Could Tanzanian Gov. stop 1994 Rwandan genocide?

mstahiki

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
308
5
Kila nikikumbuka haya mauaji machozi yananilenga....najiuliza kwanini Tanzania haikufanya chochote na ikasubiri USA na nchi nyingine za maghalibi.

Am I missing something?Nakumbuka Primary school tulisoma kwamba in 1884 Otto von Bismarck, the first Chancellor of Germany aliweka kikao cha kuigawanya Africa kiliitwa Scramble for Africa, A.k.a the Race for Africa.Sasa kama tunajua tuligawanywa kwanini leo tunapokuwa tunabatatizo tunasubiri waliotugawanya waje kutusaidia?
 

Maneno ya Mwalimu----alipohojiwa na CHARLAYNE HUNTER-GAULT wa PBS


=================================================================
JULIUS NYERERE: When we have African problems, we, ourselves, have a duty to solve our problems. I think we must accept that. When you have African problems, we should try on our own to solve those problems. We would prefer the outside world to keep out. If we want help, we can seek for help. But do you realize sometimes we ask for help, and it doesn't come. On the 5th of last month our leaders met in Nairobi, and if said need an external--we need a force to go into Zaire to help the refugees to come back. It's not happening. And we appealed to the United Nations to establish that force, and we said we would also be participating in that force. Well, quite frankly, this is not happening. What is happening is a kind of self-help within Eastern Zaire, itself. And the refugees are going back. I hope--I think the lesson which Africa should draw from that is that they should rely upon themselves to the maximum when it comes to dealing with African problems.
 
Kila nikikumbuka haya mauaji machozi yananilenga....najiuliza kwanini Tanzania haikufanya chochote na ikasubiri USA na nchi nyingine za maghalibi.

Am I missing something?Nakumbuka Primary school tulisoma kwamba in 1884 Otto von Bismarck, the first Chancellor of Germany aliweka kikao cha kuigawanya Africa kiliitwa Scramble for Africa, A.k.a the Race for Africa.Sasa kama tunajua tuligawanywa kwanini leo tunapokuwa tunabatatizo tunasubiri waliotugawanya waje kutusaidia?

good thread
Ni magharibi na siyo maghalibi

Simple answer to your question is NO! na kama unataka nikupe shule kuhusu nani wa kulaumiwa then letme know lakini uwe na kifua cha kusubiri na kudigest mijidata

uko tayari?
 

good thread
Ni magharibi na siyo maghalibi

Simple answer to your question is NO! na kama unataka nikupe shule kuhusu nani wa kulaumiwa then letme know lakini uwe na kifua cha kusubiri na kudigest mijidata

uko tayari?

I was born READY
Nimeshika PEN na Karatasi nasubiri kipindi..
 
I was born READY
Nimeshika PEN na Karatasi nasubiri kipindi..


