Could Tanzanian Gov. stop 1994 Rwandan genocide?

Dua,
Pamoja na kuwa hujasema kama hatujaendelea kiuchumi, mimi nasema ni kweli hatujaendelea kiuchumu hata takwimu za Benki ya dunia na IMF zinaonesha hivyo, this is the fact we must all face, kama tukiface ndiyo tunaweza kwenda forward, sio kudanganyana tu. Duniani sasa hivi Tanzania ni among 5 poorest countries, may be among other African countires we are only better than Somalia and Eritrea. Kwa hiyo naona ni kweli hata uchumi wetu haukuwa in a position ya kusupport kazi ya kusimamisha genocide Rwanda.

Lakini mkumbuke pia kuwa tulipigwa kidole na UN walipotuomba askari kwenda kusaidia peace keeping mission Liberia, UN ilitutapeli, kwa hiyo kzai ya Rwanda ilikuwa ni ya kujitolea tu. Na kusema kuwa Genocide imetukost Kibiashara, cost yake ni peanut, ni kweli Rwanda na Burundi walikuwa wanatumia reli ya kati, lakini kusimamisha kutumia reli ya kati hakukuwa na hasara kubwa kiuchumi kama unavyoweza kuimagine. Gharama kubwa kabisa tuliyoipata naweza kusema ni uharibifu mkubwa wa mazingira, kuenea silaha, wakimbizi kubaka dada zetu na wizi wa mifugo. Biashara ya mpakani ni kidogo sana, japo sijui contribution yake kwenye GDP yetu lakini naweza kusema ni ndogo sana,

Swala la kuendelea au kutoendelea linategemea unafananisha na nani? Nchi nyingi za Afrika zinaweza kuwa kwenye level moja katika mambo mengi lakini hii ni topic ambayo ni ya kujitegemea na mimi sina sababu yoyote ya kusema Tanzania tumeendelea kuliko Rwanda au Burundi kwani sina sababu ya kumdanganya yoyote yule katika hilo. Nilikuwa naweka msisitizo kuwa sijasema hilo kama kuna ambaye anataka kuongelea hilo swala anaweza kuanzisha Thread na kuweka kama mada.


Dua, Mimi siyo mtaalamu wa foreign policy neither did I claim to be one SIR! Taaluma yangu ni nyingine, ingawa what I can tell you is that NILIFUTA UJINGA KWA FADHILA ZA KAMBARAGE!! I always believe that hapa JF kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake bila kuonewa as you seem to do kwamba watu tukae kimya. wewe mtaalamu wa hiyo foreign policy tupe shule basi! JF ni shule tuko tayari kujifunza.

Mimi sijakuonea swala ambalo nililolisema ni bora ukae kimya ni la Membe ku-shape foreign Policy ya Tanzania, ndio nikasema ni bora ukae bila kusema neno kwa maswala ambayo huyafahamu. Sina sababu ya kumnyamazisha member yoyote bali ni facts tu the way government works.
 
GT nasema tusijikite kwenye thoeries. Hapa tujadili na kujibu swali. Hiyo UN charter it is always interpreted at the convinence of the concerned parties. Hata Israel kuingia Lebanon anatumia hiyo hiyo Charter! Hata US kuingia Iraq ametafsiri hiyo hiyo UN Charter, Hata Lord Goldsmith(a brilliant lawyer I respect by far) alipoambiwa aandike opinion yake kuhusu involvement ya UK kwenye vita ya Iraq alitafsiri hiyo hiyo Charter! na akasema Blair was right to support the invasion! you can go on and on.....

Dua, Mimi siyo mtaalamu wa foreign policy neither did I claim to be one SIR! Taaluma yangu ni nyingine, ingawa what I can tell you is that NILIFUTA UJINGA KWA FADHILA ZA KAMBARAGE!! I always believe that hapa JF kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake bila kuonewa as you seem to do kwamba watu tukae kimya. wewe mtaalamu wa hiyo foreign policy tupe shule basi! JF ni shule tuko tayari kujifunza.

Ila kuhusu Rwanda, I will say again and again, Tanzania hatukuingilia kuisaidia Rwanda among of the reasons ni widespread prejudice dhidi ya Kagame na RPF especially kwenye utawala wa mwinyi na Malecela. anayesema kwamba Darfur ni tofauti na Rwanda...ningeomba akapitie tena operation nzima ya Darfur na peace process jinsi mpaka leo kulivyo na mgogoro on who should comprise hiyo UNAMID..harafu kwamba cheki imetoka that is flat lie, kilichofanyika ni kwamba wakubwa wa Dunia wamepledge 1.3billion USD, hiyo haina maana kwamba hiyo cheki itatoka leo wala kesho, tumeona pledge ngapi zinakufa natural death??


