CRDB bank mbona mnatuibia sana wateja wenu?

mriringa

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2017
Posts
783
Reaction score
835
Nianze kwa kuwasalimia wapendwa wangu wa jamii forums kwa kuwapa pole na majukumu ya hapa na pale kwaani bila kuhangaika na kujishughulisha basi unakuwa mzigo kwa taifa na kwa familia yako kama sio kwa jamii.

Wakati naajiriwa nilifanya tafiti naweza kusema mbaya kwa vile niliangalia sababu moja pekee ya kwanini nijiunge na CRDB na sio bank nyingine na ndio bank niliyotumia wakati wote wa masomo yangu.

Niseme tu kwamba CRDB wateja wenu mmewapa mzigo mzito kwaani makato yenu sasa ni maumivu kwa wateja na yanatutesa kupita kiasi na hadi sasa nipo njiani kimawazo katika kuhama bank yenu na nijiunge hata na NMB kwaani wizi tunaofanyiwa yatosha kusema haufai kwa taasisi yoyote ambayo kwao mteja ni mfalme.

Mwezi uliopita bahati nzuri au mbaya kwa yaliyonikuta sikuchukua mshahara wangu nikiwa na maana sikutoa fedha zangu za mshahara lakini jana nikaomba taarifa ya akaunti yangu hakika nimepata hasira mbaya moyoni mwangu na ya kusikitisha sana. Akaunti yangu kwa mwezi 12/2020na 1/2021 nimekatwa sh 52,000 eti fedha za makato ya kuendesha bank, na tarehe 19.01.2021 nimekatwa 15,000 kwa wakati mmoja hakika mnatuibia sana enyi makaburu weusi.

Hivi kwanini mjiangalie nyinyi tu na msituangalie hata sisi akina bora kunakucha and days goes?? Je makato haya yanatija kwa mteja wenu?? Na je kama mteja hana fedha kwenye akaunti mnaendeshaje bank??

Maamzi yangu ni kwamba kama sitawahama on the sport basi fedha zangu nitazitunza kwenye simu na sio bank. Mshahara ukitoka nawaachia 10,000 pekee ya kutunzia akaunti ambayo ipo kisheria kwa hiyo bank yenu ya makaburu weusi maana huenda mnapoziona pesa kwenye akaunti mnawashwa na kuzichukua kwa vile mimi ni maskini na sauti yangu haifiki Ikulu. Ila mteja ni malme itoshe tu kusema hivyo.

Ila mwisho wa yote Mungu hapendezwi na huo wizi maana hakuna chenye mwanzo huwa hakikosi mwisho.
 
Pole sana mkuu, maisha magumu siku hizi pande zote.
 
Makato yao ni makubwa mno, yaan pesa wanazokata sijui wanapeleka hawa majambazi yaliyohalalishwa kisheria
 
Nianze kwa kuwasalimia wapendwa wangu wa jamii forum kwa kuwapa pole na majukumu ya hapa na pale kwaani bila kuhangaika na kujishughulisha basi unakuwa mzigo kwa taifa na kwa familia yako kama sio kwa jamii.

Wakati naajiriwa nilifanya tafiti naweza kusema mbaya kwa vile niliangalia sababu moja pekee ya kwanini nijiunge na CRDB na sio bank nyingine na ndio bank niliyotumia wakati wote wa masomo yangu.

Niseme tu kwamba CRDB wateja wenu mmewapa mzigo mzito kwaani makato yenu sasa ni maumivu kwa wateja na yanatutesa kupita kiasi na hadi sasa nipo njiani kimawazo katika kuhama bank yenu na nijiunge hata na NMB kwaani wizi tunaofanyiwa yatosha kusema haufai kwa taasisi yoyote ambayo kwao mteja ni mfalme.

Mwezi uliopita bahati nzuri au mbaya kwa yaliyonikuta sikuchukua mshahara wangu nikiwa na maana sikutoa fedha zangu za mshahara lakini jana nikaomba taarifa ya akaunti yangu hakika nimepata hasira mbaya moyoni mwangu na ya kusikitisha sana. Akaunti yangu kwa mwezi 12/2020na 1/2021 nimekatwa sh 52,000 eti fedha za makato ya kuendesha bank, na tarehe 19.01.2021 nimekatwa 15,000 kwa wakati mmoja hakika mnatuibia sana enyi makaburu weusi.

Hivi kwanini mjiangalie nyinyi tu na msituangalie hata sisi akina bora kunakucha and days goes?? Je makato haya yanatija kwa mteja wenu?? Na je kama mteja hana fedha kwenye akaunti mnaendeshaje bank??

Maamzi yangu ni kwamba kama sitawahama on the sport basi fedha zangu nitazitunza kwenye simu na sio bank. Mshahara ukitoka nawaachia 10,000 pekee ya kutunzia akaunti ambayo ipo kisheria kwa hiyo bank yenu ya makaburu weusi maana huenda mnapoziona pesa kwenye akaunti mnawashwa na kuzichukua kwa vile mimi ni maskini na sauti yangu haifiki Ikulu. Ila mteja ni malme itoshe tu kusema hivyo.