Huwezi kulaumu nchi kama Tanzania kuwa tulishindwa kuzia Rwandan Genocide na kama unataka kujua nani wa kulaumiwa basi kwanza uanalyze kisha uevaluate the role of UN systems, in particular the Secretary-General, (SG) the Secretariat, the Security Council and the Member States of the organization, katika kipindi cha peacekeeping process.
Mindhali unataka shule basi naweza kukuelezea briefly katika mgawanyiko wa sehemu tatu kama kweli una nia ya taka kujua nani wa kulaumiwa na kwa nini alaumiwe1)Kwanza au sehemu ya kwanza lazima ujue kuwa huwezi kuzungumzia UN in Rwanda bila kuzungumzia jinsi gani walivyofeli in SOMALIA
2) Pili lazima ujue atleast lazima uanalyze an overview of the UN Peacekeeping operations in Rwanda na sehemu hii ndiyo itaweza kukuprovide with the basis for an evaluation of the UN peacekeeping role na katika analysis yako lazima ufocus in particular on inputs and outputs (to measure progress against plan and targets) of the UN, wakati evaluation itakuwa inaangukia katika outcome (yaani measuring objectives attainment and UN performance) and impact (assessing the effects of the peacekeeping process on the Rwandan people)
Sasa kwa kawaida haya mamabo ya peacekeeping operation mara nyingi huwa yanashuighulisha deployment ya primary military personnel kutoka nchi mbali mbali ambao watakuwa chini ya command ya jamaa wa Umoja wa mataifa ambao mainly kazi yao ni ku control and resolve armed conflict between hostile parties. in otherwords haya mambo ya Peacekeeping, initially yalikuwa developed as a means of dealing with inter-state conflict, lakini katika siku au miaka ya karibuni yamegeuza au yameanza kuwa applied katika intra-state conflicts and civil wars.
Mfano vita vya sikuhizi frequently vinatake place between multiple armed factions with different political objectives and fractured lines of command na tatizo au tuseme challenge kubwa hutokea pale wakati ambo conflicting parties fail to live up to their commitments and fighting resumes na katika case ya Rwanda ya 1994, unaweza ku argue kuwa UN peacekeepers found no peace to keep and were faced with the dilemmas of peacekeeping and the use of force.Kama nilivyosema hapo awali sitokaa hapa kumwaga dara kuuubwa lakini nitakuwa straight to the point:1) SOMALIA EFFECT:
Kikosi cha UNAMIR kilishindwa kuzuia mauaji ilitokana na failure by the UN system as a whole. Na fundamental failure unaweza ukaanalyze na ku evaluated based on several issues:-: UNAMIR kwanza iliundwa under the shadow of events in Somalia can be argued as a possible factor for failure.Sijui umri wako uliwa vipi lakini nakumbuka nilikuwa naenda kutazama ABC NEWS pale USIS Dar na walikuwa wanaonyesha miili ya US Marines ilkiburizwa Mogadishu na ile ilikuwa ni failure ya UNSCOM 1 pamoja na US led OPERATION RESTORE HOPE na mwishowe nadhani unajua waliishia kumtafuta MF.AIDID na ile ilikuwa ni strategic failure toka kwa Pentagon na nikiianza kukuelezea jinsi gani walivyofeli wale palnners kule Pentagon tutakuwa hatulali kwani lile ni somo linalojitegemea la STRATEGIC STUDIES lakini naweza kukuambia kuwa for US Government the events in Mogadishu were a watershed in its policy towards UN peacekeeping.2) LACK OF POLITICAL WILL
Unaweza kusema kuwa hii sisi kama watanzania tulichangia lakini the truth is sisi tuliact UNILATERARY mara moja tu tulipovamiwa na IDDI AMIN (?) in 1970's. Japo lawama nyingi zilielekezwa kwa UNAMIR kule RWANDA lakini tusisahau kuwa jamaa walikuwa hawana vifaa vya kufanyia kazi zao na of course tusisahau reresponsibility of UN Member States ambao kusema kweli hawakuonyesha nia ya kupeleka majeshi wao huko RWANDA at that time. Na Genocide ilipochachamaa baadhi ya nchi za Africa zilioffer lupeleka majeshi kwa masharti kuwa wapewe AMOUR PERSONELL CARRIERS lakini guess what? CLINTON ADMINISTRATION walikubali lakini kwa sharti wapewe $15 million!
-: WABELGIJI
nao walitishia kuondoka na UNSG bwana Ghali aliwabembeleza wabakishe silaha zao kwa ajili ya UNAMIR lakini wapi jamaa waliamua kurudi kwao na silaha zao-: Vile vile RWANDA haikuwa of any strategic interest to the international community, especially the USA, sasa ndio maana USA waliamua kuexcercise CAUTION considering yaliyowakuta Mogadishu

