COPY & PASTE BUDGET: Hivi Serikalini Hakuna THINK TANG?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

COPY & PASTE BUDGET: Hivi Serikalini Hakuna THINK TANG??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kachanchabuseta, Jun 12, 2010.

 1. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  WanaJF Naomba ushauri

  Nimepitia budget ya 2010/11 nimeona hakuna jipya ndo mana nikajiuliza hivi kwanini serikali haitumii Think Tank kama wataramu wetu wa vyuo??
  Tatizo la Serikali yetu ukijifanya unajua sana wanakokorimba, wanakubaregu na kukuchachage. kwa mtindo huu TAnzania will Never nevr develop.

  Budget 2010/11
  Kodi imepungunzwa from 15%-14% anbayo TShs 1000 kwa mwezi kwe mwaka 12,000 HAPA HAKUNA KITU.

  Mishahara imepanda kwa Tshs 1200 kwa mwezi kwa mwaka tshs 14400 MAISHA GANI HAYA KWA WATANZANIA??

  Vyanzo Vya Mapato=0

  Siku zote unaweza kufikiri serikalini wamekaa viraza na mabwege yaani kila siku sehemu ya kupata mapato ni sigara sida bia

  Nashauri mapaparazi wa Serikali watembelee JF mara nyingi wapate ufumbuzi wa matatizo yao

  Ndo hilo tu wana JF
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Jun 12, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mkuu labda uko nje ya serikali, kuna vilaza wengi na wavivu. Nenda kaangalie budget za vyuo vukuu utashangaa, ni copy, cut & paste hakuna mabadiriko ktk budget documents kwa miaka kama 40 na wataalamu hawa ndo wanajifanya wako busy kweli kumbe hakuna lolote.
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Kibaya zaidi, ukiacha hayo mambo ya kupanda mishahara na kodi, kwenye mapato na matumizi ya serikali ni mchezo wa redio mtupu, wanatoa figures kufurahisha watu tu, lakini hazina hata maana, bora hata ya mchezo redio unaweza kuwa na mafunzo. They do cook up the books.
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Jun 13, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ni ukweli mtupu wamejaa vilaza kwa sababu ni majuzi tu Wafanyakazi wa serikali wameomba ongezeko la mshahara kiasi kwamba imetumika sheria ya Udikteta. Hawa watu walitakiwa kukaa na kujiuliza wataweza vipi kuponyehsa hali hii na sio kuwaadhibu kwa sababu kupounguza kodi kwa asilimia moja ni kufikiria zaidi matumizi ya serikali badala ya wananchi wenyewe.

  Mfano mdogo:-
  Kama serikali ingeweka kiwango cha hawa wenye mishahara ya chini ongezeko la asilimia hata iwe 20 kinyume cha maombi ya Tucta,
  2. Kuwepo na msamaha wa kodi kati ya mshahara wa chini hadi tuseme laki 2 na nusu..
  3. Wale wa mishahara ya juu hadi laki 6 ikabakia na kodi zile zile pasipo pungufu au Ongezeko.
  Na 4. wenye zaidi ya hapo ingeongezwa kodi zaidi kwa asilimia moja au mbili kufikidia pato la chini.

  Hii ingeweza kutoa picha nzuri kiasi kwa kuzingatia kwamba unapowapa wananchi fedha zaidi mfukoni ndivyo wanavyoweza kuzitumia na mzunguko wa fedha kuwa mkubwa ambako pato la kodi hukusanywa lakini mshahara unavyopungua ndivyo wananchi wanavyoshindwa/kuogopa kutumia fedha zao na mznguko kuwa mdogo.
  Kisha ongezeko la mishahara huhamasisha wananchi kutafuta kazi zaidi ya kuganga mtaani..Vijana wengi sana nimekutana nao hawataki kufanya kazi kwa sababu kazi hazilipi hivyo ni bora kuganga njaa na umachinga au Udalali ambao hauna kodi.

  Kilichonikera zaidi ni pale serikali ilipoondoa kodi za mafuta kwa mashirika ya uchimbaji madini (ya nje).. Hii hata sisi Conservative wakuu zangu hatupendelei Matajiri kwa mtazamo huu hata kidogo. Ila tunatazama matajiri wawekezaji kuyawezesha mashirika mengine ya ndani kuweza kufanya biashara pia. Huwaruhusu mashirika ya nje ili kuongeza ajira za ndani. Lakini unapokata kodi kwa mashirika haya ina maana mashirika ya madini hawana sababu ya kutumia Umeme wa Tanesco kwani hawawahitaji, hivyo tunazidi kulidhoofisha shirika hilo.

  Ukiangalia hata Usafiri TRA umeshindwa kutumika kwa sababu serikali inawawezesha mashirika haya kufanya kazi zao kwa kutumia mashirika ya nje. Barricks hawana magari wala hawategenezi magari. Mradi wa Usafirishaji wanawapa mashirika ya nje wakidai ni magari yao, mara nyingi kazi kubwa kama hizi huwa kuna mashrika kama manne ndani yakishirikiana kuwezesha Uchimbaji mzima. Hata mradi wa maji ni wao wenyewe hii kweli tunakusanya kitu gani toka kwao..

  What fools us ni kuona nembo za Barricks ktk magari na vifaa vingi wanavyotumia kila siku most of them are supplied na mashrika ya huko huko Ulaya wanaingia mkataba na Barricks na masharti ya kutumia nembo yao wakati huku kwetu mashirika kama hayo yanakufa..Hii inapunguza ajira kwa mashirika yetu na hakika hakuna mnyororo unaounganisha ongezeko la ajira.

  Ukiangalia kasheshe la BP Shell huko Lusiana limewashinda Wamarekani kutoa maamuzi ya haraka kwani ktk mradi huo kuna mashirika matano mengine makubwa ya Kimarekani ambayo yana hisa na uchimbaji Mafuta hayo.

  Hivyo tunaposoma BP Shell na mradi ya Offshore drilling mawazo yetu yote yanakwenda BP Shell shirika la Kiingereza lakini hatujui kwamba BP kuwezeshwa kufanya hivyo imetoa kazi nyingi kwa mashirika ya ndani Marekani hivyo kuongeza mchango mkubwa ktk ajira.

  Hivi ndivyo sisi Conservative tunaangalia, tunaangalia mchango wa shirika katika kuzalisha ajira ndani na kuyawezesha mashirika yetu ya ndani kupata tender...Sio kila kitu tunahitaji wawekezaji hivyo tulegeze masharti pasipo kuangalia trickle down of such investment.
  .
   
 5. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Asante mkuu lakini kwa manufaa ya taifa Serikali ni azina ya watu kwa hiyo haina budi kuwatumia VILAZA HAWA NDO WANAARIBU NCHI
   
Loading...