Corona inatuchana makavu live: Vipi wanasiasa na matajiri wako tayari kuuopkea huu ukweli mchungu?

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,487
2,344
1. Tabia ya serikali na wanasiasa kujisifu pale tunapokuwa na ka akiba (reserve) kakutuwezesha kutumia kwa miezi mitatu. Corona inatuambia tunajidanganya, tunajifariji kwa maneno matupu, ikiamua kutukazia kwa miezi 3 nchi inafirisika, inatushauri kukazana kuchapa kazi ili tuwe na akiba ya miaka kadhaa mbele ili kuwa salama.

2. Ni kawaida ya wanasiasa na wenye fedha kukimbilia kutibiwa au kuchekiwa afya zao nje ya nchi ila kwa sasa corona ni kikwazo maana nchi zile wanazozikimbiliaga hazipokei wageni hivyo wote tutatibiwa hapa hapa nchini, kama ni kufa tutakufa pamoja.

Corona inashauri, hao matajiri wawekeze kwenye sekta ya afya, na serikali iangalie namna ya koboresha sekta ya afya ili na hao viongozi watibiwe hapahapa maana hata sisi tusio na uwezo tunatamani hizo huduma zinazopatikana huko majuu wanakokimbiliaga.

3. Kuna watu wanakimbiza watoto wao kusoma nje bila kuboresha elimu yetu.
 
Dah! Hii korona ikija huku na vile navyopenda kuzurura hiyo lockdown nitaenda kuielewa kaburini.
 
mwakimu mkuu corona. yeye anafundisha kuanzia wasiojua kusoma mpaka mainjinia hajacha madaktari na hakuwatenga wanasisa wote waanlishwa darasa
 
Back
Top Bottom