3)LACK OF ANALYTICAL CAPACITY
Mzee kama unasomea mambo ya strategic studies lazima uelewe kuwa a critical analysis of the nature of the conflict will contribute to conceptualizing a comprehensive peacekeeping action. in short kama uko effective katika kuhandle peace process then lazima ujue kuwa it depends on accurate political analysis of the conflict lakini ukiangalia kwa makini utagundua kuwa jamaa wa UNAMIR pamoja na UN Headquarters however, walikuwa wahawana analysis ya Rwandan political situation na hii ilipelekea kwa UNAMIR kufeli kuwalinda viongozi wa kusiasa, raia na UN STAFF OF COURSE MATOKEO YAKE YAKAWA NI UMWAGIKAJI WA DAMU. hawajamaa wa UNAMIR walitakiwa kuwalinda moderate politicians ambao walikuwa wako tayari kutekeleza yale waliyoyakubali kwenye ARUSHA AGREEMENT (I) lakini wapi jamaa walikula mapanga yaliyokuwa yakiongozwa na propaganda toka kwa redio za akina HASSAN NGEZI na akina JEAN BOSCO BRYRAGWIZA4)LACK OF UNITY OF COMMAND
Huwezi kuamini kuwa wakati wanachi wa Rwanda walikuwa wanchinjana kama kuku UNAMIR walikuwa hawana unity of command Another failure was the lack of unity command.HUWEZI UKAWA NA PEACEKEEPING OPERATION YA MAANA BILA HILO maajabu ni kuwa kila CONTIGENT iliyokuwa RWANDA ilikuwa inafanya kazi kivyake! na kila kikosi kilikuwa kinafuata amri toka country of origin kwa kufuata their own national agendas sasa niambie hapo kuna cha peace keeping au vichekesho?5) CONFUSION OF CHAIN OF COMMAND


hii inahusian kidogo na hiyo point ya juu lakini naweza kukuambia kuwa GENERAL DALLIARE aliomba wanajeshi 5000 lakini waheshimiwa kule NEWYORK wakampa nusu ya hiyo ili asitishe ile genocide ya watu milioni moja! mzee hapa naweza kukuelezea kwa kirefu tuu kuhusu ile FAX iliyotumwa iliyokuwa inaelezea jinsi mauaji ya watusi yangeanza lakini kule UN watu waliipata na of course kulikuwa na wahutu wengine waliamua kuificha lakini inshort GENERAL DALLIERE alituma mpaka CABLE kule lakini wapi! ndio maana mimi leo mtu aniambie nikafanye kazi field huko DARFUR siwezi kukubali kwani najua urasimu wa UN unaweza ukakucost maisha hivi hivi
nadhani hapo umenipata na based on above arguments ni makosa kutulaumu sisi watanzania kwa kushidwa kuzia yale mauaji ilihali sisi tulishaplay a very crucial ROLE yetu kwa kugharamia ile mikutano ya ARUSHA 1 & 2


kama kuna mtu anataka kujua zaidi basi ingia hapa kama unataka kuachana na simplistic replies na kutaka kujua what went wrong in Rwanda an failures zilikuwa ni za nani:

United Nations An Evolving Technique: http://www.un.org/Depts/dpko/intro/1.htm

United Nations Peacekeeping: Some questions and answers: http://www.un.org/Depts/dpko/dpko/ques.htm

United Nations Report of the Independent Inquiry into the Actions of the United Nations in the Rwandan Genocide: http://www.un.org/News/ossg/rwanda_report.htm


 
Kuna sababu nyingi, ni vigumu kuzitaja zote hapa. Lakini naweza kusema kuwa Tanzania ya Nyerere ambao ilikuwa tayari kubeba mzigo wa uchumi kwa ajili ya wengine, ni tofauti kabisa na Tanzania ya Mwinyi ambayo kwanza ilikuwa shatterd na haikuwa na vision kama hiyo.
Kulikuwa na lesson vilevile, what did we get from our involvement in Msumbuji, Zimbabwe, Uganda.....hatukupata lolote lile la maana, zaidi ya kulose kiuchumi. Hata hivyo contribution ya Rwanda kiuchumi kwa Tanzania ni very minimal kwa hiyo kuchujnana kwao hakukuwa na impact kubwa sana kwa Tanzania, ndiyo maana waliamua kukaa na kusubiri kitokee kinachotokea, na kukubali matokeo.
 
