mayowela
JF-Expert Member
- Nov 2, 2014
- 2,124
- 1,746
Tumeshasikia kitu wanaita ujasiliamali wa maudhui (content enterpreneurs), hii ikoje?
Hii ni biashara kama biashara zingine na wengi wanafanya na wanapiga mpunga wakutosha. Kuna baadhi ya wadau nimewataja hapo juu wanafanya hii kitu na wengine wengi.
Inafanyikaje?
Kinachofanyika watu hurekodi vipindi vya redio au TV na kuviuza kwenye media houses au kuingia ubia na kugawana kinachopatikana.
Ninaowafahamu wanafanya biashara hii ni , Sky Walker (Fredrick Bundala), Millard Ayo, Dorin Noni, Salama Jabir, Oka and Carpoza na wengine wengi.
Kuna vipindi ambavyo watu hujiuliza mbona kipindi flani siku hizi hakiruki tena, au mbona kinarushwa na TV mbili tofauti, au flani mbona karekodi kipindi kimeenda you tube na kwenye TV kinaruka.
ON AIR with Millard: Kinaruka Clouds Plus ni kwa mkataba; kuna kipindi itafika mkataba utaisha na kipindi kinaweza endelea au kikasitishwa, ile Content ni ya Millard sio Clouds Plus, wao wamenunua.
WOMEN MATTERS: Inaruka Wasafi TV kile ni kipindi idea ni ya Sky Walker na mkewe ila baadae Wasafi walikipenda na dili likafanyika.
SALAMA NAA: Hii ni Idea ya amabayo inaruka kwenye akaunti ya YouTube ya salama pia inaruka EATV.
MEZA YA USHINDI: Ni kipindi kinachoruka Classic FM kikitangazwa na Sky Walker, lakini pia kwa kauli yake kipindi hicho kinaweza ruka hata redio zingine endapo kutakuwa na makubaliano kama ilivokuwa kwenye CHILL NA SKY ilikuwa ikiruka redio nyingi za mikoani.
Hata wewe unaweza ukaja na wazo zuri ukalifanyia kazi na ukalipeleka kwenye media; wakikubali wataingia makubaliano na wewe na utakuwa unapiga mpunga wa kutosha tu.
Kama kuna addition ya wajasiriamali wa maudhui unaweza ukawaongezea.
Ahsante.