Hayo ya kupeleka askari kwenye hatari ni part ya jinsi ulimwengu unavyoishi na tunavyorelate kama mataifa..hiyo ni international relation subject na mkuu wangu GT atalielezea kwa mapana maana ni mtalaamu katika hizi analysis...

Kifupi, I am inclined to support generation ya viongozi kama akina Kagame katika Africa yetu ambao wanaweza kuwa bold na kumwambia master mkubwa kama France NO na kukata diplomatic relations! Kwa Africa ya leo ni viongozi wachache saana wanaoweza kufanya kitu kama hicho-Only Nyerere could do it! It doesnt mean kwamba Kagame is always right, but surely what he is doing, offers a grimpse of hope for our continent that with determination we can turn things around.


Masanja:

Hapa tutabiashana mpaka kesho. Mada sio ku-support Kagame. Mada je Tanzania ingeweza kusimamisha mauaji yalitokea Rwanda. Jibu ni kuwa Tanzania isingeweza.

Ukubwa wa pua sio wingi wa makamasi.
 
Could Tanzania Gov.stop 1994 Rwanda Genocide..?.

The answer is Yes.

Tanzania ilikuwa inao uwezo huo.Na ninampongeza sana Rais Mwinyi kwa kutoiingiza Tanzania kwenye mgogoro huo.

SABABU Tanzania iliamua kutopeleka majeshi yake baada ya kujifunza mengi kutoka kipindi cha miaka ya nyuma.Tanzania imejitolea sana kusaidia nchi nyingi kusini mwa Africa mpaka kufikia pahala pa kuharibu kabisa uchumi wake.Kwa hiyo haikuwa jambo la busara kujiingiza kwenye migogoro mingine au kujifanya African police kwa wakati huo wakati uchumi wetu ndiyo ulikuwa unaanza kuamka baada ya kukaribia kufa kabisa kutokana na sera za Nyerere za kusaidia kila mtu.

Na hivyo basi Tanzania iliamua kuwekeza kwenye kusuluhisha mgogoro wa Rwanda tangu hata ya hiyo Genocide ya 1994 kwa Amani kwa kukaribisha viongozi na pande mbalimbali ili kutafuta suluhu.Na kwa kweli mambo yalikuwa yanaenda vizuri tu.

NANI WA KULAUMU:
Kagame na RPF pamoja na ndugu yao Museveni(CIA agent). Hawa ndiyo waliochafua kila kitu.Ikumbukwe kwamba baada ya vita ya kwanza ya Ghuba Marekani ilichukua(na kutaifisha) silaha nyingi za Sadam zikiwemo zile za kutungulia ndege.Silaha hizi zilifika kwa RPF kupitia kwa Museveni.Silaha hizi zilisafirishwa kupitia Misri(Egypt) hadi Kampala-Uganda na baadaye kwenda mpakani mwa uganda na Rwanda. Na RPF walizitumia kutungulia ndege iliyokuwa imembeba Habyarimana na Rais wa Burundi(Ntaharyamira).

Sasa swali ni kwanini 1994? ikumbukwe kuwa kulikuwa tayari na mazungumzo kati ya serikali ya Habyarimana na rebels (RPF)ambayo yalikuwa yanaendelea na Habyarimana alikuwa anaelekea kupata suluhu na kuwapa percentage fulani ya uwakilishi kwenye serikali yake, ila Habyarimana alikuwa naye anapata presha kubwa toka ndani ya serikali yake mwenyewe hasa wale wahutu wenye msimamo mkali ambao walikuwa hawataki kuwatambua au kuwapa rebels(RPF)mamlaka makubwa! Hivyo baadaya ya Habyarimana kusaini huo mkataba pale Dar es salaam 1994, RPF wakaona hiyo ndiyo time nzuri ya kumassasinate kwa kuwa walijua kuwa wataeneza propaganda yao kuwa ni wahutu wenye msimamo mkali wamemuua Habyarimana!

USHAURI:
Mimi ningewashauri wananchi wa Rwanda wamweke kitimoto Kagame ili wamuhoji ni kwanini aliamuru kutunguliwa kwa ndege ya Habyarimana huku mkataba wa amani ulikuwa tayari umeshasainiwa na hali ulikuwa unawapa asilimia kubwa watutsi ya uwakilishi kwenye serikali ya Habyarimana.Na waache kuilamu Tanzania na UN kwa matatizo ambayo Kagame amewasababishia.
 