Lakini sababu nyingine kulikuwa na Grand Tutsi movement ambayo ilikuwa inaendelea, na kulikuwa na long term goal ya kumuondoa Mobutu madarakani baada ya Kagame kuingia Kigali. Inaonekana kulikuwa na miscalculation ya outcome ya kuondoka kwa utawala wa Habyarimana, waliokuwa wakipiga hesabu walijua baada ya Habyarimana kuondolewa madarakani, Kagame anaweza kuingia kiulaini Kigali na baadaye kuweka base ya kudeal na Mobutu( which he did), lakini bahati mbaya haikuwa rahisi hivyo.
Kama Tanzania ingeingilia hiyo plan huenda ingekuwa haina maana yoyote, kwanza kiuchumi tulikuwa hoi zaidi kuliko tulivyosasa, na huenda tungeharibu whole plan ya kumshughulikia Mobutu!
 
Has anybody seen "The Devil Came On Horseback"? Inaonyesha jinsi mjeshi wa kimarekani alivyopelekwa ku "observe the peace" in Sudan bila mandate ya kutumia force, ikabidi jamaa aishie kufilm documentary.

What is Africa doing?
 
Mwanaharakati ameuliza a straightforward question: kwanini Tanzania haikufanya chochote kuzuia mauaji yale ya Rwanda 1994?

Hizi habari za sijui UN, US, Pentagon, UNAMIR na sijui nani kafanya hivi na vile zinatokea wapi jamani? Mimi naona tunajitafutia visingizio tu... tukubali tu kuwa tuliona kujiingiza huko Rwanda hakuna maslahi (si kwa nchi yetu wala kwa viongozi wetu), mbona Idi Amini tulimuandama mpaka Kampala tukamtoa. Gadafi alipopeleka msaada kwa Idi Amin tukawapa kichapo vilevile hatukusubiri cha UN, US, UNAMIR wala nini... kujificha nyuma ya Strategic studies rahisi sana.
 
Somo la GT ni zuri lakini liko tu theorectical for a normal person to comprehend. Kwenye swala la Rwanda kuna conspiracy theories nyingi sana, but what I can say is:

1. Mwanaharakati, kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba, Rwanda haikuwa na maslahi kwetu na Tanzania yetu and by then we were very much in bed with Habyarimana administration! Kwa kifupi ni kwamba Mwinyi na Malecela, Malecela ndiyo as a PM! walikuwa ni strong supporters wa Habyarimana na Kagame alikuwa anaonekana kama kijana mtukutu tuu, kwa hiyo sisi kama taifa tayari tulikuwa tumeshatake side indirectly. Ingawa Nyerere alikuwa symphathiser wa Kagame na RPF-big time! Na ndiye alikuwa wa kwanza kuwatambua walipoingia Kigali hata kabla ya Serikali ya mwinyi kutoa tamko! (hii inatukumbusha kwamba ki-policy Nyerere na Samweli walidiffer kwa mambo mengi)

2. UN is a very strange organization, lakini kifupi, kulikuwa na camp mbili na UN ilijua fika kabisa kwamba Genocide was more likely to happen, lakini kulikuwa na VERY STRONG influence ya Ufaransa aliyekuwa in bed na utawala wa Habyarimana, kwa hiyo hata the rest of the Permanent members walikuwa wanamtegemea France saana (infact naambiwa kwamba kwenye briefing za UN kila siku, Kuna vitu vingi SG Boutros Ghali aliwa anadanganya on instructions from France na kumbuka Ghali utawala wake ulikuwa unategemea France big time, na this was one of the reason hakupewa second term baada ya kuona France ilivyomtumia kwenye hili saga la Rwanda...) na alipitisha amri kwamba anything to do with Rwanda or any statement kabla haijatolewa kwenye media or to any body lazima ipite kwenye meza yake! Kifupi kulikuwa na complacent ya Ufaransa big time. Members wengi were kept in the dark about the situation in Rwanda.

