kuu mbili".

  Sasa hii ya CRDB na Kanisa hii noma! Naamini ilikusudiwa kuwa ya kufungia mwaka.

  TAHADHARI: Isije kuwa thread hii ilipaswa kuwa kwenye Jokes umeipost huku kwa bahati mbaya.
   
 8. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  kufuru!
   
 9. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Haya ndo matokeo ya serkali legelege inayohongwa suti, imetufikisha hapa tulipo kila kiongozi mahala pake anafanya atakavyo, kiongozi wa benki muislam anaanzisha shariah banking, mkiristo anaomba misa kanisani. kama hatua muhimu za kuiondoa hii serkali madarakani hazitachukuliwa haraka hakika tusubirie maafa hapa tanganyika mithili ya somalia na nigeria. Mimi binafsi nilikuwa na mashaka ya nchi kuongozwa na mswahili tangu 2005, anyway i gave him the benefit of doubt, he has failed.
   
 10. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #10
  Dec 24, 2011
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kati yawachangiaji wote, hakuna aliyeonesha ubaya wa crdb kuomba Misa ya shukrani.Wala hakuna aliyeonesha ubaya wa kanisa kukubali kuadhimisha misa hiyo kwaajili ya crdb. Ninyi mnaopinga hicho kitendo hebu tupeni sababu badala yakulalamika na kulaumu. Hivi kumshukuru Mungu kwa mafanikio ni kosa? Kuomba Misakwa mafanikio ni kosa? Mbona watu binafsi huomba Misa kwa mafanikio yao yakiroho na hata ya kimwili, mf. biashara? Kwa nini liwe ni kosa kwa benki kuombamisa ya shukrani? Ubaya uko wapi? Elezeni vizuri hapo!
   
 11. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #11
  Dec 24, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,155
  Likes Received: 3,353
  Trophy Points: 280
  Unaugua Minyoo wewe na udini wako.
   
 12. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #12
  Dec 24, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Islamic bank ni matokeo ya udini wa JK. Zitafutwa 2015 haraka.
   
 13. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #13
  Dec 24, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hakuna tatizo katika hilo, tena linaimarisha zaidi Umoja wa Watanzania bila kuhangaika na imani zao! Kwa miaka yote Kanisa Katoliki limekuwa likifanya maombi maalum kwa viongozi wa Nchi yetu bila kujali dini zao, wamekuwa wakiombea wagonjwa kwa ujumla wao...kuna ajabu gani kumshukuru Mungu kwa mafanikio ya Asasi ambayo inahudumia binadamu bila kuwabagua kwa imani zao?
   
 14. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #14
  Dec 24, 2011
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,216
  Likes Received: 10,583
  Trophy Points: 280
  mi sioni kama kuna tatizo hapo! kumshukuru mungu ni jambo la kawaida. mbona tuliadhimisha misa kumshukuru mumgu kwa miaka hamsini ya uhuru?
   
 15. ng'wanankamba

  ng'wanankamba JF-Expert Member

  #15
  Dec 24, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 341
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Hali hii ikiachiwa iendelee, tutakuja kukuta hata mabango ya matangazo mbali mbali kanisani. Ifikie mahali kanisa liwe na msimamo.
   
 16. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #16
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  sidhani kama ni shida kwani kuomba misa inaruhusiwa kwa mtu binafsi au kikundi
  ,kwa hivo misa haijaombwa na bank bali waumini au wanajumuia
  tuseme wafanyakazi wa bank .si rahisi misa kudhaminiwa hiyo haipo. kumshukuru mungu kwa mafanikio ni jambo la kawaida.
  hata makanisa yana bank zao mfano mkombozi na efatha banks ondoa shaka tigoairtel au bank kudhmini ibada.
   
 17. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #17
  Dec 25, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,611
  Likes Received: 3,913
  Trophy Points: 280
  haukuelewa...na ulifanya kosa kutouliza palepale au baada ya misa! pole.
   
 18. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #18
  Dec 25, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Wao hawataki riba bwana, sasa kwanini twende msikitini?
   
 19. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #19
  Dec 25, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,934
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Mkuu unaweza kuliweka sawa jambo hili? Nahisi kuna upotoshaji mkubwa katika hili la crdb kuomba/kufanya misa ya shukrani.
   
 20. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #20
  Dec 25, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hakuna tatizo kabisa kwa mtazamo wangu,
  Nawapongeza hao kwa kumkumbuka Mungu wa Kweli kwenye biashara zao,
  CRDB ina wafanyakazi ambao wana imani tofauti lakini waliamua kwenda kanisani kushukuru kwa Mungu wa kweli, wanastahili pongezi
   
Loading...