Corona imewapiga chenga ya mwili Manabii na Mitume bandia

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,824
Kutabiri si jambo la mchezo ni karama na kipawa cha kipekee mno. Usijaribu kutabiri kwakuwa kuna mwelekeo wa matokeo fulani. Usitabiri kidunia. Tabiri kiroho. Niulize mimi nilipotabiri Simba itashinda NNE nunge. Ndoto yangu ya utabiri iliniingiza chaka mpaka leo najiuliza kwanini ile ndoto ikanifanya vile.

Labda kwakuwa mass trending ilionesha wazi Simba itamchapa Yanga tena kwa mabao ya kutosha kutokana na Simba ilivyokuwa fit kwenye ligi huku Yanga ikichechemea.

Tuna watabiri wa kila mwaka. Yaani mwaka unapoanza wao huweka utabiri wao huku wakisema wameshushiwa maono. Hawa ni wale Manabii na Mitume bandia janja janja wanaosafiria nyota ya mwelekeo wa mambo. Watabiri wa kidunia hawa kwa koti la dini.

Kuna utabiri wa Bible ulioitabiria Italy vifo vingi na mpaka mahali pakatajwa lakini watabiri wetu janja janja wakazibwa macho na ufahamu wasijue lolote kuhusu huu utabiri.

Manabii na mitume bandia bandia wa kutumainiwa duniani kote wanaojaza makanisa yao maelfu kwa maelfu ya waumini hawakufua dafu kwenye hili. Kwakuwa hawa si halisi ni bandia na bandia hainaga ukweli hata mara moja. Corona imethibitisha uwezo wao mdogo. Na wale waliojaribu kusema Corona inapona kwa imani saa hii wanaendelea kuoza hawapo tena!

Dini ni kitu kizuri. Imani inahitajika sana ili kuleta usawa duniani. Lakini shida ni hawa viongozi wa hizo dini. Nawe usianguke kwenye blind face. Imani bila ufahamu wa kutosha ni mzigo mzito sana.

Watenda miujiza, wanaofanya maajabu ya kuponya, kutoa utasa kuleta utajiri nk. Huu ulikuwa wakati wao sahihi wa kuonesha uwezo wao wa uponyaji. Lakini kwa bahati mbaya sana kipindi hiki wamekutana na kisiki chenye mizizi mirefu.

Jr
 
Maadiko lazima yatimie kama mwana wa mungu aliedhaliwa na bikira alikamilisha unabii nyinyi ni nani naniyo trop sijui troph uko USSR kaz ipo
 
Mshana Jr,
FB_IMG_1586549224178.jpg
 
Wote wako mafichoni huku wakichungulia kwa mbali, wakiitumia madhabahu kukusanya vya wajinga waingiao kwenye makanisa yao bila barakoa wakiamini miujiza ya uponyaji.

Sent from my TA-1024 using Tapatalk
 
Back
Top Bottom