3. Nakubaliana na GT Somalia effect iliwademolorize waamerika, lakini usisahahu ilikuwa ni kulindana kati ya mataifa makubwa, Other P5 members walijua fika kwamba hii issue ni ya Ufaransa kama colonial master! kwa hiyo walimuachia yeye na kwa sababu France alikuwa anamlinda Habyarimana, basi alipata alichokitaka, namely non interference ya mataifa mengine.

Harafu usisahahu Balkan effect, US na most of Europe walikuwa occupied na Issue ya Balkan unaambiwa by then Ambassodor wa US pale UN Albright briefing zake kwa Secretary Warren Christopher ilikuwa ni kuhusu Balkan na Africa ilikuwa haimo kabisa kwa sababu it was assumed (sometime kwa kudanganywa na Ufaransa) kwamba all is well and will be handled by France. Though again US had no pushing factors to intervene in Rwanda.

4. Generally the so called Peace keeping is just a political gimmic au naiweza kuiita minimalist approach ya hawa watu wa magharibi! wanaposhindwa kutatua migogoro ambayo wameianzisha wenyewe sometimes. UN haina polisi au askari wala pesa! wanategemea hawa wazee watoe vyote hivyo, sasa usitegemee US au Ufaransa kutoa askari wake pale ambapo hawana maslahi. Rwanda haikuwa one of them. Chukulia Darfur tangu Koffi Annan aanze kushuttle kwenda kumuomba Bashir aruhusu hao peace keepers ni lini? mpaka amestaafu hao askari hatujawaona Darfur! kila siku envoys wanateuliwa kwenye peace mission za Darfur na kuondoka but we hardly see anything! Kwa hiyo sometimes (as Mseven rightly puts it, peacekeeping ni nonsense phenomena developed by the west kuabdicate their responsibilities)

5. Je Africa as whole tulikuwa wapi? yes, tulikuwa tunaangalia wakati wenzetu wanachinjana, kwa sababu hatukuwa na political will ya kuingia Rwanda, tayari kulikuwa na negative propaganda dhidi ya Tutsi movement kwamba wanataka kutawala na kila mtu aliona amwachie Habyarimana kwani ndivyo alitaka! Lakini kikubwa Kagame hakuwa na symphathiser apart from KAGUTA na mzee Nyerere!

Its very sad, but what I see Kagame is consistently proving wrong his detractors and critics. France tried to use all its mighty to smear Kagame and his administration, but the man is proving formidable. Swala la kujiuliza mauaji kama haya yanaweza kutokea? I would say big time! yanatokea especially kwa sababu kama Waafrica hatujajifunza, bado tunakubali kugawanywa na wenye interests zao. Congo, Somalia, Chad, Sudan ni mifano michache. Na unfortunately uwezo wetu kiuchumi ni mdogo sana (juzi ilikuwa ni aibu kuona Burundi haina uwezo wa kupeleka askari wake mia moja tuu pale Somalia, walikuwa wakihaha kutafuta helicopter!!) the situation is similar to other African countries who want to do something badala ya kuwategemea waungwana wa magharibi...

Kwa hiyo mimi kwa swala la Rwanda naona kwamba waafrica na watanzania hatukuingilia kati kwa sababu tulikuwa over negatively indoctrinated na madhambi ya watutsi. Mpaka leo watutsi wanaonekana kama expansionist na wanaopenda kutawala at the expense ya wengine...on and on....you can go....Tulikuwa sahihi au hatukuwa sahihi? The jury is still out na historia itatuhukumu!
 
Mwakilishi
NI kweli hakukuwa na maslahi yoyote, labda kama tungekuwa na sababu tungesingizia humanitarian interest. Kuna Phrase moja wanatumia wamarekani inanifurahisha sana, "you are damn if you do you, are damn if you don't" hapo ndipo tulipofikia Tanzania. Kwa hiyo hatukuwa na sababu yoyote ya kutafuta sifa kwa kutumia pesa na kuhatarisha maisha ya askari wetu.
Ile ya Uganda mimi siwezi kusema sana kwa sababu nilikuwa bado mdogo sikujua yaliyotokea, lakini hata hivyo nadhani ulikuwa ni ujinga tu, tusingemchokoza nduli kwa kum-host Obote yasingetokea yaliyotokea, au tusiruhusu ardhi yetu itumike kuisimbua Uganda yote yale yasingetukuta, labda hii ni issue tofauti.
 
