Connection Jiko Janja la umeme bei nafuu zaidi ya majiko yote ni (Induction Cooker)

Ni kweli lina ufanisi kuliko jiko la gesi? Ni kweli linaweza kuwa economical kuliko jiko la gesi?
Ndio kama unatumia pans na sufuria zake maalum. Jamaa kakata maelezo nusu ukitaka sufuria lako la aluminium utaenda Rwanda na kurudi msosi bado na unamaluza umeme wote
 
Ndio kama unatumia pans na sufuria zake maalum. Jamaa kakata maelezo nusu ukitaka sufuria lako la aluminium utaenda Rwanda na kurudi msosi bado na unamaluza umeme wote
INDUCTION COOKER zinatumia sufuria zenye asili ya chuma (stainless steel) ni masuria tunayotumia majumba mwetu pia siyo watu wote wanaotumia mafuria ya aluminium (ambayo si salama kwa afya yako).
 
Ndio kama unatumia pans na sufuria zake maalum. Jamaa kakata maelezo nusu ukitaka sufuria lako la aluminium utaenda Rwanda na kurudi msosi bado na unamaluza umeme wote
Ukweli ni kwamba kama unatumia sufuria ambayo siyo ya chuma stainless steel jiko linazima baada ya sekunde chache kwa maana hiyo utakuwa utumii umeme wowote wakati huo.
 
Induction cooker ni majiko mazuri sana.

Ukitoa sufuria linazima. Pia unaweza set muda wa kujizima.
 
  • Thanks
Reactions: 1x1
__opt__aboutcom__coeus__resources__content_migration__treehugger__images__2016__07__cookingcom...png
 
Nimetumia jiko janja kwa zaidi ya miaka 2 sijapata shida yoyote.Na ukitumia power meter kupima kiasi cha umeme unaotumika kupikia kwa muda wa kama masaa mawili ni chini ya unit mbili.Kwa kweli ni jiko zuri linapunguza sana gharama za nishati nyinigine kama gesi na mkaa.Pia linapika kwa haraka sana ukilinganisha na gesi au mkaa.
 
Mimi ninalo kwa zaidi ya miaka miwili na sijapata tatizo lolote.Pia lina option ya kuweka timer ili lizime baada ya muda fulani kuzuia kuunguza kama uko mbali.
Mkuu kama hutojali tuma na picha ya hilo lako basi.
 
Screenshot_2023-11-09-22-07-38-505_com.alibaba.aliexpresshd.jpg

Mkuu nimecheki huko AliExpress, jamaa wanadai et ukiwekea umeme wa 110V linalipuka, hivi hapa kwetu ni ngapi asee.
dronedrake Mkuu karibu, hivi haya majiko ukipata hilo sufuria la chuma ni kweli ni alternative ya gas.
Au jamaa wanafanya biashara tu.
 
Mkuu nimecheki huko AliExpress, jamaa wanadai et ukiwekea umeme wa 110V linalipuka, hivi hapa kwetu ni ngapi asee.
kwetu ni 220V, mengi ni smart, yakipata umeme mdogo hayawaki kabisa

Mkuu karibu, hivi haya majiko ukipata hilo sufuria la chuma ni kweli ni alternative ya gas.
Au jamaa wanafanya biashara tu.
Gas cooker iko fasta zaidi ya Induction, kwa gharama sikupata kupiga hesabu
ila nyama ya 1kg, gas cooker yangu(yenye burner iliyo na rings 2 zile za kutolea gesi) inamaliza kila kitu ndani ya dk 25, Induction inakimbilia dk 45-50 huko
 
Back
Top Bottom