Tungeweza kabisa kusimamisha genocide bila ruksa ya mtu yeyote kama tungetaka kufanya hivyo kwani yule mkuu wa kikosi cha UN alikwisha piga la mgambo kuomba msaada,Tulisikia vizuri lakini tuliweka pamba masikioni.. trust me vita ile imetu cost zaidi kiuchumi na kifikra kuliko msaada wetu kusaidia Mozambique.
GAME THEORY,
Naomba utufafanulie kama Tanzania ingeweza kuzuia mauaji yaliyotokea Congo.
Somo la GT ni zuri lakini liko tu theorectical for a normal person to comprehend. Kwenye swala la Rwanda kuna conspiracy theories nyingi sana, but what I can say
Dua you mean kwamba Tanzania hatujaendelea kiuchumi kwa sababu tulitumia raslimali zetu kuwakomboa wengine especially majirani? kama Zimbabwe, Uganda, SA nk? Or Iam missing a point?
Harafu nadhani WITH DUE RESPECT approach yako kwenye foreign policy yetu ni very minimalist! Mzee hakuna anayeishi kisiwani ati! Huwezi kusema eti Tanzania tuliamua kumuachia Mseveni kwa sababu tulitaka kurekebisha uchumi wetu? upi huo? Comrade labda ufafanue zaidi, leo Membe akiadopt mawazo yako, our foreign policy will be a TRAGEDY! Ohh I hope it is not-yet! Otherwise from your comments naona ni ile ile usual over negative indoctrination ya watutsi katika ukanda wa maziwa makuu!
Mkuu whether we like it or not, Rwanda and Burundi are our NEIGHBOURS so is Malawi, Kenya, Uganda, DRC etc we have to live with them na tupendane, na step ya kwanza ni kuwaleta kwenye East Africa Community! Tunaweza tusipende na kulaumu waliofanya huo uamuzi, lakini the bigger picture is umaskini ndo unasababisha yote haya. Leo Kagame kaondoa work permit kwa mtu yeyote anayetoka East Africa anayetaka kufanya kazi Rwanda.....Hiyo ni challenge, harafu tukiona jamaa wanaendelea ndo hapo tunaanza protectionism! My Compatriots Tanzanians TUAMKE tuache visingizio. We either compete or compete! kuwapiga vita haitasaidia chochote! Ndo maana mi nasema kila mara, hii sumu tuliyomwagiwa dhidi ya watutsi ni mbaya sana! Alot needs to be done by us.
Mwanaharakati ameuliza a straightforward question: kwanini Tanzania haikufanya chochote kuzuia mauaji yale ya Rwanda 1994?
Hizi habari za sijui UN, US, Pentagon, UNAMIR na sijui nani kafanya hivi na vile zinatokea wapi jamani? Mimi naona tunajitafutia visingizio tu... tukubali tu kuwa tuliona kujiingiza huko Rwanda hakuna maslahi (si kwa nchi yetu wala kwa viongozi wetu), mbona Idi Amini tulimuandama mpaka Kampala tukamtoa. Gadafi alipopeleka msaada kwa Idi Amin tukawapa kichapo vilevile hatukusubiri cha UN, US, UNAMIR wala nini... kujificha nyuma ya Strategic studies rahisi sana.
WAUNGWANA, TUTATUMIA SABABU ZA KILA AINA KWA NINI HATUKUWASAIDIA MAJIRANI ZETU KIPINDI WALIPOKUWA WANAHITAJI MSAADA WETU, lakini ukweli unabaki pale pale, we as NEIGHBOURS (ACHA HIZO THEORIES ZA INTERNATIONAL COMMUNITY na kutupia mpira UN as if UN can do anything against the wishes of its members...) we failed Rwanda na inabidi tuone aibu kama Bob alivyoandika hapo juu.
Jiulize leo Rwanda ndo anaongoza juhudi za kulinda amani Darfur! Of all countries. I tell you, Africa kwa sasa tunahitaji viongozi kama akina Kagame wenye light touch ya udikteta na vision za kuikomboa Africa! The guy is succeeding wakati sisi wengine ni kumcriticize tuuu bila kuangalia mazuri anayoyafanya!
La muhimu, tujifunze namna ya kuyakabili matatizo kama haya siku za mbeleni. Lakini nitakuwa mnafiki nisiposema kwamba sisi Waafrica hatujifunzi lolote, maana watu wanapukutika Darfur, Somalia, Eritrea, Chad...na the best Africa can do we are bickering and arguing on the right statistics za wanaokufa!!!!!!!!!!!
Mwanaharakati ameuliza a straightforward question: kwanini Tanzania haikufanya chochote kuzuia mauaji yale ya Rwanda 1994?
Hizi habari za sijui UN, US, Pentagon, UNAMIR na sijui nani kafanya hivi na vile zinatokea wapi jamani? Mimi naona tunajitafutia visingizio tu... tukubali tu kuwa tuliona kujiingiza huko Rwanda hakuna maslahi (si kwa nchi yetu wala kwa viongozi wetu), mbona Idi Amini tulimuandama mpaka Kampala tukamtoa. Gadafi alipopeleka msaada kwa Idi Amin tukawapa kichapo vilevile hatukusubiri cha UN, US, UNAMIR wala nini... kujificha nyuma ya Strategic studies rahisi sana.
Mwakilishi
NI kweli hakukuwa na maslahi yoyote, labda kama tungekuwa na sababu tungesingizia humanitarian interest. Kuna Phrase moja wanatumia wamarekani inanifurahisha sana, "you are damn if you do you, are damn if you don't" hapo ndipo tulipofikia Tanzania. Kwa hiyo hatukuwa na sababu yoyote ya kutafuta sifa kwa kutumia pesa na kuhatarisha maisha ya askari wetu.
Ile ya Uganda mimi siwezi kusema sana kwa sababu nilikuwa bado mdogo sikujua yaliyotokea, lakini hata hivyo nadhani ulikuwa ni ujinga tu, tusingemchokoza nduli kwa kum-host Obote yasingetokea yaliyotokea, au tusiruhusu ardhi yetu itumike kuisimbua Uganda yote yale yasingetukuta, labda hii ni issue tofauti.
Hivi clause ya OAU kuhusu non-interference inasemaje? Nafikiri kimsingi ilichangia mataifa mengine kuingilia bila kufuata a lot of red tape.Ndiyo maana Tanzania ikaweka effort katika mazungumzo.
..mbona tumepeleka majeshi Liberia na tumeahidi kusaidia mafunzo Somalia?
..hivi kila wanachofanya Rwanda basi na sisi Tanzania lazima tuige?
..mbona tayari tuna askari wanalinda amani Lebanon? mbona hakuna anayeuliza kama Rwanda wako huko?
..siungi mkono askari wetu kwenda eneo lolote lile nje ya mipaka ambako maisha yao yatakuwa hatarini.
..kama ni kupoteza askari basi tuwapotezi kwa kulinda mipaka yetu.
Jamani,
Nadhani hamfahamu impact ya vita hata kidogo na huo msalaba sijui utaubeba vipi ikiwa wewe mwenyewe una njaa kutokana na jirani yako hana muda na uwezo wa kununua mali yako. wakati huo huo nakubaliana nanyi mnaposema kuwa hatupati malipo ya kazi yetu.
Ni maisha ya kawaida ya Mtanzania (mwafrica) kuwa kila mtu na mzigo wake na ndio maana utakuta mtu tajiri ndugu zake hawana kitu. Kibaya zaidi ni kwamba hata akiwasaidia wao watahakikisha wanampeleka chini.... Yaani kazi kweli kweli.