Basi wanajamvi na "harakati za komputa" wazidi kuwa na nguvu, na wapongezwe, kama ndivyo.
Lakini wakati tunapima ufanisi na tija ya mchango wa JF, ingependeza tujue wana JF walifanya nini katika kuzuia majengo haya yasiendelee. Katika maandamano ya wakazi wa eneo hilo kulikuwa na bango la JF? Au katika pingamizi rasmi lililoletwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wanaharakati wa JF wametajwa kama wadau? Au wanaharakati wa JF ndio waliowashtua watu wa makazi hayo kwamba kuna ujenzi unaendelea kinyemela amkeni? Au JF walienda wizara ya Ardhi kushinikia ujenzi usiendelee, ni vipi yani?
Tutaidie, wewe umejuaje wana JF ndio wamesababisha kusimamisha ujenzi huu?