Ila mwisho wa yote Mungu hapendezwi na huo wizi maana hakuna chenye mwanzo huwa hakikosi mwisho.
Mkuu, labda ni maagizo toka juu, au tozo mpya ya Tra..
Mi-5 tena🙄
 
Mkuu nakushauri ucheki taarifa zako upya hakuna makato makubwa hivyo ya kuendesha akaunti,binafsi ni mteja waCRDB miaka 15 Sasa.

Huwa unadesturi ya litany’s reconciliation kwa account yako mkuu ili kuweza jua mako ni kiasi gani..
 
Taarifa zipi mkuu sidaiwi mkopo wowote na sikusoma kwa mkopo. Na kama ningekuwa nadaiwa ningeona kwenye bank statement?? Nami nimeshangaa huu mwezi japo sinaga kawaida ya kuangalia bank statement ya akaunti yangu, sasa jana nikataka kutoa M kadhaa nichukue kiwanja baada ya kutoa nikaomba risiti walai nilitaka kuzimia maana sio makato yale.

Na jumatatu nawaendea ofisini siwezi kuibiwa kiurahisi hivyo yaani. Na kama shida kuziona hela kwenye akaunti bora nihame bank au nihamishe namna ya kuhifadhi fedha zangu kwa kufungua NMB saving akaunti.

Nimecho kwa wizi huo na huenda nilikuwa naibiwa toka siku nyingi ila sikuwa na mazoea kuangalia au kuomba bank statement. Kuanzia sasa fedha zangu kwenye simu nitahamishia au kufungua akaunti bank nyingine.
 
Umeniogopesha sana nilipanga nikivuna huu uwele wangu nifungue account crdb bank ya ushirika na maendeleo vijijini..!!
 
Huwa unadesturi ya litany’s reconciliation kwa account yako mkuu ili kuweza jua mako ni kiasi gani..
Nashukuru kwa ushauri wako mkuu. Jana ilikuwa siku mbaya kwangu maana huenda toka siku nyingi naibiwa ila nilikuwa sijui chochote. Mshahara wenyewe wa ngama huu si tutauana jamani
 
Mimi nakumbuka mwaka nipo advance form 5 nilkweka akiba kama elfu 20 tukafunga mwezi wa 12 lakini mwezi wa kwanza baada ya kufungua shule nilitaka kwenda kuchukua elfu 10 nilichokuta ni namba kama frequency za redio kwenda ofisin kwao wanasema huwa wanakata ku update account tangu apo nikawakimbia

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Umeenda kuongea nao lakini waka kueleza hiyo 52k ni kweli kuendesha akaunti? Maana huo mpunga ni mrefu sanaa.

Wang'ang'anie hao wakueleze vizuri ikibidi uongee hata na manager.
 
Taarifa zipi mkuu sidaiwi mkopo wowote na sikusoma kwa mkopo. Na kama ningekuwa nadaiwa ningeona kwenye bank statement?? Nami nimeshangaa huu mwezi japo sinaga kawaida ya kuangalia bank statement ya akaunti yangu, sasa jana nikataka kutoa M kadhaa nichukue kiwanja baada ya kutoa nikaomba risiti walai nilitaka kuzimia maana sio makato yale.

Na jumatatu nawaendea ofisini siwezi kuibiwa kiurahisi hivyo yaani. Na kama shida kuziona hela kwenye akaunti bora nihame bank au nihamishe namna ya kuhifadhi fedha zangu kwa kufungua NMB saving akaunti.

Nimecho kwa wizi huo na huenda nilikuwa naibiwa toka siku nyingi ila sikuwa na mazoea kuangalia au kuomba bank statement. Kuanzia sasa fedha zangu kwenye simu nitahamishia au kufungua akaunti bank nyingine.
Wana huduma ya email mkuu,binafsi napata statement ya akaunti ya kila mwezi kupitia email,jiunge na hiyo utaona kila kitu
 
Hiyo mteja ni mfalme futa kauli hiyo,hyo dhana haifanyi kazi kbsa sikuizi ,wateja ni watumwa.
Watumwa siku zote hawaishi kuwalalamikia ma bwana zao(wafalme) kwa unyonyaji waotendewa.
Wateja wa voda,ttcl,halotel n.k ni ,wanalialia kila leo
Wateja wa eiticl,tiaraei,ma bank,tisiaraei,n.k
Wanalalamika mno na hawasikilizwi ipasavyo..
Sasa huo ni ufalme au utumwa?
 
Af wajanja sana statement wanachelewa kutuma wanatuma kwenye tarehe 13 adi 15. Mtu kama mfanyabiashara unahitaj ufanye hesabu mwanzoni mwa mwezi inakulazimu uombe statement pale ambayo ina makato. Benki sio ile sikuizi
 
Mi mkuu nakimbia mazima kule hel ikitoka nahamishia NMB account yangu wez kwel wale mkuu
 
Karibu NMB benki ya Makabwela! Huku sisi hata buku 5 ikibakia, tunaweza kuihamishia kwenye simu halafu maisha yanaendelea kama kawaida.

Huko CRDB, huwa tunakuja kuvuta mikopo tu, tena ile ya wafanyakazi. Mikopo ya biashara, huwa tunarudi tena Nmb!!
 
Back
Top Bottom