Hope Masanja you do not mean that actually 'we are not normal persons'!

Kwi kwi kwi!!!

Tafadhali mkuu! bila kuathiri maana ya mchango wa GT..... nimeona GT ametoa shule kubwa saana ambayo inahitaji mtu kuingia deep sana kwenye hizi modus operand za UN!
 
Kila nikikumbuka haya mauaji machozi yananilenga....najiuliza kwanini Tanzania haikufanya chochote na ikasubiri USA na nchi nyingine za magharibi.

Am I missing something? Nakumbuka Primary school tulisoma kwamba in 1884 Otto von Bismarck, the first Chancellor of Germany aliweka kikao cha kuigawanya Africa kiliitwa Scramble for Africa, A.k.a the Race for Africa.Sasa kama tunajua tuligawanywa kwanini leo tunapokuwa tunabatatizo tunasubiri waliotugawanya waje kutusaidia?

Tanzania imefanya mengi katika kusaidia nchi jirani na kuwawezesha kupata uhuru wao au kupata hifadhi ya ukimbizi n.k. Kutokana na kuwabebesha watanzania mzigo huu ambao ni mkubwa Tanzania ilikuwa inaelekeza rasilimali zake katika maswala kama haya kwa muda mrefu na matokeo yake tumekuwa kichekesho kwa nchi majirani zetu ambao wanatucheka kwamba sisi si chochote kwa sababu uchumi wetu uliathirika sana na kuelekeza juhudi kwenye kuikomboa Afrika. Rejea jinsi SADC ilivyoanza na kwisha kwa vita baridi.

Matatizo ya Congo, Somalia na hata kwa kiasi fulani Malawi na Kenya kutokuwa na uhusiano wa karibu kuliko nchi za SADC ni moja katika harakati hizo, bila kusahau jinsi USA walivyoingilia swala la Somalia kwa nguvu zote katika kumiliki njia za kiuchumi katika ghuba.

Matatizo ya Rwanda anayeweza kulaumiwa moja kwa moja ni M7 ambaye ndiye alikuwa catalyst na Tanzania walikuwa wanalielewa hilo na jinsi M7 alivyokuwa katika mstari wa mbele kwenye swala hilo ingawaje hivi sasa anataka kujiweka mbali na tuhuma hizo. Tanzania ilikuwa haina resource za kutosha na ilikuwa sio jambo jema kuingilia kwa undani ukichukulia kwamba baada ya Mwalimu kustaafu ilikuwa ni open kwamba tusijihusishe na maswala ambayo sio yetu na tujaribu kuweka uchumi wetu katika hali nzuri na kuacha wengine washughulikie matatizo ya watu wengine. Ndio sababu kuna warundi wengi ambao hivi karibuni wamekuwa wanapelekwa marekani kwani sisi sio mama wa Afrika yote.

Tukomalie kwenye maswala yetu na yasiyo yetu wenye ubavu wayavalie njuga. We have done enough.
 
Dua you mean kwamba Tanzania hatujaendelea kiuchumi kwa sababu tulitumia raslimali zetu kuwakomboa wengine especially majirani? kama Zimbabwe, Uganda, SA nk? Or Iam missing a point?

Harafu nadhani WITH DUE RESPECT approach yako kwenye foreign policy yetu ni very minimalist! Mzee hakuna anayeishi kisiwani ati! Huwezi kusema eti Tanzania tuliamua kumuachia Mseveni kwa sababu tulitaka kurekebisha uchumi wetu? upi huo? Comrade labda ufafanue zaidi, leo Membe akiadopt mawazo yako, our foreign policy will be a TRAGEDY! Ohh I hope it is not-yet! Otherwise from your comments naona ni ile ile usual over negative indoctrination ya watutsi katika ukanda wa maziwa makuu!