Hata mimi naona maelezo ya GT ni very complex. Bila kuzama ktk geopolitics kwa sababu sio fani yangu, naomba kueleza yafuatayo.

1.Tanzania ilikuwa ikiunga mkono utekelezwaji wa makubaliano ya amani ya Arusha. Kama Habyarimana aliamua kusaini makubaliano hayo basi tulikuwa na sababu zote za kumuunga mkono.

2.Kama Tanzania hatukumpenda Kagame, au RPF, ni kwasababu ya kutukukubaliana kwao na mkataba wa amani wa Arusha.

3.Kifo cha Habyarimana kinaelezewa na theories mbili. Ya kwanza inadai aliuwawa na Hutu extrimists ambao walikuwa hawakubaliani na Arusha accords. Ya pili, inadai aliuawa na RPF kwasababu all along hawa walikuwa hawataki ku-share madaraka na Wahutu. Kuna uwezekano basi Habyarimana alikuwa moderate.

4.Majirani ya Rwanda ni Tanzania,Uganda,Burundi, na Zaire. Sasa Uganda alikuwa tayari imechukua upande. Burundi ilikuwa ni sehemu ya tatizo, na Zaire ilikuwa imedhoofika. Naamini kwamba toka mwanzo Tanzania iliamua kwamba haitajiingiza kijeshi Rwanda na ndiyo maana ika-facilitate mazungumzo ya amani Arusha.

5.Kagame is hiding under internationals community guilty of in-action during rwandan genocide. Kagame na RPF wanahusika na mauaji ya kikatili na uporaji wa mali uliotokea na unaoendelea DRC.

6.Kagame amefanikiwa kuwa-label Wahutu wote kama "genocideire." Katika mazingira hayo hakuna nchi iliyoko tayari kuwatetea Wahutu kwa jambo lolote lile.

7.Hebu tujiulize Kagame anapataje ushindi wa tsunami ktk chaguzi za Rwanda? Ninavyoelewa mimi Wahutu bado ni majority Rwanda. Je, wameanza lini kumpenda Kagame kiasi hicho?

8.Habari ya Kagame kuondoa "vibali vya kazi" kwa raia wa Afrika Mashariki is just a gimmick. Mimi ningemchukulia seriously kama angesema anaruhusu wamachinga wa Tanzania kwenda kuendesha shughuli zao Rwanda.
Hapo kwenye 4&5, mkuu ulimaliza kila kitu, nafikiri hasa namba 5 hapo juu ndio sababu inayowafanya Tonny Blair na Bill Clinton waendelee kumtetea Kagame, si kwa mazuri bali kwa uzembe wao, ingawa ukisoma sana unaweza ukaona ni namna gani Marekani walikuwa behind the 1994 massacres of Hutu wengi karibu 600,0000 na Watusi wachache karibu bya 200,000 japo hadithi sasa imegeuzwa juwa waliouwawa wengi wao walikuwa Watutsi
 
1. Genocide yenyewe haikuwa clear, ilikuwa imejificha ndani ya vita miaka minne kati ya RPF na serikali ya Habyarimana. Katika situation kama hiyo ni vigumu kujua kama kuna genocide inaendelea au ni yale yale mapigano ya kawaida. Kuingilia kati kwa Tanzania kungewezekana iwapo tu RPF wangebaki nje ya Rwanda, hapo ndipo tungepata moral authority ya kuingilia affairs za ndani ya Rwanda. kwani ingekuwa wazi kuwa serikali either inafanya genocide au imeshindwa kustopisha genocide.
2. Genocide ilifanywa na interahamwe sio jeshi la nchi. Interahamwe ingawa ni millitia (kama vile sungusungu if i'm correct) bado ni civilians. Jukumu la kusimamisha genocide against tutsis lilikuwa chini ya serikali ya habyarimana, na lingeweza kufanikiwa isipokuwa tayari walikuwa bize kupambana na RPF waliokuwa wanafanya mapinduzi at the same time.
3. Baada ya kugundulika kuwa kuna genocide, UN walitaka kuongeza vikosi ili kuzuia mauaji zaidi yasiendelee. Kwa mtu yoyote mwenye akili timamu, kuwapo kwa jeshi la watutsi la kagame linalopigana kupindua nchi ambayo majority ni wahutu LAZIMA ingeleta genocide kati ya wanajamii vs wanajamii kwani watutsi wangeonekana wao ni wasaliti. Cha ajabu Kagame sio tu alikataa bali alitishia kupambana na majeshi ya UN!! matokeo yake genocide against tutsis ikaendelea, na yeye akaendeleza mauaji dhidi ya wahutu ambayo mpaka leo hataki watu wakumbuke.
 
