Mtu_Mzima
JF-Expert Member
- Oct 1, 2014
- 1,174
- 1,150
Nimelifuatilia gonjwa hili, dalili na nini kifanyike.
Kwa upande wa tahadhari hapo naona serikali, taasisi zake, mashirika binafsi na watu kwa ujumla hawajafanya vya kutosha. Hebu tuangalie maisha yetu ya kawaida yalivyo hatarini.
1. MAOFISINI.
Mtu ungetegemea uone tahadhari za kueleweka haswa kwenye maofisi yanayotoa huduma kama mabenki, posta, TRA, mamlaka za maji nk. Ofisi ziwe na mask kwa ajili ya wateja waliokuja bila mask kuepuka mtu kukukoholea. Alcohol rub milangoni, vyooni na kwa wafanya usafi nk. Gloves kwa watu wa masjala wanaopokea mafaili kutoka nje nk.
2. MIKUSANYIKO.
Mikusanyiko ya kijamii kama harusi, send off, misiba nk bado haijawekewa utaratibu na mamlaka husika.
3. NYUMBA ZA IBADA
Huku nako hakuna utaratibu uliokubalika kati ya mamlaka za afya na nyumba za ibada.
4. VYOMBO VYA USAFIRI
Vyombo vya usafiri kama mabasi, treni, fery, ndege, meli na majahazi havijapewa utaratibu wowote wa kujihami.Fikiri mwendo kasi na daladala zinavyojaza na zile chuma za kujishikilia. Haswa ile ya pale mlangoni.
5. VYOO VYA UMMA
Mara nyingi usafi kwenye maeneo haya hauridhishi kwa hali ya kawaida. Je, kipindi hiki cha hatari ni tahadhari gani zimechukuliwa kuimarisha ukaguzi wa usafi?
6. MASHULENI NA VYUONI
Hali ya mikusanyiko kama hii mpaka leo hakuna tahadhari, wala elimu stahiki imetolewa kulinda afya za watoto na vijana wetu.
7. MIHADHARA
Tufike mahali mikutano na mihadhara itolewe kauli ya kusitishwa mpaka hali ya ugonjwa kidunia itulie.
8. WAGENI TOKA NJE YA NCHI
Kuna watu sijui wanatumia akili gani. Inakuwaje sisi tupokee wageni kwenye nchi zenye wagonjwa wengi kama china na nyinge za ulaya na marekani?
Tuseme, wageni toka nchi hizi wasipewe viza ya Tanzania. Basi.
Watalii, tungezidisha umakini na watu hawa maana tusiangalie pesa tukaeaangamiza watu wetu.
9. MALLS
Malls kama za mlimani city zingepaswa kuwa na mahali pa kunawa mikono kabla ya kuingia ndani na kila siku ifungwe mapema kuruhusu fumigation.
10. MICHEZO NA MATAMASHA YA MUZIKI
Hivi vingelipigwa marufuku kwa sasa. Tusisubiri shida ndio tuanze kuhangaika.
11. KUACHA BAADHI YA TAMADUNI
Zipo tamaduni za kuchangia vitu kama kule kwenye sinia, kunywa kahawa, tangawizi na alkasusu ( ambapo yale maji ya kuosha kikombe hayana uhakika) nk.
12. MAHOSPITALINI
Wagonjwa wengi ni waongo kwa kuogopa kutengwa hivyo kuwaweka watoa huduma kwenye hatari ya maambukizi. Je, tunawakingaje watoa huduma wetu?
13. MNAOENDA KWA WAGANGA
Sijui ya huko ila pima kwa makini mselekezo yao[emoji2][emoji2]
Ongeza na la kwako tujadili maana madhara ni yetu wote.
Sent using Jamii Forums mobile app