Conte amtema Diego Costa kwa meseji

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292

upload_2017-6-8_12-57-15.jpeg

London, England. Mshambuliji wa Chelsea, Diego Costa amesema ametumiwa ujumbe mfupi wa simu kutoka kwa kocha Antonio Conte akitakiwa kutafuta maisha sehemu nyingine.

Ndoto za Costa kubaki kwenye Uwanja wa Stamford Bride zimezimwa na kauli hiyo ya kocha ambaye hivi sasa yupo kwenye harakati za usajili kwa ajili ya kukisuka kikosi chake.

Taarifa za mchezaji huyo kuondoka kwenye klabu hiyo mabingwa wa England msimu ulioisha, ziliaanza kuripotiwa kwenye vyombo vya habari kabla hata ligi hiyo kumalizika.

Costa alikuwa anahusishwa kuhamia Ligi Kuu ya China hata hivyo hivi karibuni alibadili mawazo na kutanga kwamba angependa kuendelea kubaki England.

Nafasi yake kubaki Chelsea imekuwa ndoto kutokana na uongozi huo kuongeza kasi kumsajili mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku.

Mchezaji huyo mwenye miaka 28 amepewa taarifa za kutokuwapo kwenye mipango ya Conte jambo lililomfanya kuiwa njiapanda.


“Nimetumiwa ujumbe mfupi kwenye simu kutoka kwa Conte akisema sipo kwenye hesabu zake za msimu ujao” alisema Costa alipokuwa akizungumza na waaandishi wa habari wakati timu yake ya Hispania ilipotoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Colombia jana Jumatano.

Costa alisema huenda kocha wake amechukua uamuzi huo kutokana na kufanyua vibaya msimu uliopita
 
ni muda wa wenga kumchukua kwa bei zake za rejareja
 
ila mpunga upoo?? maana jana ilisikika kuwa madrid waliwachomolea nje man u kwenye dili la morata
Madrid wanawadindia Man Utd kwa kuwa labda wanataka Dea Gea awemo somehow kwenye deal. Morata hawamtaki kihivyo, ndo maana alikuwa anaaingia dakika za majeruhi na yeye hataki tena kusugua benchi. Madrid wanamtaka zaidi yule dogo wa Monacco - Kylian Mbappe
 
Madrid wanawadindia Man Utd kwa kuwa labda wanataka Dea Gea awemo somehow kwenye deal. Morata hawamtaki kihivyo, ndo maana alikuwa anaaingia dakika za majeruhi na yeye hataki tena kusugua benchi. Madrid wanamtaka zaidi yule dogo wa Monacco - Kylian Mbappe
Ahaa sawa mkuu
 
Back
Top Bottom