Kumbukumbu zangu zinaonesha kuwa mwaka 1994 wakati mauaji yakiendelea, tanzania ya mwinyi ikawa kimya kabisa. Mwalimu nyerere akawaita wanahabari pale msasani. Akaufungua ulimwengu macho. Akasema ni ajabu sana watu wamekaa kimya huku rwanda watu wakimalizana. Waandishi nao wakashangaa kusikia hivyo. Mwl akasema inashangaza kuona wauaji wanaachwa, lakini wanakemewa wale wanaouawa. Ndipo kuanzia hapo vyombo vya habari vya tanzania na kimataifa vikajua kinagaubaga kuwa rwanda kuna mauaji ya kimbari, na si ya halaiki. Kwa hiyo hapa nasema mwalimu nyerere, kama kiongozi mahiri aliyeijua afrika na dunia, alikuwa wa kwanza kuuamsha ulimwengu juu ya mauaji ya rwanda.kwa faida tu, rejeeni magazeti ya mwaka 1994 na 1995 mwanzoni. Asanteni.
 
Mkuu Manyerere Jackton ni kweli Mwl Nyerere aliwahi kulizungumzia hili jambo lakini wakati ule serekali ya Mzee Ruksa Mwinyi haikutaka kujiingiza sana iliamua kukaa kimya.Kuna habari kwamba serekali kupitia vyombo vyake vya habari hasa Redio Tanzania vilikatazwa kabisa kutokusema habari ya genocide iliyokuwa ikiendelea Rwanda.Nasikia waziri wa habari kama sikosei marehemu Wiliam Shija alimwagiza mkurugenzi wa radio Tanzania kuondoa habari ya Mwl Nyerere.

Kumbukumbu zangu zinaonesha kuwa mwaka 1994 wakati mauaji yakiendelea, tanzania ya mwinyi ikawa kimya kabisa. Mwalimu nyerere akawaita wanahabari pale msasani. Akaufungua ulimwengu macho. Akasema ni ajabu sana watu wamekaa kimya huku rwanda watu wakimalizana. Waandishi nao wakashangaa kusikia hivyo. Mwl akasema inashangaza kuona wauaji wanaachwa, lakini wanakemewa wale wanaouawa. Ndipo kuanzia hapo vyombo vya habari vya tanzania na kimataifa vikajua kinagaubaga kuwa rwanda kuna mauaji ya kimbari, na si ya halaiki. Kwa hiyo hapa nasema mwalimu nyerere, kama kiongozi mahiri aliyeijua afrika na dunia, alikuwa wa kwanza kuuamsha ulimwengu juu ya mauaji ya rwanda.kwa faida tu, rejeeni magazeti ya mwaka 1994 na 1995 mwanzoni. Asanteni.
 
Last edited by a moderator:
Hii vita ilihusisha nchi za magharibi kwa sana na uki connect dots utagundua baadhi ya viongozi wetu ambao hawakuwa majasiri walitii amri za kishetani za hawa wazungu
 
Wakulaumiwa ni wa-Tutsi waliovimbishwa kichwa na wabelgiji kwamba wao ni superior kuliko wa Hutu na wao wakaamini kichwa kichwa uongo huo na kuukumbatia na kuu-manifest katika maisha yao ya kila siku dhidi ya wahutu, it was inevitable. Cha msingi makosa yaliyopelekea kutokea Genocide yarekebishwe ili isije kutokea nyingine, ni mawazo yangu tu.
 
Kila nikikumbuka haya mauaji machozi yananilenga....najiuliza kwanini Tanzania haikufanya chochote na ikasubiri USA na nchi nyingine za maghalibi.

Am I missing something?Nakumbuka Primary school tulisoma kwamba in 1884 Otto von Bismarck, the first Chancellor of Germany aliweka kikao cha kuigawanya Africa kiliitwa Scramble for Africa, A.k.a the Race for Africa.Sasa kama tunajua tuligawanywa kwanini leo tunapokuwa tunabatatizo tunasubiri waliotugawanya waje kutusaidia?
Nyerere angekuwepo madarakani tungeingia Rwanda tena kimya kimya. Kinachoniumiza kichwa ni hili bomba la mafuta la Uganda. Je Waganda wakianzisha sabotage kwa M7, Tanzania tutaingia Uganda. Kumbuka pesa ya mafuta ni tamu.
 


