COURSES MPYA NA SEKTA YA VIWANDA

Genisys

Senior Member
Oct 14, 2015
158
93
SALAAM..

Nachukua fursa hii kuwasilisha kwenu, shukrani za kipekee sana kwa Raisi wetu kwa kuja na sera ya viwanda ili Tanzania ielekee uchumi wa kati.

Japo kuwa changamoto ni nyingi sana kwenye sector hii ikiwemo uhitaji wa resources za kutosha hususa ni Umeme wa uhakika, ili kuifanya sekta hii ifikie kule tunakotegemea.

AJIRA!!

Viwanda vilivyopo kwa kiasi chake vimesaidia sana kutoa nafasi za ajira kwa watu kwenye vitengo tofauti tofauti. Courses nyingi vyuoni zimekua zikianzishwa ili kuendana na uhitaji kwenye sekta hii ya viwanda.

Lakini mbali na hapo wahitimu wake wamekuwa wakisahauliwa sana, unakuta kijana anasoma course mpya, soko la ajira halimtambui. Yupo chuo anaenda kuomba field sehemu anaulizwa unafit sehemu gani? Hii ni changamoto kubwa sana.

Kingine unakuta hata ajira zinapotangazwa kwenye zile requirements, Hiyo course yake haipo na hiyo nafasi inajikita zaidi kwenye mambo aliyosomea. Huku kuna mfanya kijana awe less competitive.

Nyie wahusika mnapoanzisha hizi course mpya tafuteni na namna ya kumsaidi kijana kupambana mtaani. Sio kuajiriwa tu hata kujiajiri. Baada ya muda fulani mnawaacha wenyewe wajitegemee maana inakua siyo tena ngeni kwenye Jamii. Kuwaacha wenyewe tu wajitegemee sidhani kama watakuwa wamepata msaada wa kutosha.

Mbaya sana kusikia "Hiyo course ni nzuri sana, unasoma halafu ukishagraduate unaona kama mzigo kwako!
 
Watu wa kada ya elimu wajue mtaani kuna uhitaji gani. Kama viwanda vinahitaji watu basi waanzishe hizo kozi. Vile vile mabadiliko ya teknolojia, yaendane na kinachofundishwa, la sivyo tunaishia kuwa na wahitimu wasiokidhi mahitaji ya soko.
 
Back
Top Bottom