CPU ya HP ina tatizo la kuzima baada ya saa

dadanga

Member
Jan 27, 2019
63
47
Nina computer huwa inafanya kazi Ila Kama baada ya masaa hata saba inazima yenyewe, halafu baada ya muda inawaka tena ,tatizo linaweza kuwa ni nini? Inatumika kwenye video library.
 
Hiyo inaweza sababishwa na power supply, RAM, Feni/ AC kufeli au processor.

Feni ikifeli inasababisha mashine ipate joto kupitiliza hivyo inajizima kujipooza na baadaye kuwaka.

Power supply kama iko hovyo mashine itazima lakini ukiiwasha hapo hapo inawaka.

RAM mashine itajizima lakini itabaki idle. Yaani utaona maandishi kwenye monitor au lile giza la kuashiria mashine itawaka sasa hivi.

Kwa hayo mimi nahisi feni yako ndiyo ishu.

Hata hivyo mimi siyo mzuri sana kwenye hardware kwahiyo hizo ni assumptions ninazokupa za kuanza kuchunguza mwenyewe mashine yako. Washa mashine iangalie feni inavyobehave, kama ina kelele sana au haizunguki mpaka muda upite.
 
Nina HP ya AMD ina hili tatizo,

Ni Elitebook 756 G6. Na nilinunua mpya imetumika miezi 8 tu.

Nimepeleka Warranty center, wakinijibu nitakuja update pia hapa.
 
Back
Top Bottom