Huwezi kulaumu nchi kama Tanzania kuwa tulishindwa kuzia Rwandan Genocide na kama unataka kujua nani wa kulaumiwa basi kwanza uanalyze kisha uevaluate the role of UN systems, in particular the Secretary-General, (SG) the Secretariat, the Security Council and the Member States of the organization, katika kipindi cha peacekeeping process.
Mindhali unataka shule basi naweza kukuelezea briefly katika mgawanyiko wa sehemu tatu kama kweli una nia ya taka kujua nani wa kulaumiwa na kwa nini alaumiwe1)Kwanza au sehemu ya kwanza lazima ujue kuwa huwezi kuzungumzia UN in Rwanda bila kuzungumzia jinsi gani walivyofeli in SOMALIA
2) Pili lazima ujue atleast lazima uanalyze an overview of the UN Peacekeeping operations in Rwanda na sehemu hii ndiyo itaweza kukuprovide with the basis for an evaluation of the UN peacekeeping role na katika analysis yako lazima ufocus in particular on inputs and outputs (to measure progress against plan and targets) of the UN, wakati evaluation itakuwa inaangukia katika outcome (yaani measuring objectives attainment and UN performance) and impact (assessing the effects of the peacekeeping process on the Rwandan people)
Sasa kwa kawaida haya mamabo ya peacekeeping operation mara nyingi huwa yanashuighulisha deployment ya primary military personnel kutoka nchi mbali mbali ambao watakuwa chini ya command ya jamaa wa Umoja wa mataifa ambao mainly kazi yao ni ku control and resolve armed conflict between hostile parties. in otherwords haya mambo ya Peacekeeping, initially yalikuwa developed as a means of dealing with inter-state conflict, lakini katika siku au miaka ya karibuni yamegeuza au yameanza kuwa applied katika intra-state conflicts and civil wars.
Mfano vita vya sikuhizi frequently vinatake place between multiple armed factions with different political objectives and fractured lines of command na tatizo au tuseme challenge kubwa hutokea pale wakati ambo conflicting parties fail to live up to their commitments and fighting resumes na katika case ya Rwanda ya 1994, unaweza ku argue kuwa UN peacekeepers found no peace to keep and were faced with the dilemmas of peacekeeping and the use of force.Kama nilivyosema hapo awali sitokaa hapa kumwaga dara kuuubwa lakini nitakuwa straight to the point:1) SOMALIA EFFECT:
Kikosi cha UNAMIR kilishindwa kuzuia mauaji ilitokana na failure by the UN system as a whole. Na fundamental failure unaweza ukaanalyze na ku evaluated based on several issues:-: UNAMIR kwanza iliundwa under the shadow of events in Somalia can be argued as a possible factor for failure.Sijui umri wako uliwa vipi lakini nakumbuka nilikuwa naenda kutazama ABC NEWS pale USIS Dar na walikuwa wanaonyesha miili ya US Marines ilkiburizwa Mogadishu na ile ilikuwa ni failure ya UNSCOM 1 pamoja na US led OPERATION RESTORE HOPE na mwishowe nadhani unajua waliishia kumtafuta MF.AIDID na ile ilikuwa ni strategic failure toka kwa Pentagon na nikiianza kukuelezea jinsi gani walivyofeli wale palnners kule Pentagon tutakuwa hatulali kwani lile ni somo linalojitegemea la STRATEGIC STUDIES lakini naweza kukuambia kuwa for US Government the events in Mogadishu were a watershed in its policy towards UN peacekeeping.2) LACK OF POLITICAL WILL
Unaweza kusema kuwa hii sisi kama watanzania tulichangia lakini the truth is sisi tuliact UNILATERARY mara moja tu tulipovamiwa na IDDI AMIN (?) in 1970's. Japo lawama nyingi zilielekezwa kwa UNAMIR kule RWANDA lakini tusisahau kuwa jamaa walikuwa hawana vifaa vya kufanyia kazi zao na of course tusisahau reresponsibility of UN Member States ambao kusema kweli hawakuonyesha nia ya kupeleka majeshi wao huko RWANDA at that time. Na Genocide ilipochachamaa baadhi ya nchi za Africa zilioffer lupeleka majeshi kwa masharti kuwa wapewe AMOUR PERSONELL CARRIERS lakini guess what? CLINTON ADMINISTRATION walikubali lakini kwa sharti wapewe $15 million!
-: WABELGIJI
nao walitishia kuondoka na UNSG bwana Ghali aliwabembeleza wabakishe silaha zao kwa ajili ya UNAMIR lakini wapi jamaa waliamua kurudi kwao na silaha zao-: Vile vile RWANDA haikuwa of any strategic interest to the international community, especially the USA, sasa ndio maana USA waliamua kuexcercise CAUTION considering yaliyowakuta Mogadishu