Mkuu whether we like it or not, Rwanda and Burundi are our NEIGHBOURS so is Malawi, Kenya, Uganda, DRC etc we have to live with them na tupendane, na step ya kwanza ni kuwaleta kwenye East Africa Community! Tunaweza tusipende na kulaumu waliofanya huo uamuzi, lakini the bigger picture is umaskini ndo unasababisha yote haya. Leo Kagame kaondoa work permit kwa mtu yeyote anayetoka East Africa anayetaka kufanya kazi Rwanda.....Hiyo ni challenge, harafu tukiona jamaa wanaendelea ndo hapo tunaanza protectionism! My Compatriots Tanzanians TUAMKE tuache visingizio. We either compete or compete! kuwapiga vita haitasaidia chochote! Ndo maana mi nasema kila mara, hii sumu tuliyomwagiwa dhidi ya watutsi ni mbaya sana! Alot needs to be done by us.
 
Hata mimi naona maelezo ya GT ni very complex. Bila kuzama ktk geopolitics kwa sababu sio fani yangu, naomba kueleza yafuatayo.

1.Tanzania ilikuwa ikiunga mkono utekelezwaji wa makubaliano ya amani ya Arusha. Kama Habyarimana aliamua kusaini makubaliano hayo basi tulikuwa na sababu zote za kumuunga mkono.

2.Kama Tanzania hatukumpenda Kagame, au RPF, ni kwasababu ya kutukukubaliana kwao na mkataba wa amani wa Arusha.

3.Kifo cha Habyarimana kinaelezewa na theories mbili. Ya kwanza inadai aliuwawa na Hutu extrimists ambao walikuwa hawakubaliani na Arusha accords. Ya pili, inadai aliuawa na RPF kwasababu all along hawa walikuwa hawataki ku-share madaraka na Wahutu. Kuna uwezekano basi Habyarimana alikuwa moderate.

4.Majirani ya Rwanda ni Tanzania,Uganda,Burundi, na Zaire. Sasa Uganda alikuwa tayari imechukua upande. Burundi ilikuwa ni sehemu ya tatizo, na Zaire ilikuwa imedhoofika. Naamini kwamba toka mwanzo Tanzania iliamua kwamba haitajiingiza kijeshi Rwanda na ndiyo maana ika-facilitate mazungumzo ya amani Arusha.

5.Kagame is hiding under internationals community guilty of in-action during rwandan genocide. Kagame na RPF wanahusika na mauaji ya kikatili na uporaji wa mali uliotokea na unaoendelea DRC.

6.Kagame amefanikiwa kuwa-label Wahutu wote kama "genocideire." Katika mazingira hayo hakuna nchi iliyoko tayari kuwatetea Wahutu kwa jambo lolote lile.

7.Hebu tujiulize Kagame anapataje ushindi wa tsunami ktk chaguzi za Rwanda? Ninavyoelewa mimi Wahutu bado ni majority Rwanda. Je, wameanza lini kumpenda Kagame kiasi hicho?

8.Habari ya Kagame kuondoa "vibali vya kazi" kwa raia wa Afrika Mashariki is just a gimmick. Mimi ningemchukulia seriously kama angesema anaruhusu wamachinga wa Tanzania kwenda kuendesha shughuli zao Rwanda.
 
8.Habari ya Kagame kuondoa "vibali vya kazi" kwa raia wa Afrika Mashariki is just a gimmick. [COLOR="Black" said:
Mimi ningemchukulia seriously kama angesema anaruhusu wamachinga wa Tanzania kwenda kuendesha shughuli zao Rwanda.Ohhh just thinking loud!!!!

Happy New Year!
 
Hivi clause ya OAU kuhusu non-interference inasemaje? Nafikiri kimsingi ilichangia mataifa mengine kuingilia bila kufuata a lot of red tape.Ndiyo maana Tanzania ikaweka effort katika mazungumzo.
 
Back
Top Bottom