3)LACK OF ANALYTICAL CAPACITY
Mzee kama unasomea mambo ya strategic studies lazima uelewe kuwa a critical analysis of the nature of the conflict will contribute to conceptualizing a comprehensive peacekeeping action. in short kama uko effective katika kuhandle peace process then lazima ujue kuwa it depends on accurate political analysis of the conflict lakini ukiangalia kwa makini utagundua kuwa jamaa wa UNAMIR pamoja na UN Headquarters however, walikuwa wahawana analysis ya Rwandan political situation na hii ilipelekea kwa UNAMIR kufeli kuwalinda viongozi wa kusiasa, raia na UN STAFF OF COURSE MATOKEO YAKE YAKAWA NI UMWAGIKAJI WA DAMU. hawajamaa wa UNAMIR walitakiwa kuwalinda moderate politicians ambao walikuwa wako tayari kutekeleza yale waliyoyakubali kwenye ARUSHA AGREEMENT (I) lakini wapi jamaa walikula mapanga yaliyokuwa yakiongozwa na propaganda toka kwa redio za akina HASSAN NGEZI na akina JEAN BOSCO BRYRAGWIZA4)LACK OF UNITY OF COMMAND
Huwezi kuamini kuwa wakati wanachi wa Rwanda walikuwa wanchinjana kama kuku UNAMIR walikuwa hawana unity of command Another failure was the lack of unity command.HUWEZI UKAWA NA PEACEKEEPING OPERATION YA MAANA BILA HILO maajabu ni kuwa kila CONTIGENT iliyokuwa RWANDA ilikuwa inafanya kazi kivyake! na kila kikosi kilikuwa kinafuata amri toka country of origin kwa kufuata their own national agendas sasa niambie hapo kuna cha peace keeping au vichekesho?5) CONFUSION OF CHAIN OF COMMAND


hii inahusian kidogo na hiyo point ya juu lakini naweza kukuambia kuwa GENERAL DALLIARE aliomba wanajeshi 5000 lakini waheshimiwa kule NEWYORK wakampa nusu ya hiyo ili asitishe ile genocide ya watu milioni moja! mzee hapa naweza kukuelezea kwa kirefu tuu kuhusu ile FAX iliyotumwa iliyokuwa inaelezea jinsi mauaji ya watusi yangeanza lakini kule UN watu waliipata na of course kulikuwa na wahutu wengine waliamua kuificha lakini inshort GENERAL DALLIERE alituma mpaka CABLE kule lakini wapi! ndio maana mimi leo mtu aniambie nikafanye kazi field huko DARFUR siwezi kukubali kwani najua urasimu wa UN unaweza ukakucost maisha hivi hivi
nadhani hapo umenipata na based on above arguments ni makosa kutulaumu sisi watanzania kwa kushidwa kuzia yale mauaji ilihali sisi tulishaplay a very crucial ROLE yetu kwa kugharamia ile mikutano ya ARUSHA 1 & 2


kama kuna mtu anataka kujua zaidi basi ingia hapa kama unataka kuachana na simplistic replies na kutaka kujua what went wrong in Rwanda an failures zilikuwa ni za nani:

United Nations An Evolving Technique: http://www.un.org/Depts/dpko/intro/1.htm

United Nations Peacekeeping: Some questions and answers: http://www.un.org/Depts/dpko/dpko/ques.htm

United Nations Report of the Independent Inquiry into the Actions of the United Nations in the Rwandan Genocide: http://www.un.org/News/ossg/rwanda_report.htm


Exactly
 
Nyerere angekuwepo madarakani tungeingia Rwanda tena kimya kimya. Kinachoniumiza kichwa ni hili bomba la mafuta la Uganda. Je Waganda wakianzisha sabotage kwa M7, Tanzania tutaingia Uganda. Kumbuka pesa ya mafuta ni tamu.
Unataka kusema kwamba M7 ametupa hili bomba kama mlungula ili tumlinde?
 
Back
Top Bottom